Kuelekea uchaguzi mkuu 25/10/2015, makada hawa wapo hatarini

By. Martin Madafa

HALI ya kisiasa ni mbaya kwa sasa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika wiki mbili zijazo yaani 25/10/2015, viashiria vya uvunjifu wa amani vimejikita ndani ya chama cha mapinduzi kwa ubia wa vyombo vya dola nchini., Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinasema makada wa UKAWA John Mrema, Yericko Nyerere na Reginalnd Munisi kwa zaidi ya mwezi sasa wanawindwa na vyombo vya dola kwa siri kubwa kwa shinikizo la kisiasa (ccm). Makada hao ndio wanaoongoza idara ya mikakati ya ushindi ya ukawa.

Taarifa hizi zinakaziwa na kutoweka kwa kada wa Chadema Yericko Nyerere, Tangu siku ya jumatatu ya tarehe 15/9/2015, Yericko hajaoneka hadharani wala kwenye mitandao yakijamii jambo linalozusha wasiwasi mkubwa hasa kwa vijana ambao niwafuasi wake mitandaoni na katika siasa nchini, simu zake zote 0755865544 na 0715865544 zote hazipatikani, pia taarifa za kuaminika toka kwa majirani zake huko kigamboni zinasema nyumba yake imetelekezwa.

Katika ukurasa wake wa facebook tarehe 16/9/2015 Yericko aliandika kuwa “Jeshi la polisi jana usiku limefanya uvamizi nyumbani kwangu, kwa bahati mbaya mimi sikuwepo, lakini kiongozi wa uvamizi huo aliponipigia simu alisema wanahitaji kuchukua maelezo yangu, Wiki mbili zilizopita alinipigia simu ZCO Mr Mbuta, akaoomba kuonana na mimi, nilimuuliza ni mazungumzo ya kawaida au ya kiofisi? Akajibu ni yetu ya kawaida tu, ieleweke kuwa ninafahamiana na huyu Mh na nimarafiki, hivyo kwakuwa nipo kwenye kampeni nilimweleza kywa nikimaliza kampeni nitakuja mh, Lakini kumbe nyuma ya pazia kulikuwa na hili, Ushauri wangu, jeshi la polisi liache kutumika kisiasa”, Hii inaonyesha Yericko anamahusiano ya karibu na vigogo wa hao wa dola nchini, kama anafahamiana nao, ilikuwaje avamiwe usiku na wavamizi wakajitambulisha wametumwa toka ikulu? Kuna utata mkubwa juu ya hili.

Taarifa toka ndani ya ccm zinasema kuwa vigogo wa chama hicho kuna nyaraka muhimu za MKAKATI ya USHINDI wa UKAWA wanazozitafuta kwa mda mrefu sana, sasa kupitia kwa aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema Dr Slaa ambae kwa sasa ni mpiga kampeni wa Magufuli, aliwadokeza kuwa wakitaka kuipata nyaraka hiyo wamuone Yericko ndie aliyeandaa, inatajwa kuwa tayari walishatumia mbinu nyingi ikiwemo kujaribu kumshawishi kupitia kwa marafiki zake lakini kijana huyo alionyesha kukataa. Inaelezwa kuwa mswada wa mkakati huo awali alikabidhiwa Dr Slaa kabla hajajiuziru na kuasi chama hicho,

Kada wa ccm ambaye hakutaka kutajwa anasema, “Dr ametueleza kuwa mkakati huo aliupokea kutoka kwa mwandaaji (Yericko) akaenda nao nyumbani , baada ya siku chache akajiuzuru ukatibu. Anazidi kusema kuwa baada tu ya kujiuzuru Dr alizima simu zake zote na akawa na namba mpya ambayo alikuwa akiwasiliana na mshauri wake Yericko Nyerere tu kwa zaidi ya siku tatu. Nikipindi hicho ndicho Yericko alikutana na Dr nyumbani kwake aliuchomoa mkakati huo hali iliyopelekea Dr kukosa nyaraka yoyote mhimu yakuwavuruga ukawa”, Inasadikiwa kuwa hata Mwenyekiti Mh Mbowe alilazimika kuwasiliana na Dr Slaa kupitia kwa Yericko katika kipindi kile cha mgogoro.

Viongozi wa Chadema hakuna aliyepatikana na kulizungumzia kwa undani hili, lakini Mh Mbowe alipoulizwa alisema, “tunatambua hila zote dhidi ya watu wetu, tunalionya jeshi lapolisi na ccm kuheshimu uhuru, haki ya mtu kuishi na kufikiri” simu yake ikakatwa na alipopigiwa tena hakupokea. Mtandao huu umeweza kuona mkakati huo wenyekichwa kisemacho “THE PEOPLES’ AMANDLA ELECTORAL VICTORY THE ROAD TOWARDS IKULU” unaonyesha umeandikwa na Yericko Nyerere ukiwa na kurasa 150 kwa lugha ya Kiswahili na kiingereza.

By Yericko Nyerere

Kwamfumo wa utendaji wa Idara ya Usalama wa Taifa, Viongozi wa kisiasa wapo SALAMA.

By:  Yericko Nyerere

Nataka kuzungumza dhana ngumu kidogo machoni pawengi, lakini hima nitaeleweka bila mawaa wala chembe ya makunyanzi. Nazungumza kama mtaalamu wa mifumo ya kiulinzi duniani hasa nikiangaza mifumo ya kiusalama ya Franks Secur, Westm secur, Latino secur, Kremlin secur.

Siasa tuiache kando utaalam uchukue nafasi yake, na hapa nataka tujikite kuuangalia mfumo wa utendaji kazi wa idara ya Usalama wa Taifa na vyombo saidizi vyake katika kulitumikia taifa la Tanzania chini ya Westm secur

Usalama wa Taifa Tanzania ni idara iliyochini ya Ofisi ya Rais, hii inamaana kuwa mkuu wa idara hii anaripoti kwa rais mojakwamoja, pia mkuu wa idara hii huteuliwa na rais kwakuzingatia vetting maalumu iliyochini ya command ya ndani.

Muundo wa utendaji wa idara hii umegawanyika katika sehemu kuu sita, ambazo ni idara ndogondogo ndani ya idara hiyo kubwa nazo ni idara ya mambo ya ndani, idara ya siasa, idara ya mambo ya nje, idara ya ichumi, idara ya ukusanyaji taarifa, idara ya uchakataji taarifa na idara ya vita.

Hapa nataka kuzungumzia idara ya siasa ambayo ndio tunayokumbana nayo mtaani kila kukicha na tunashirikiana katika maandamano nk,

Idara hii nayo ina vitengo mhimu vya kiutendaji ikiwemo ulinzi wa chama na serokali, sera za kisiasa na muundo wa siasa kutegemeana na chama kilichopo madarakani wakati huo.

Pia idara hii inajukumu la kufuatilia na kutambua mienendo ya wanasiasa viongozi na wale wote watu maarufu katika taifa, bila kusahsu kufuatilia mawasiliano yao, baruapepe zao, mizunguko yao ya kila siku, vyakula vyao vya kila siku, vipato vyao nk.

Idara hii pia imepewa jukumu la kuwalinda viongozi wa kisiasa (mawaziri na wabunge) kwa saa 24 bila kukoma. Mfano, Rais hulindwa na watu 40 wanaoonekana na 48 wasioonekana, hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def S2).zingatia kukiwa na hali ya hatari (Def Cond) kiwango cha ulinzi huongezeka.

Makamu wa Rais hulindwa na watu 15 wanaoonekana na 10 wasioonekana, hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def S2).zingatia kukiwa na hali ya hatari (Def Cond) kiwango cha ulinzi huongezeka

Waziri mkuu hulindwa na watu 15 wanaoonekana na 8 wasionekana hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def S2) zingatia kukiwa na hali ya hatari kiwango cha ulinzi huongezeka.

Mawaziri hulindwa na watu 3 wanaoonekana, na 5 wasioonekana, hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def s2).

Majukumu ya walinzi wanaooneka na wasioonekana yanatofautiana na kila mtu kati yao huripoti kwa boss wake,
Wale walinzi wanaoonekana huripoti kwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, na wale wasioonekana huripoti kwa rais kila mmoja kwa wakati wake bila wao kujuana.

Hii inamaana kuwa kila anachotaka kufanya ama anachofanya waziri yoyote kabla hajakitenda basi taarifa huwa mikononi mwa rais na mkurugenzi wa Usalama nchini.

Wale wanaoonekana wanaomlinda Rais huripoti kwa mkurugenzi na mnadhimu, wale wasioonekana 10 huripoti kwa rais moja kwa moja, na 30 huripoti pande zote tatu lakini kwa umakini mkubwa bila kujuana.

Mpendwa msomaji, sio nia yangu kusafisha wanasiasa, bali nia yangu nikukuelezeni kitaalamu mfumu wa ulinzi nchini unavyoendeshwa na madhari ya kisiasa kuwa waziri fulani ni mwizi ama fisadi kwa dhana ileile ya kisiasa.

Kwenye medani ya siasa huko kuna filosi tofauti kidogo ambayo hutafsiri uwajibikaji kisiasa katika dhana inayokinzana na uhalisia wa kiutaalam katika mifumo ya kiulinzi.

Hapo sijazungumzia intelligence ya jeshi la polisi ambayo nayo ni mdau, pia sijaigusa Tanzanian Military Intelligence ambayo ndio mwamuzi wa mwisho katika muktadha wa taifa hili..
“Kuna watu wasipokuelewa maneno na matendo yako, mshukuru Jah, wewe bado unafikra chanya, wakianza kukuelewa jichunguze ni wapi umeanguka maana umeanza kuwaza kama wao

By Yericko Nyerere

DB Cooper Research Team, kikosi cha uchunguzi kilichovunja rekodi ya dunia

Kwa wale wapenzi wa tamthilia ya Prison Break watakuwa wanakumbuka katika msimu wa kwanza wa tamthilia kipindi muhusika mkuu wa tamthilia Michael Scofield akijaribu kuwashawishi wafungwa kadhaa aliowachagua wamuunge mkono kwenye mpango wake kabambe wa kutoroka kutoka katika gereza la Fox River, kulikuwa na mzee wa makamo aliyeitwa Charles Westmoreland ambaye alimpa changamoto kubwa kukubalia kujiunga na mpango huu.

Watu ambao Micheal aliwachagua kila mmoja alimteua kwa sababu maalumu kutokana na umuhimu fulani alionao ambao utahitajika katika kufanikisha tukio la kutoroka. Mfano alimchagua cell mate wake Fernando Sucre ili aje kuwasaidia katika mpango wa kuingia nchi ya Mexico kiurahisi baada ya kutoroka, alimchagua John Abruzzi ili aje kusaidia kupata usafiri wa ndege watokomee pindi tu wakitoroka Fox River, na wengineo wote waliojumuishwa kwenye mpango huo walikuwa na umuhimu maalum.

Kujumuishwa kwa Charles Westmoreland kwenye mpango huo ni kutokana na Michael kung’amua mapema kwamba watahitaji fedha za kujikimu mara tu wakifanikiwa kutoroka na hatimaye kuingia nchini Mexico.

Swali je, fedha wanapata wapi? Ndipo hapo anapoingia Charles Westmoreland, ambaye licha ya kutumia jina hili la Charles Westmoreland, Michael Scofield aliamini kuwa huyu mzee ni D.B Cooper jambazi aliyefanikiwa kuiteka ndege na serikali kukubali kulipa dola milioni moja ili aiachie, jambazi ambaye mpaka mda huo alikuwa bado anatafutwa na FBI, jambazi pekee aliyefanikiwa kuweka historia katika nchi ya marekani kufanya tukio la utekaji ndege kwa mafanikio na kesi kushindwa kuwa kuwa solved na FBI kwa miaka 45! Licha ya Charles Westmoreland kukataa katakata kuwa yeye siye D.B Cooper lakini Michael aliamini yeye ndiye na fedha alizofanikiwa kulipwa na serikali bado hajazitumia ziko mahali fulani amezificha..

Baada ya majaribio kadhaa ya kumshawishi kushindikana, mwishoni kabisa Charles anakubali kuungana katika mpango wa kutoroka baada ya kugundua kuwa hatopewa fursa ya kumuona binti yake aliyekuwa anaumwa na ana karibia kufa, na kuthibitisha hilo anamuonyesha Michael noti ya fedha ya marekani yenye serial number D 1192589 ambayo ni moja ya noti katika fedha alizolipwa na serikali ili aweze kuiachia ndege aliyoiteka na baadae kabisa anakiri kwa Michael kuwa hakulipwa dola milioni moja kama inavyoripotiwa kwenye vyombo vya habari bali alilipwa dola milioni tano.

Katika msimu wa pili wa tamthilia sehemu kubwa inahusu jinsi wafungwa waliofanikiwa kutoroka (Michael, Burrows, T-bag, Sucre e.t.c) wanavyofanya juhudi ili wazipate November Charles Westmoreland (D.B Cooper) katika eneo la Utah.!

TUKIO LA KWELI KATIKA MAISHA HALISI.

Siku ya November 24 mwaka 1971, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mji wa Portland jamaa aliyevaa suti nyeusi na koti refu jeusi kwa juu akiwa amebeba brief case nyeusi alifika katika counter ya kampuni ya ndege ya Northwest Orient Airlines na akatoa fedha cash dola 20 kununua tiketi ya ndege Flight 305 kwenda mjini Seattle, ambayo kwa kawaida ni safari inayochukua dakika 30. Jamaa huyu alijitambulisha kama ‘Dan Cooper’.

Baada ya kuingia kwenye ndege akakaa kwenye siti namba 18C, baadae akakaa siti namba 18E na baadae 15D.

Ilipofika mida ya saa nane na dakika hamsini mchana ndege ikaruka na baada ya ndege kuruka Mr. Cooper akawasha sigara na akaagiza soda!

Siti ambayo alikaa Cooper ilikuwa siti ya nyuma kabisa na alikaa karibu kabisa na siti ya muhudumu wa ndege wa kike aliyeitwa Florence Schaffner.
Baada ya dakika chache Cooper alitoa kikaratasi mfukoni kilichochapwa kwa unadhifu na maandishi yakiwa yameandikwa kwa herufi kubwa na kisha akampatia Bi. Schaffner kikaratasi hicho.

Baada ya Bi. Schaffner kupokea kikaratasi, kutokana na mazoea akajua ni kawaida tu abiria alikuwa ametokea kumtamani na hivyo amempa namba ya simu, kwa hiyo Bi. Schaffner hakukisoma kikaratasi bali alikiweka moja kwa moja kwenye mkoba. Mara baada ya kukiweka kikaratasi kwenye mkoba, Cooper akainama kidogo na kumnong’oneza Bi. Schaffner na kumwambia “Miss you would better take a look at that note. I have a bomb” (Bibie ni vyema ungekisoma hicho kikaratasi. Nina bomu).

Baada ya kumueleza hivyo kimya kimya akamuamuru muhudumu huyo akae karibu nae na kuanza kumpa maagizo. Lakini kabla ya hapo yule mhudumu akataka ampe uhakika kama kweli ana bomu. Cooper akachukua briefcase yake na kuifungua kidogo tu ili muhudumu aangalie na alipoangalia ndani ya briefcase akaona cylinders nane, nne zikiwa chini na nne zikiwa juu zikiwa zimeunganishwa kwa nyaya nyekundu ambazo nazo zinaenda kuunganika kwenye battery yenye rangi nyekundu pia ikiyopo pembezoni mwa briefcase. Baada ya kuchungulia muhudumu akaamini kweli Cooper alikuwa na Bomu.

Cooper akampa maagizo muhudumu akaongee na marubani kwa kupitia intercom kuwa wawasiliane na uwanja wa ndege wa Seattle na wawaeleze juu ya ndege kutekwa na mtu mwenye bomu na yuko tayari kulipua ndege hiyo na abiria wote 36 na watumishi wa ndege 6 waliopo umo ndani.. (Ndege ilikuwa haijajaa yote, ilijaa kama theluthi moja tu (1/3)).

Ili asilipue ndege hiyo Cooper alihitaji apewe ‘Fedha halali za kimarekani’ dola 200,000 (msemo huu ‘fedha halali za kimarekani’ utakuja kuleta maana sana huko mbele kwenye upelelzi wa FBI). Pia aliamuru apewe parashuti nne na ndege itakapofika uwanja wa ndege wa Seattle kuwe na gari ya kujaza mafuta inasubiri ili ijaze ndege mafuta na kumpeleka sehemu atayoitaka.

Muhudumu Bi. Schaffner akawasiliana na mapilot na kuwahakikishia kuwa ni kweli jamaa ana bomu na akawapa orodha ya vitu alivyokuwa anavitaka.

Baada ya kupewa orodha ya demands za Bwana Cooper, marubani wakawasiliana na uwanja wa ndege wa Seattle na watu wa uwanja wa ndege wakawasiliana na vyombo vya ulinzi na baada ya mtiririko wa mawasiliano kati ya uwanja wa ndege, wamiliki wa ndege na vyombo vya ulinzi kufanyika wakakubaliana kuwa ili kuepusha hasara ya kibiashara na kupoteza maisha ya watu 42 ni vyema wakampatia mtekaji anavyovitaka lakini vyombo vya ulinzi vitaangalia kama kutapatikana fursa yoyote waweze kumkata au kumdungua mtekaji huyo.

Hivyo basi wahudumu wote waliopo kwenye ndege waliamuliwa wampe ushiriakiano Cooper ili kuepusha hatari yoyote na pia wamueleze kuwa awape mda kidogo ili kukamilisha kupata vitu alivyokuwa anavihitaji.

Baada ya jibu hilo kurudishwa juu kwenye ndege na marubani kuwasiliana na muhudumu Schaffner kupitia intercom, muhudumu alirudi kwenye siti aliyokaa Cooper na alikuta sasa amevaa miwani meusi ya jua na yuko amerelax kabisa bila presha wala wasiwasi wowote! Akampatia jibu walilopewa kutoka chini kwenye uwanja wa ndege.

Baada ya kupewa jibu hilo Cooper akaitikia kwa kichwa kisha akawasha sigara nyingine na kuagiza Soda nyingine na maji ya kunywa, na kwa mshangao akalipia na chenji iliyorudi akampa ‘tip’ muhudumu Schaffner.

Muda wote huu abiria wengine walikuwa hawajui kinachoendelea ndani ya ndege na ili kuepusha wasije wakapata wasiwasi kutokana na kuchelewa kutua wakatangaziwa kuwa kulikuwa na tatizo la kiufundi hivyo itawalazimu wachelewe kutua mpaka tatizo litakapo shughulikiwa.

Kama nilivyoeleza awali kutoka Portland mpaka Seattle ni safari ya nusu saa kwa ndege lakini ndege ilikaa angani taribani masaa mawili ikiwa inazunguka tu ili kusubiria kule chini mamlaka usika ziandae vitu cooper alivyohitaji.

Ndani ya masaa mawili FBI walifanikiwa kukusanya noti za dola 20 zipatazo elfu kumi (jumla dola 200,000) kutoka bank za karibu na zote wakazipiga picha! Pia walifanikiwa kupata parashuti nne kutoka katika kituo cha jeshi la anga cha Tacoma kilichopo karibu na uwanja wa ndege wa Seattle! Baada ya kumaliza kufanya maandalizi yote haya mnamo majira ya saa kumi na moja dakika ishirini na nne wakawasiliana na ndege juu kumtaarifu Cooper kuwa vitu vyake vyote alivyohitaji viko tayari.

Baada kumpa orodha ya vitu hivyo Cooper akaamuru kuwa hataki parashuti za kijeshi anataka apewe parashuti za kawaida za kiraia na FBI wakafanikiwa kuzipata kutoka katika kituo cha kufunza watu skydiving.

Robo saa baadae (saa kumi na moja dakika 39) ndege ilitua katika uwanja wa Seattle na Cooper akamuamuru rubani aisimamishe ndege sehemu pweke na yenye mwanga wa kutosha. Pia akamuamuru rubani azime taa zote ndani ya ndege ili kuepusha wadunguaji (snipers) wa FBI kufanya yao.

Baada ya ndege kusimama mtumishi mmoja wa kampuni ya Northwest Orient Airlines aliyejulikana kama Al Lee akiwa amevalia kiraia ili kuepuka kumchanganya cooper asidhani ni askari akiwa amevaa sare za uwanja wa ndege, alikabidhiwa mabegi yaliyokuwa na fedha pamoja na maparashuti.

Al Lee akaisogelea ndege na Cooper akamuamuru muhudumu mwingine ndani ya ndege binti aliyeitwa Mucklow afungue mlango mdogo wa dharura pembeni ya ndege na kupokea mabegi hayo. Na Mucklow akatii.

Baada ya Cooper kuhakikisha kuwa fedha na kila kitu alichohitaji kiko sawa sawa akawaruhusu abiria wote washuke. Pamoja na abiria alimruhusu muhudumu Schaffner pamoja na muhudumu mwingine ambaye alikuwa anaonekana kuwa na umri mkubwa. Lakini akabaki na marubani wote wawili, yule binti mwingine muhudumu aliyeitwa Macklow pamoja na fundi wa ndege.

Kisha akaamuru gari la kujaza mafuta liletwe na kuwajazia mafuta.
Wakiwa wanawajazia mafuta Cooper aliwapa maagizo marubani kuhusu anakotaka waende na jinsi ambavyo anataka wasafiri. Kwanza akawaeleza kuwa anataka wafuate njia inayoelekea Mexico City na ndege iendeshe katika speed ya km 190/hour na ndege iruke umbali wa futi 10,000 kutoka ardhini.

Pia aliwaeleza kuwa anataka waondoe mgandamizo ndani ya ndege (cabin pressure) na wakiruka matairi yabaki kana kwamba wanatua, pia mlango wa nyuma ya ndege ubakie wazi kana kwamba mizigo inapakiwa na mabawa ya ndege ya pembeni yawekwe kwenye nyuzi 15.

Baada ya majadiliano kampuni ya Northwest Orient wakakataa ombi la cooper ndege iruke ikiwa imefunguliwa mlango wa nyuma mkiani au pembeni kwa madai kuwa itahatarisha usalama lakini Cooper kwa kujiamini kabisa akawaeleza kuwa ni salama na hakutaka kubishana nao sana kwani baada ya ndege kuruka tu aliufungua mlango wa pembeni mwenyewe.

Ndege iliruka kutoka kwenye uwanja wa ndege wa Seattle mnamo majira ya saa kumi na moja dakika arobaini ikiwa na watu watank pekee, yaani Cooper, muhudumu Macklow, fundi na marubani wawili! Watu watatu yaani fundi na marubani wawili walikuwa mbele kabisa kwenye chemba/chumba cha marubani kuendeshea ndege (cockpit) na Cooper pekee na muhudumu Macklow walokuwa kwenye sehemu ya abiria.

Mara tu baada ya ndege kuruka, ndege mbili za kivita aina ya F-106 kutoka kituo cha kijeshi cha McChord Air Force Base nazo ziliruka kuifuatilia ndege iliyotekwa na Cooper na ziliruka katika namna ambayo zisingeweza kuonekana na Cooper au mtu yeyote aliyeko ndani ya ndege, ndege moja ya iliruka juu nyingine chini ya ndege ya akina Cooper.

Baada ya mda kidogo kupita Cooper ali muamuru muhudumu aende mbele kwenye chumba cha marubani na akamfungia huko pamoja na wengine na akabaki peke yake katika sehemu ya kukaa abiria.

Takribani saa mbili kamili usiku alarm ikalia mbele kwenye chumba cha marubani kuashiria kuwa kifaa cha kufungua mlango wa nyuma kwenye mkia wa ndege kimehuishwa (activated). Dakika chache baadae sehemu ya nyuma ya ndege ilitikisika kwa nguvu na kuwa kama inainuliwa juu na marubaini wakabaini kuwa mlango wa nyuma kwenye mkia wa ndege ulikuwa umefunguliwa na ili kuepusha ndege isidondoke marubani iliwalazimu waishushe ndege chini na kutua kwenye uwanja wa ndege wa Reno, Nevada takribani majira ya saa nne na robo usiku.

Baada ya ndege kutua tu maofisa wa FBI na polisi waliizunguka na kuingia ndani kufanya upekuzi na ndani ya dakika chache wakagundua D.B Cooper hakuwepo ndani ya ndege.

MSAKO WA KIHISTORIA.

Baada ya FBI kujiridhisha kuwa Cooper hakuwa ndani ya ndege nadharia pekee iliyobakia ni kuwa aliruka ndege ikiwa angani kwani baada ya kuipekua ndege walikuta paradhuti mbili hazipo. Jambo la ajabu ni kuwa marubani wa ndege za kivita zilizokuwa zinaifuatilia ndege ya akina Cooper walisema kuwa hawakuona mtu akiruka kutoka kwenye ndege wala parashuti kufunguliwa.
Baada ya kutafakari kwa kina FBI wakaamua waitengeneza upya safari kama ile ile ambayo ilitokea siku ya tukio.

Hivyo basi kwa kutumia ndege ile ile na rubani yule yule FBI walorusha ndege kutoka uwanja wa Seattle kuelekea uwanja wa Rona, ndege ikiondoka Seattle muda unaofanana kabisa na ule ambao siku ile ya utekaji ndege iliondoka Cooper akiwemo ndani.

Kitendawili kikubwa ni mahali gani hasa ndipo kulikuwa na uwekano kuwa Cooper alitua ardhini. Lakini ili waweze kujua ni wapi alitua ilikuwa ni lazima wajua ni mahali gani ndege ikiwa angani aliruka na kufungua parashuti.

Na kitendawili kingine kama ikitokea wakagundua ni mahali gani angani ambapo aliruka itawapasa kung’amua ni muda gani Cooper alitumia kuwa katika ‘mdondoko huru’ (free fall) kabla hajafungua parashuti! Kwasabu mda mrukaji anaotumia kuwa katika free fall kabla hajafungua parashuti ‘inadetermine’ mahali anapotua ardhini.

Kwahiyo baada ya FBI kurusha ndege kutoka uwanja wa Seattle kuelekea uwanja wa Rona. Kwa kuzingatia maelezo waliyoyapata kuwa ndege ilitikisika majira ya saa mbili dakika kumi na tatu hivyo basi FBI wakafikia muafaka kuwa huo ndio muda ambao Cooper alifungua mlango wa nyuma ya mkia wa ndege na kuruka! Kwahiyo FBI nao wakarusha maafisa kadhaa katika usawa ule ule wa anga na walibakia katika free fall tofauti tofauti kabla hawajafungua maparashuti! Baada ya maafisa wote kutua wakatafuta mzingo (circumference) wa eneo hilo ambalo ndio eneo pekee lililokuwa na uwezekano wa Cooper kutua siku aliporuka.

Na baada ya kubaini ili eneo ambalo Cooper alitua, walibaini pia kuwa siku ya tukio eneo hili lilikuwa na mvua kali na kimbunga! Hivyo basi ukizingatia kuwa Cooper aliruka ndege ikiwa umbali wa futi 10,000 kutoka ardhini na siku ilikuwa na mvua kubwa iliyoambatana na kimbu na pia ilikuwa ni usiku wa giza totoro wakakubaliana kuwa hakukuwa na uwezekano wa Cooper kutua akiwa hai.

Pia walizingatia sababu nyingine kuwa kumbuka siku ya tukio Cooper aliletewa maparashuti ya kijeshi alafu akayakataa akadai apewe parushuti nne za kawaida na FBI wakenda kwenye kituo cha kufundisha skydiving na wakampatia. Sasa kwenye yale maparashuti manne, mawili yalikuwa kwa ajili ya kufundishia tu darasani na mawili ndio yalikuwa hasa yanaweza kutumika kuruka angani.

Kitu cha ajabu ni kwamba FBI wlikuja kugundua kuwa Cooper aliyaacha yale maparashuti mawili ambayo ndio yanayopaswa kutumia kurukia na na akaruka na yale mawili ya kufundishia darsani ambapo parashuti moja walidhani kuwa alivaa yeye na lingine alifunga begi la fedha.

Kwahiyo kama ilivyoelezwa awali kuwa siku hiyo ilikuwa na mvua kubwa na kimbunga kwahiyo FBI waliamini kuwa maparashuti hayo ya kufundishia yasingeweza kuhimili hali ya hewa ya siku hiyo na kumuwezesha Cooper kutua salama, hivyo walifanya kazi wakiwa na hisia kuwa Cooper hakutua salama.

Baada ya kubaini eneo ambalo ndilo lilikuwa na uwezekano mkubwa wa Cooper kutua, eneo ambalo lilikuwa nyikani kuzunguka mto Lewis karibu na ziwa Merwin! FBI kwa kutumia maofisa waliokuwa kwa miguu ardhini na helicopters angani wakafanya kazi ya kulikagua eneo lote hilo.

Lakini pia FBI wakatumia ndege na helicopters kukagua njia inayopitwa na ndege kutoka Seattle kwenda Rona (vector 23). Baada ya msako na upekuzi wa eneo lote hilo kwa siku kadhaa FBI hawakufanikiwa kumpata Cooper hai au amekufa, hakupata hata mabaki ya vifaa vya parashuti wala mabegi.

Pia walitumia submarine kutafuta chini ya sakafu ya Mto Lewis na Ziwa Merwin lakini kote hakukuwa na dalili ya Cooper wala mabaki ya vifaa alivyoruka navyo.

Baada ya mwaka mzima 1971 kuisha pasipo mafanikio yoyote ya kumpata kupa hai au mwili wake au hata mabaki ya vifaa alivyoruka navyo FBI ikabidi iombe msaada kutoka jeshi la marekani kusaidia msako huo. Hivyo basi jeshi la marekani wakatoa wanajeshi 200 kusaidia msako huo, pia wakapata msaada kutoka jeshi la Anga (Air force), pamoja na wanajeshi kutoka jeshi la ulinzi wa ndani ya nchi (national guard troops).

Kwa pamoja wakafanya msako wa kina zaidi katika eneo lote ambalo lilidhaniwa kuwa kuna uwezekano Cooper ndipo alipotua. Pia kampuni ya EEC ambayo inahusika na kufukua vitu vilivyozama majini (marine salvage firm), ilijitolea submarine ili kufanya msako chini ya ziwa Merwin kuona kama labda yeye Cooper au vitu alivyoruka navyo alizama umo.

Msako huu wa kina uliohusisha maafisa wa FBI, jeshi la marekani, makampuni binafsi pamoja na national guard troops ulifanyika kwa siku kumi na nane ndani ya mwezi march mwaka 1972 na pia ukafanyika tena mwezi April 1972 kwa siku kumi na nane nyingine.

Msako ulikuwa wa kina hasa kwani nukta baada ya nukta ilikaguliwa kwenye eneo lote ambalo walihisi cooper labda ametua ardhini na majini lakini mpaka msako huu unaisha ndani miezi miwili hiyo hawakufanikiwa kupata hata unywele au kipande cha nyuzi ya nguo ya Cooper au mabaki ya kitu chochote ambacho aliruka nacho siku ya tukio.

Kitendawili kikawa kigumu zaidi. Baada ya misako mingine mirefu zaidi bila mafanikio FBI ikawabidi waje na nadharia nyingine kwamba labda walikuwa wanafanya msako sehemu ambayo sio sahihi. Safari hii ikawabidi wafanye mahesabu ya kisayansi kabisa kwa kuzingatia kasi ya upepo siku ya tukio na uzito wa Cooper na mizigo aliyokuwa nayo na matokeo ya nadharia yao mpya ya mahesabu ya kisayansi ikawaambia Cooper atakuwa alidondokea eneo la kusini mashariki ya eneo walilokuwa wanafanya msako sasa. Eneo hili jipya walilolibaini kwa kuongozwa na hesabu za kisayansi lilikuwa linazunguka mto Washougul.

Hapa napo msako mkali ukafanyika kwa miezi kadhaa bila mafanikio yoyote.

Baada ya FBI kuona kuwa hakuna mafanikio yoyote katika misako yao ya maeneo ambayo walidhani labda cooper alitua ikawabidi wabadilishe nadharia yote. Sasa wakaweka nadharia mpya kuwa labda kuna uwezekano Cooper alitua salama salimini na yuko mtaani anatumbua hela zake.

Hivyo basi kwa kuwa FBI walizipiga picha noti moja moja ya fedha zote alizopewa Cooper (kumbuka walimpa noti 10,000 za dola 20). Kwahiyo walikuwa na serial number ya kila noti aliyopewa Cooper. FBI wakasambaza serial number hizi kwenye mabenki, macasino, maduka na kila sehemu ambayo fedha inatumika lengo ni kuwa kama noti hata moja ambayo Cooper alipewa itatumiaka mahali popote na kuingia kwenye mzunguko wa hela basi FBI watadetect na kutrace hiyo hela imetoka kwa nani.

Lakini wakasubiri miezi na miaka hakuna noti hata moja ambayo iliingia kwenye mzunguko wa hela.

Kitendawili kikazidi kuwa kikubwa zaidi! Kama Cooper hakufanikiwa kutua salama kwanini wameshindwa kupata mwili wake au mabaki ya vitu alivyoruka navyo ukizingatia kuwa wamefanya msako nukta baada ya nukta ya sehemu ambayo alitua. Na kama alitua salama na kuingia mtaani, kwanini hazitumii hela alizozipata maana hakuna noti hata moja kwenye mzunguko.

Fumbo hili liliwatesa FBI kwa miaka saba mpaka mwaka 1978 ambapo mwanga kidogo ulipatikana kuhusu tukio hili..

VIDHIBITI VINAFANYA FUMBO KUWA GUMU ZAIDI BADALA YA KUSAIDIA

Mwaka 1978 muwindaji mmoja aliokota kikaratasi chenye maelekezo ya namna ya kushusha mlango wa nyuma wa ndege aina ya Boeing 737 (Northwest Orient Flight 305 ilikuwa ni Boeing 727) na FBI wanaamini labda kikaratasi hiki kilidondoshwa na Cooper.. Lakini kidhibiti hiki hakikusaidia sana.

Kidhibiti ambacho kilikuwa na mchango mkubwa kwenye kuleta maswali zaidi kwa FBI kilipatikana mwaka 1980.

Mtoto wa miaka 8 aliyeitwa Brian Igram akiwa kwenye vacation na familia yake kwenye beach ya mto Columbia alikuwa akichimba chini ili kusaidia familia kuwasha moto waote. Igram alikuwa akichimba kwa mikono kama watoto wafanyavyo na akachimba shimo refu kiasi na akiwa anachimba alikutana na makaratasi. Baada ya kuyatoa hayo makaratasi kutoka kwenye shimo alilochimba wazazi wake waligundua kuwa zilikuwa na vibunda vitatu vya hela.

Baada ya kuzichunguza kwa makini wazazi wakahisi kuwa inawezekana fedha hizo zinahusiana na D.B Cooper tukio ambalo lilitawala kwenye vyombo vya habari kwa kipindi hicho. Hivyo basi wazazi wakawasiliana na vyombo vya ulinzi na baada ya FBI kuzisoma serial number za noti hizo wakathibitisha kuwa ni kweli noti hizo ni sehemu ya fedha alizopewa D.B Cooper mwaka 1971. Swali, je zilifikaje pale?

Hivyo basi FBI ikatumia wataalamu wake ili kupata mwanga kidogo.
Kwanza vibunda vyenyewe vya hela vilikuwa kama ifuatavyo; kila kibunda kilikuwa peke yake kinajitegemea kimoja kilikuwa na noti 100 zilizofungwa pamoja kwa rubber band isipokuwa kibunda kimoja tu ambacho kikikuwa na noti 90 lakini nazo zilifungwa pamoja kwa rubber band.

Pia licha ya kuwa noti zilikuwa zimefungwa pamoja kwa rubber band lakini zilikuwa zimekaa hovyo hovyo katika umbo la mviringo na wataalamu wa FBI wakatoa conclusion kwamba zilikuwa zimekaa hovyo hivyo kwa umbo mviringo kwasababu zilikuwa zime ‘kururuka’ na maji ya mto kutoka mahali fulani na kuna kunasa hapo.

Na hakika huu ndio ufafanuzi ambao angalau ulikuwa unaingia akilini.
Lakini swali linakuja; inawezekanaje vibunda vitatu vya hela ambavyo havijaungana kila kimoja kinajitegemea ‘vikururuke’ na maji alafu vije vyote vinase sehemu moja? Kitu kama hicho ni almost imposible.

Kutokana na kesi hii kuteka vyombo vya habari kipindi hicho kugundulika kwa noti hizi kuliteka hisia za watu na hii ikapelekea mtaalamu wa jiolojia aliyeitwa Leonard Palmer kutoka chuo kikuu cha Portland kufanya tafiti katika beach ambayo vibunda hivi vitatu vilipatikana na matokeo ya utafiti wake ndio yalishangaza zaidi FBI.

Kwanza kabisa kumbukumbu zilionyesha kuwa sehemu kubwa ya mto Columbia ikiwemo sehemu vinunda hivi vya hela vilipatikana ilifanyiwa dredging mwaka 1974. Dredging ni vile wanatumia vifaa maalum kutoa udongo chini ya mto na pembezoni mwa mto na kuumwaga kwenye beach ya mto. Kitendo hiki huwa kinafanyika ili kuongeza kingo za mto au kuboresha ubora wa beach.

Sasa basi, alichokigundua huyu mtaalamu ni kwamba katika lile shimo ambalo mtoto Igram alichimba na kukuta vinunda vya hela za Cooper chini yake kulikuwa na matabaka mawili ya udongo na ukichimba tena unakutana na tabaka la tatu ambalo lina udongo wa mfinyanzi ambao ndio udongo unaopatikana baada ya kufanya dredging. Sasa hii ina maana gani? Maana yake ni kwamba hivyo vibunda vya hela za Cooper vilikuwa deposited hapo baada ya dredging kuwa imeshafanyika. Sasa kumbuka kuwa dredging ilifanyika mwaka 1974 na tukio la Cooper likitokea mwaka 1971.

Kuna tofauti ya miaka miatatu hapo. Sasa je hivi kweli inawezekana hela zikururuke na maji miaka mitatu na kwa bahati mbaya au nzuri isiyomithilika bibunda vitatu vyote vikwame sehemu moja?

Kama hiyo haitoshi; kumbuka kuwa mtaalamu anasema kuwa chini ya shimo alilochimba mtoto Igram kulikuwa na matabaka mawili ya udongo ndipo ufikie tabaka la udongo mfinyanzi uliotokana na dredging hii inamaanisha kuwa baada ya dredging kufanyika mwaka 1974 ilipita miaka kadhaa amabapo yale matabaka mawili mengine yakajitengeneza kwa juu ya udongo mfinyanzi ndio hivyo vibunda vya hela za Cooper zikawa deposited hapo.

Na mtaalmu alikisia hivyo vibunda vya hela vimekuwa deposited hapo labda miaka miwili tu iliyopita. Sasa huo ulikuwa ni mwaka 1980, miaka miwili nyuma maana yake ni 1978 na kumbuka tukio la Cooper lilitokea mwaka 1971.! Kuna tofauti ya miaka saba hapo katikati. Na hili lilikuja kuungwa mkono na kikosi kazi maalum kilichoundwa baadae na FBI kilichojulikana kama Cooper Research Team kuwa vibunda vya hela lazima vilikuwa deposited hapo miaka kadhaa baada ya tukio la sivyo rubber band walizozikuta vimeshikilia noti zingekuwa zimeharibika kabisa.

Ugunduzi huu uliwapa maswali na kuwachanganya zaidi FBI badala ya kuwasaidia kwasababu haiingii akilini hela zikururuke na maji miaka saba.
Kumbuka umbali kutoka mto Columbia na ‘Vector 23’ (njia ambayo ilipita ndege ya akina Cooper siku ya tukio) kulikuwa na umbali wa kilometa 20.

Hivyo basi hata kama maji yangekuwa yanatembea taratibu isingechukua zaidi ya dakika 40 kwa vibunda hivyo kufika hapo. Kwahiyo kwa namna yoyote ile isingewezekana kwa sehemu ya kuchukua dakika 40 itumike miaka saba, na kwa namna yeyote ile habadani haiwezekani vibunda vitatu ambavyo havijashikana vije vikwane exactly sehemj moja!

Katika ofisi ya FBI maswali na mafumbo yalikuwa mengi kuliko majibu! Hizo fedha za Cooper zimefikaje pale? Zimekuja na maji? Mtu kaziweka? Kama ni mtu kwanini aziweke pale? Je, fedha nyingine ziko wapi? Kwnini vibunda viwili vina noti 100 kila kimoja na kibunda kimoja kina noti 90 tu? Noti kumi zimeenda wapi? Na hii inatoa clue gani kuhusu D.B Cooper?

Baada ya miaka sita ya kitendawili kuhusu fedha zilizookotwa zimetoka wapi hatimaye mwaka 1986 FBI ikanyoosha mikono juu na kusalimu amri kuwa fedha hizo zilizookotwa haziwezi kuwasaidia kumpata Cooper. Hivyo basi wakafikia makubaliano ya kuziganya fedha. FBI wenyewe wakachukia noti 14 kama kidhibiti na noti zilizobaki zikagawanywa kwa kijana Igram aliyeziokota na nyingine wakapewa kampuni ya Bima waliowalipa fidia Northwest Orient Airlines.
Igram aliziuza kiasi kidogo cha baadhi ya noti zake mwaka 2008 katika mnada wa hadhara kwa thamani ya Dola 37,000.
Mpaka leo hii noti nyingine zilizobakia ambazo Cooper alipewa mwaka 1971 (takribani noti elfu tisa na mia saba) hazijulikani zilipo.

SAIKOLOJIA YA MKAKATI WA COOPER

Baada ya miaka mingi ya upelelezi na kujiuliza maswali mengi hatimae mwaka 2007 FBI walitangaza kwa umma baadhi ya mambo waliyoyabaini katika mkasa mzima wa D.B Cooper.
Kwa mfano siku ya tukio Cooper alihitaji parashuti moja tu ili aweze kuruka lakini aliwaagiza kuwa anahitaji maparashuti manne. FBI wanaamini kuwa Cooper alitoa maagizo ya dizaini hii ili kupandikiza wazo kwa vichwani mwa maofisa wa FBI kuwa kulikuwa na uwezekano akaruka na mateka ambao watatumia maparashuti mengine matatu yaliyobaki. Hii iliwalazimu FBI kumpatia maparashuti manne ambayo hayana hitilafu au ubovu wowote. Na iliwachukua muda sana kubaini kuwa Cooper alicheza na akili zao bila wao kujua.

Pia uchaguzi wa kuiteka Northwest Orient Flight 305 haukuwa wa bahati mbaya. FBI wanaamini kuwa Cooper alifanya uchunguzi wa kina na kuchagua kuiteka ndege hiyo. Kumbuka kuwa Orient Flight 305 ilikuwa ni aina ya ndege ya Boeing 727.
Kwa kipindi hicho Boeing 727 ndio zilikuwa ndege pekee ambazo zilikuwa na uwezo wa kufunguliwa mlango wa nyuma mkiani ikiwa bado iko angani. Kitu hiki kilikuwa hakijulikani kwa raia na hata watu wa ndege wenyewe walikuwa hawafahamu jambo hili. Na taarifa hii ilifichwa kwasababu kwa kipindi hiki haikuwa kitu cha kawaida kwa ndege ya abiria kuwa na ubunifu wa aina hii.
Watu pekee ambao walikuwa wanafahamu suala hili na kuwahi kutumia advantage ya ubunifu huu walikuwa ni CIA ambao walitumia ndege kama hii kudondosha mizigo na maafisa wao katika maeneo husika katika vita ya Vietnam.

Pia injini za Boeing 727 zilikuwa juu kidogo tofauti na ndege nyingine za abiria ambazo injini zake zilikuwa chini chini karibia usawa wa madirisha. Kumbuka kuwa injini ya ndege ikiwashwa ikiwa inazunguka kitu chochote kikipita mbele yake kinavutwa na kumezwa kwenye injini na kuharibiwa au injini yenyewe kupata hitilafu. Hivyo basi uchaguzi wa kuruka kutoka kwenye Boeing 727 ilimaanisha kuwa ilipunguza hatari ya mrukaji kuvutwa na kumezwa na injini.

Pia FBI wanaamini kuwa Cooper alifahamu kuwa Boeing 727 ilikuwa na teknolojia mpya ambayo iliruhusu kujaza mafuta kwenye matanki matatu ya ndege kwa kutumia tundu moja tu. Kama isingekuwa na teknolojia hiyo hiyo ya kujaza mafuta kwa tundu moja tu FBI wangeweza kutumia mwanya wa gari la kujazia mafuta likiwa linazunguka upande mwingine wa ndege kupenyeza maafisa wao.

Pia Boeing 727 ilitoa advantage nyingine katika ufunguaji wa mlango wa nyuma wa ya mkia wa ndege ambapo ukiwasha tu kifaa cha kufungua mlango huo hata rubani aliye mbele hawezi kuufunga. FBI wanaamini Cooper alilifahamu hili ndio maana baada ya kuwafungia watu aliobaki nao kwenye chumba cha rubani. Alifungua mlango wa nyuma kwa kujiamini na kuruka.

Pia Boeing 727 ilikuwa na ubunifu mwingine adhimu tofauti na ndege nyingine kwa kuwa ilikuwa unaweza kucontrol speed na mwinuko wa ndege ‘manually’ hata ukiwa katika sehemu ya kukaa abiria, pia kwa kipindi hicho Boeing 727 ndio ilikuwa ndege pekee ya abiria ambayo ilikuwa na uwezo wa kugeuza mabawa yake ili yakae katika nyuzi 15.

FBI wanaamini kuwa Cooper alifanya utafiti wa kina na kuweka mkakati kabambe kabla ya kutekeleza tukio na alitumia advantage zote hizi za ndege ya Boeing 727 ili kutekeleza tukio lake kwa ukamilifu wa 100%.

Lakini jambo lingine la muhimu zaidi ilikuwa ni uchaguzi wa siku ya tukio. November 24.
Kwanini?? Baada ya tukio FBI kugundua Cooper alikuwa ameruka nyikani wazo mojawapo ambalo walilipata ni kwamba kwakuwa sehemu aliyoruka ilikuwa mbali mno na makazi ya watu, hivyo basi ingemchukua Cooper takribani siku hata tatu kusafriri ili kurudi mtaani. Kwahiyo FBI walidhani kwa kuwa Cooper asingeliwezakutumia siku moja kusafiri kurudi mtaani hivyo basi kama kesho yake wangembelea kila ofisi na maeneo ya kazi kukusanya orodha ya watu ambao hawajatokea kazini lazima watu hao mmoja wao angekuwa ni Cooper.
Lakini hii ilikuwa haiwezekani! Kwanini? Kwasababu November 24 usiku wake ulikuwa ni sikukuu ya ‘Thanks giving’ maana yake ni kwamba kesho yake haikuwa siku ya kazi. Mbaya zaidi November 24, 1971 ilikuwa ni siku ya Jumatano kwahiyo kesho yake alhamisi pamoja na ijumaa zilikuwa siku za sikuu na siku zilizofuata zilikuwa ni weekend. Kwahiyo hii ilimpa Cooper siku nne za kutosha kabisa kusafiri kutoka nyikani mpaka mtaani. Na kama alikuwa mfanyakazi ofisi fulani maana yake Jumatatu aliingia ofisini kama watu wengine.!!! FBI wakapiga saluti..!?

“MAISHA BAADA YA TUKIO LA D.B COPPER”

Baada ya tukio la utekaji la Cooper kutokea na FBI kuonekana dhahiri kuwa wameshindwa kufikia mwisho wa kutengua kitendawili cha tukio hili hali ilikuwa tete katika viwanja vya ndege na kusababisha marekebisho mengi ya protokali za ulinzi na utoaji huduma katika viwanja vya ndege nchini marekani.
Kwanza kabisa serikali ya marekani ilitilia mkazo uanzishwaji upya na kuboresha programu ya maaskari wanaosindikiza ndege za abiria (Sky Marshal Program).
Pia serikali ilichukua hatua kali zaidi kwa mara ya kwanza kabisa kuanzisha mpango wa kupekua mizigo ya abiria kabla hawajapanda kwenye ndege. Hatua hii ilisababisha mvutano mkali kati ya wananchi wa marekani na serikali yao katika miaka ya sabini ambapo ilifikia hatua kesi za kikatiba zilifunguliwa dhidi ya serikali ya marekani kwa madai ya kwamba kupekua mizigo ya abiria ilikuwa inavunja Kipengele/Marekebisho ya Nne ya katiba ya marekani (Fourth Amendment) kipengele kinachomlinda raia wa marekani dhidi ya upekuzi na kuingiliwa faragha yake. Lakini mwishoni serikali ilishinda kesi hizi na tangu hapo imekuwa ni jambo la lazima kwa mizigo kukaguliwa kabla ya abiria kupanda ndege.

Si hivyo tu, serikaki kupitoa idara ya usafiri wa anga nchini marekani (FAA) ikaenda mbali zaidi kwa kuzitaka kampuni zote za usafiri wa anga zinazotumia ndege aina ya Boeing 727 wafunge kifaa maalum cha kuzuia mlango wa nyuma mkiani mwa ndege kufunguka pindi ndege ikiwa angani. Kifaa hiki kilipewa jina ‘Cooper Vane’.
Na pia FAA walitoa maagizo kuwa ndege zote ziwekwe matundu maalum ya kuchungulia (peepholes) katika mlango wa chumba cha marubani ili kuwawezesha waweze kuona kinachoendelea upande wa abiria.

Pia, mwaka 2013 Earl Cossey mmliki wa kituo cha kufundisha Skydiving sehemu ambapo maparashuti manne yaliazimwa na FBI na kumpa Cooper mwaka 1971 alikutwa ameuawa nyumbani kwake. Bw. Cossey alikuwa ameajiriwa na FBI mara tu baada ya tukio la Cooper akiwa kama mshauri muelekezi (consultant) katika juhudi za kumtafuta Cooper na alihusika katika hatua zote za upelelezi.
Ziko nadharia nyingi zinazoamini kuwa vyombo vya usalama vya marekani vinahusika katika kifo cha Cossey na watu wanadhani kuwa kuna jambo la siri ambalo alikuja kulibaini katika upelelezi huo wa tukio la Cooper na FBI walihofia labda Bw. Cossey asingeliweza kutunza siri hiyo, hivyo basi suluhisho jepesi wakaona ni kumwondosha.

Hatimae..

Mwezi July mwaka 2016 tarehe 14, shirika la upelelezi la FBI wanatarajiwa kufunga jalada la kesi ya Cooper na kukivunja kikosi kazi maalum cha kuchunguza tukio la Cooper (Cooper Research Team) kwa madai kuwa hakujawa na tumaini lolote la kufikia hitimisho katika upelelezi huo.
FBI watafunga jalada katika miezi sita ijayo wakiwa bado hawafahamu kama Cooper yuko hai au ameshafariki, hawajui kama hilo ni jina lake halisi au la kubuni, hawafahamu fedha alizopewa zimekwenda wapi na wala hawafahamu ni namna gani binadamu mmoja alifanikiwa kutekeleza tukio kwa usahihi wa asilimia mia moja kama tukio hili.
Tukio la Utekaji la Cooper ndilo miezi sita ijayo litaingia kwenye orodha ya kumbukumbu ya shirika la FBI kama kesi iliyotumia muda mrefu zaidi kufanyiwa uchunguzi (miaka 45) na tukio hili litaingia kwenye vitabu vya historia ya nchi ya marekani kama tukio pekee la utekaji wa anga (hijacking) ambalo limeshindikana kufikia hitimisho.

Kwa hivi sasa katika maeneo mbalimbali nchini marekani na hasa eneo la Airel, mjini Washington kila mwaka mwezi November watu husherehekea ‘Cooper day’ kukumbuka tukio hilo la kihistoria nchini marekani lilotekelezwa na binadamu mmoja peke yake ambaye kutokana na ustadi alioutumia kufanikisha azma yake amebakia kwenye vitabu vya historia, na umahiri wake umemfanya kugeuzwa kutoka kuwa binadamu wa kawaida mpaka kuwa ‘binadamu wa kusadikika’! Mwenyewe alijitambulisha kama D.B Cooper!

By Yericko Nyerere

Ikulu ya Dar ihamishwe ndani ya miezi 18 kuanzia 01/01/2015.

By: Yericko Nyerere

Ikulu (State House) ya nchi ya Tanzania lijengwa kwa namna ya kipekee na Wajerumani mwaka 1891 na gavana wa Kihuni Chakosi Dikwe na kutumika kama ngome ya gavana. Iliharibiwa wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia. Baada ya vita ya kwanza ya Dunia Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa kikoloni wa Waingereza na hapo ngome hiyo (state house) iliitwa Government House na ilijengwa tena mwaka 1922 ambapo gavana wa Kiswahili Sir Unapima Mkali alipochukua utawala. Majengo hayo yamejengwa kwa ubora wa pekee na ni ya kihistoria kwani yalikuwa ni Ngome za magavana.

Makazi haya ya rais nchini Tanzania yaliko Kaskazini Mashariki mwa jiji la Dar katika nyuzi 2 kutoka usawa wa bahari ndio makazi ya kiongozi wa nchini yaliyohatarini zaidi kuliko makazi ya rais yeyote barani Afrika kwa sasa,
Mathalani, kutoka lango kuu la ikuu kwenda mpaka chumba anacholala rais ni mita 63.2. Hii inaonyesha kuwa Rais wa nchi hii hayuko salama hasa linapokuja suala la artificial security,

Eneo la ikulu hii ni dogo, halizidi eneo la mraba 13,200 Ambacho ni kipimo kidogo kabisa kwa dunia ya leo kwakuweka makazi ya kiongozi wa nchi.

Upande wa Kaskazini mita 10 kuna bahari yenye kina cha mita 18 hadi 33, hii inaweza kuruhusu nyambizi ndogo zenye makombora ya masafa mafupi kuifikia ikulu, ulinzi wa eneo hili ni natural security jambo ambao linatia shaka zaidi usalama wa rais wetu,

Upande wa mashariki mwa Ikulu kuna majengo manne yenye urefu kati ya mita 30,43 na 56 ambayo ni wizara ya ardhi, wizara ya utumishi, mnara wa kuongozea meli, na chuo cha ukarani. Katika itifaki ya kiusalama majengo haya ni hatari kubwa mno kwakuwa yapo umbali wa mita 40 hadi 160 tu, eneo hili laweza kutumiwa na walenga shabaha kuelekea ikulu, hii inatokana na sehemu kubwa ya vyumba vya shughuli za rais kuelekezwa upande huu wa mashariki, mfano, chumba cha mazozi, Choo na bafu na chumba cha siri cha mikutano (PU),

Sniper yeyote akitumia moja ya majengo ya eneo hili anaweza kumuua kiongozi wetu aliye ndani ya bafu,choo ama chumba cha mikutano tena bila idara za usalama zilizo ndani ya ikulu kutambua mlenga shabaha huyu alipo mpaka uchunguzi wakutumia carbon fire missile ambao kimsingi sniper atakuwa keshatokomea.

Eneo hili pia lina soko la samaki ambapo kiafya ni hatari zaidi kwakuwa moshi unaotokana na ukaangaji wa samaki hujaa ikulu waweza dhani mapishi hayo yanafanyika ndani ya ikulu hii.

Upande wa kusini mwa ikulu kuna majengo matatu marefu, Wizara ya fedha, Benk kuu na magereza eneo hili linatazama lango la ikulu, majengo haya yapo umbali wa mita 200 na 240, japo kuwa majengo haya ni ya serikali na yanatumiwa na serikali lakini kiusalama haya hayafai kuwepo maeneo haya, ikiwa adui yeyote mlenga shabaha za mbali (sniper) atatumia majengo haya basi shabaha yake itakuwa ni nyakati za rais kuingia ama kutoka ndani ya ikulu hii ya Dar.

Upande wa Magharibi lipo jengo moja ambalo ni refu linalokadiriwa kuwa na ghorofa 18, jengo hili lipo umbali wa mita 370 kutoka chumba cha kulala rais ndani ya ikulu hii, na katika upande huu wa Magharibi mwa ikulu ndiko chumba cha cha kulala rais kiliko maarufu kama DDO,

Jengo hili refu ni eneo la kibiashara na makazi ijapokuwa sehemu ya makazi ya juu kabisa ya ghorofa yamechukuliwa (yamepangishwa) kwa maafisa usalama wa serikali lakini hilo haliondoi uhatari uliopo kutokana na uwepo wa majengo haya marefu pembezoni mwa Ikulu hii,

Mlenga shabaha yeyote mwenye nia mbaya na taifa hili ikiwa atatumia jengo hili basi shabaha yake itakuwa ni wakati rais yupo chumbani na shabaha yake kuu itakuwa kichwani kwenye usawa wa dirisha la magharibi.

Haya ni vema tukayasema ili kuliweka taifa mahali pausalama zaidi kutokana na taifa liendako, ikumbukwe kuwa miaka michache tu iliyopita eneo hili la ikulu halikuwa na uzio kabisa na watu walikuwa wakijatiza langoni kabisa kule wakitoka feri kwenda Hospital ya Saratani. Lakini kadiri mageuzi ya nchi yanavyokwenda mambo yamebadilika sasa angalau ukifika hata getini kuna artificial security kuliko natural security,

Sasa Tanzania tunaingia kwenye nchi zennye uchumi mkubwa kutokana na raslimali gesi tuliyonayo, ambayo kwa sasa inakadiriwa kuwa Tz ina wingi wa gesi yenye ujazo mm3 9.4trilioni, kiwango hiki ni robo tatu ya gesi izalishwa Urusi, na bado utafiti zaidi bado unaendelea.

Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Afrika kuwa na gesi nyingi kwa sasa ambapo kwa kiwango kulichogunduliwa tu inauwezo wa kuihudumia Italia, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza na kukidhi mahitaji yao kwa miaka mia moja mbele.

Kaimu mkuu wa shirika la gesi nchini Urusi Korov Matoriv anasema, ikiwa gesi iliyogunduliwa nchini Tanzania serikali ya nchi hiyo ikiandaa sera na kuzifanya kuwa kwa maaslahi ya nchi hiyo basi Tanzania itakuwa nchi yenye uchumi mkubwa kwa miaka 15 tu kuanzia 2015,

Katikati ya neema hii ya utajiri ndipo viongozi wa kitaifa huhitaji ulinzi maradufu na chuki za nje huongezeka huvi ulinzi wetu ukiwa legelege tutarajie assassination kwa viongozi wetu toka mataifa makupe ya kimagharibi hasa CIA na M16,

Kwa sasa njia mwafaka ni kuhamisha ikulu hapa ilipo na kuipeleka Dodoma ikiwa dhamira ya uhamiaji Dodoma bado ipo, lakini kama Dodoma bado ni kizungumkuti basi sehemu mujarabu na yenye uwiano mzuri wa protokali za kijasusi na kiulinzi basi ni Kigamboni.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Rais ajae 2015

By Yericko Nyerere

Nadharia ya Usalama wa Taifa (TISS) ibadilike kuanzia sasa, Taifa lipo hatarini

By: Yericko Nyerere

Taasisi hii ambayo ndio uhai wa taifa letu imefanya mengi ya kutukuka na yasiyomithirika hata kwa chembe ya haradali. Wadadisi wa masuala ya kijasusi wataungana nami kuwa TISS ndicho chombo pekee cha nchi hii kilichofanya kazi yake kwaufanisi mkubwa na kulifikisha taifa hapa lilipo, Naelewa wengi watanishangaa na kuhamaki, kwanini naisifia taasisi hii ambayo wengi wapo nayo mlengo wakushoto.
Kama si uimara wa taasisi hii leo tungalikuwa tunanena kwa lugha yake kila mmoja wetu hapa nchini.

Pamoja na kusimama imara kwa taasisi hii, yapo mambo ya msingi yanayo takiwa kuwekwa sawa ili taasisi hii iendane na mageuzi ya dunia ya leo hasahasa kuelekea 2015, mahuisho katika chombo hiki muhimu ni lazima yaguse nyanja zote kuanzialeadership,watendaji,te knolojia na sheria.

Sheria iliyounda chombo hiki inamapungufu kwa sasa kulingana na mageuzi ya kifikra na kiteknolojia,

Sheria hii inaififisha tasisi hii huku ikiruhusu siasa kujipenyeza ndani ya chombo hiki adhimu na muhimu kwa uhai wa taifa letu,

Mathalani sheria hiyo inasema, “taasisi hii itahusika/itajihusisha na kutambua/kubaini na kutoa ushauri tu”

Kwamaneno hayo tu, TISS imenyimwa nguvu ya mojakwamoja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu.

Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (wakisiasa) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi. Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika chombo hiki,

Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hii ili taasisi hii ya Usalama wa Taifa iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe), Hata hivyo nafikiri ihuishwe sheria hii imlazimishe kiongozi anayeshindwa kuchukua hatua kwa ushauri wa taarifa sahihi za usalama au anayechukua hatua zisizotakiwa wakati ana taarifa na ushauri sahihi wa taasisi hii hawajibike. Ili hii iwe na maana chombo hiki kinatakiwa kiimarishwe lakini pia kitenganishwe na siasa ya kivyama.

Kwa taifa ambalo ni imara,Usalama wa Taifa ni taasisi inayotakiwa kufanya kazi kwa weledi kuliko idara yoyote ile.Weledi wake hautakiwi kutiliwa shaka yoyote kwa viwango vya kitaifa,kiakanda(regional) au kimataifa kwa maana pana zaidi.TISS inatakiwa kutengeneza mfumo ambao ni more sophisticated katika kufanya information sharing wakati huo huo ikijaribu kuimarisha vitengo vilivyopo ili kutimiza malengo ya idara na taasisi kwa ujumla kama ilivyo mifumo ya mataifa makubwa kama mkakati wa ulinzi na usalama wa Marekani,Uingereza,Pakistan,Is rael,Afrika Kusini,China,India na Canada

Ingawa miakati mingi ya mataifa yaliyoendelea imekua sensitive zaidi kwenye maslahi yao ya kiuchumi na ushindani wa nguvu na mamlaka kimataifa(Power Interests) lakini kwa taifa lililofikisha umri wa miaka 50 ni lazima liwe na mtazamo imara na kwa kuanzia ni lazima tungeanza na kanda yetu ya Maziwa makuu,Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, hii nikwakuwa Tanzania tumeingia kuwa taifa tajiri zaidi barani afrika kwa sasa baada ya ugunduzi wa GESI yakutosha inayokadiriwa kuweza kulihudumia bara la ulaya kwa miaka 100 bila kukoma.

Kwa mfano tuna washindani wetu kiuchumi na power struggle hapa east afica ambao ni Kenya.Hatujaweza vya kutosha kwenye Economic intelligence kule Kenya inagawa wao wamewekeza hapa kwetu.Leo hii Kenya ina-export TANZANITE,Wana-Export gold n.k.Balance of trade kati ya Tanzania na Kenya ni subject of Economic intelligence.tunapotunga sera zetu za kiuchumi tunatakiwa tutumie taarifa za kiinteligesnsia kwa kutumia wataalamu waliobobea na pia tuangalie possible scenarios na move za washindani wetu.Katika maofisa ubalozi wetu walioko Kenya tujiulize ni wangapi wenye uwezo kusimamia maslahi yetu ya kiuchumi hapa EAC au ukanda kupitia economic power house(Kenya) katika ukanda huu?

Kuna mgogoro kati ya dola na sarafu yetu.Je hakuna uwezekano kwamba dola zimekua zikinunuliwa kwa wingi na kuwa smuggled kwenda Kenya ili kuhujumu uchumi wetu na ku-frustrate fisical na monetary policy zetu?
Usalama wetu bado unahitaji mageuzi kutegemeana na matakwa ya kisheria na kuboresha malengo ya TISS ili iwe modern zaidi
Malengo ya TISS kulingana na trend ya dunia kwa sasa na mahitaji ya taifa tunakopitia kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni yaegemee katika kutabiri(si utabiri wa majini/tunguri bali utabiri wa kisayansi),Kupenya,na kuwahi matukio ya hatari kwa maslahi na usalama wa taifa letu,na kuwasaidia wale wanaotekeleza sera yetu ya ulinzi na usalama,kulinda taifa na watu wake,utekelezaji wa sheria na kulinda maslahi na sera zetu kitaifa bila kuathiriwa na ushawishi au hatari yoyote kutoka ndani na nje ya taiafa letu na kulinda malengo yetu kama jamii kwenye Nyanja za kimataifa(jamii nyingine)
Malengo makuu yanatakiwa kujikita katika:

Mosi,Kuongeza nafasi na umuhimu wa idara ya mahakama na vyombo vya kutoa haki.Lengo hapa linatakiwa kuwa juu ya kuunganisha idara za mahakama,wizara ya mambo ya ndani na vitengo vyake kwa kuzingatia upeanaji wa taarifa huku haki za msingi za kiraia zikilindwa pamoja na uhuru wake tofauti na ilivyo sasa ambako TISS inatuhumiwa kutumika kuhujumu haki za kiraia kwa visingizio lukuki.Lengo kuu liwe kulinda haki na uhuru wa watu bila kuathiri maslahi ya jumla.Hili linahitaji ushirikiano kuanzia serikali kuu,mikoa,wilaya,majimbo ya uchaguzi,kata na hata ngazi ya mitaa pamoja na sekta binafsi

Pili,Utengenezwe utamaduni mpya wa kuahamasisha mawazo mbadala na matumizi ya weledi(professionalism/expertise):Kubadili utamaduni ndani ya TISS ni muhimu sana ili kuepuka mimosa ya kimkakati. It is necessary to create an intellectual culture that promotes discussion as well as dissenting opinion. It will require the use of collaborative technology, where subject expertise is maximized, increased cross-agency communication, and the exploration of alternative analysis

Tatu,Kurahisisha zaidi ukusanyaji wa taarifa za kintelijensia:TISS haina budi kuwa mbele katika matumizi ya teknolojia na pia ku-update wataalamu wake kitaaluma na katika matumizi ya zana za kisasa zaidi ili kurahisisha ukusanyaji huo kutoka Open-sources na kutoka Human-sources

Nne,Kuajiri watu kulingana na uwezo na taaluma zao na pia kuajiri watu ambao tayari wana ajira kwenye vitengo vingine lakini walipwe vizuri kwa ajili ya kazi ya usalama ili kupunguza gharama za kupachika watu wapya katika idara,mashirika na taasisi nyeti nchini.Pamoja na hili kitu cha muhimu watu hawa ni lazima wawe na sifa zinazofanana (common attributes) katika ujanja,uwezo wa hali ya juu na haraka katika utendaji huku maadili ya juu kabisa katika vigezo vya utendaji katika idara hii vikizingatiwa

Tano,TISS ibadili utamaduni wa kuhitaji-kujua kwenda Kuhitaji-kutoa taarifa(changing from the culture of need-to-Know to need-to-share):Ili kuongeza ushirikiano na ufanisi katika kila ngazi ni lazima mtazamo wa idara hii ubadilike na suala la kutoa taarifa liwe ndiyo njia kuu ya kufanikisha malengo ya idara katika ngazi zote kwa hiyo kuna haja ya kuangalia jinsi taarifa zinavyofika kwa ubora unaotakiwa,kwa usahihi na kwa muda muafaka na hili ni muhimu na litasaidia zaidi kuwa karibu na watunga sera(policy makers)

Sita,Kuimarisha na kupanua zaidi uhusiano kati ya TISS na washirika wa ndani ya nchi na vitengo vingine vya kijasusi vya mataifa ya nje:Hii ni kwa kuwa tunaweza kuwa na common threats kwenye uchumi,kiitikadi,kiutamaduni,k iulinzi n.kHata hivyo taarifa za kijasusi kutoaka kwa washirika wetu ni lazima ziangaliwe kwa umakini wa hali ya juu na pia tuwe na taarifa zetu ambazo tunaweza kulinganisha na taarifa za washrika wetu.Hizi kwa kijasusi zinaitwa ‘Corroboration codification’
Saba,kitengo kidogo kabisa cha mwisho ndichokinachotakiwa kuwa na acces ya taarifa nyeti lakini kitengo hicho kiwe scrutinized kwa hali na mali.Hata hivyo nitajadili kuhusu juu ya mfumo wetu mbovu wa counterintelligence

Nane,Kujenga mfumo ambao ni uniform zaidi katika utekelazi kisayansi na kiteknolojia,Ni lazima sasa idara iwe centralized katika kutoa maelekezo na iwe more decentaliced katika utekelezaji kwa mtindo ambao unaitwa ‘pyramid execution’.unified research itumike ili kuongeza ushirikiano na idara mbali mbali

Tisa,Mfumo wa kupongeza na kuzawadia utumike kuongeza performance

Kumi,mtindo wa kutumia miongo utumike lakini zaidi kwa haraka mtindo wa kutumia siku utumike badala ya miaka.Kwa mfano 720 days plan itumike badala ya miaka 2,180 days pla itumike badala ya 6 months plan kwa ajili ya monitoring na kuepuka urasimu na uvivu usio wa lazima

Pia ni vyema kutokana na power struggle ya ukanda tuunde vitengo vya ujasusi vya nje.kitengo hiki kifanane kwa muundo ingawa kutakua na marekebisho kidogo lakini kifanane na kitengo cha RAW cha india ambacho kiliundwa baada ya vita ya India na China.kabla ya hapo kulikua na kitengo cha IB ambacho kilikua na miaka 120 lakini hicho kilitumika kuchunguza watu zaidi na taasisi za kisaiasa.waingereza walikitumia kuwachunguza akina Mahatma Gandhi,Azad na Nehru zaidi.Kitengo cha RAW kinatumika kwa ajili ya military Intelligence na financial intelligence.Kuna haja ya kupima maofisa ubalozi wetu wanaopelekwa nje pamoja na Mwambata wa jeshi katika balozi zetu(defence attaché) kulingana na sera yetu.

Naiona hatari iliyombele yetu, hasa ya kisiasa, kiuchumi na machafuko ya kiroho.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki TISS.

By Yericko Nyerere

Ujasusi/Upelelezi/Udukuzi, maana yake halisi na uhatari wake.

By: Yericko Nyerere.

Mpelelezi ni mtu anayekusanya taarifa za adui , mshindani wa biashara au serikali adui ila saa nyingine mpelelezi huyo anaweza kufanya kazi ya kumpeleleza adui ila akamgeuka basi wake aliyemtuma kwa sababu mbalimbali .

Mtu huyu huwa anakusanya taarifa hizi kwa siri kwa kuangalia , kusikiliza , kufuatilia na kutumia vifaa vingine kutokana na ukuaji wa tekinolojia lakini lengo ni lile lile kupata taarifa za siri bila mhusika , wahusika kujua kwamba taarifa zao zinachukuliwa .

Shuguli za upelelezi zimekuwepo kwa miaka mingi toka binadamu ameanza kuishi duniani na kila kipindi zinabadilika utokana na ukuaji wa binadamu kimbinu , vifaa na wahusika wenyewe .

Kutokana na kukua kwa tekinologia watu wengi wametumia tekinologia hizo kukusanya taarifa na kuacha njia za asili ya upelelezi ambazo wakati mwingine ni sahihi kabisa kwa wakati huu .

Ili jamii Fulani isonge mbele kwenye maendeo Fulani ni vizuri iwekeze sana kwenye nyenzo na vitendo vya kipelelezi na hujuma kwa kuwa na watu wazuri kila sehemu pamoja na vifaa.

Labda tujiulize sasa kwanini kuna upelelezi , kwanini watu wanakuwa wapelelezi , mtu anavutiwa kukusanya taarifa za siri za mtu au kampuni au serikali nyingine kwa njia ya siri ?

Kwa kweli hakuna maana moja ya kwanini mtu anaamua kuwa mpelelezi au anaamua kusaliti wenzake kwenye upelelezi na kwenda upande wa adui lakini kuna vichocheo vinne vikuu ambavyo vinatumika kwenye shuguli hizi .

Kitu ambacho kinaweza kuwa namba moja ni hela , fedha au uchumi . kama nchi jirani imeshindwa kabisa kuingiza wapelelezi ndani ya baraza la mawaziri ili kupata taarifa kutumia njia za kawaida basi pesa inaweza kutumika katika kuhonga watu haswa wasaidizi au mawaziri wenyewe hata viongozi wengine ili kupata taarifa wanazozitaka .

Ushindani wa viwanda na biashara kati ya nchi au kampuni unategemeana sana na fedha ambazo hutolewa kwa wapelelezi au wachunguzi wengine ili kupata siri za mshindani wake sokoni au popote .
Katika shuguli za kijeshi zinazofanywa na nchi moja dhidi ya nyingine au vikundi vya kigaidi na vya kihalifu fedha hutumika sana na mfano hao ni tunaposikia kuhusu kundi la al shabab kuhonga baadhi ya polisi wa mipakani ili wavushe silaha na watu kwa ajili ya kufanya mashambulizi au wapewe taarifa mapema wakati polisi wanapofanya msako kwenye maeneo yao .

Kichocheo cha pili ni Itikadi ambayo ni Msimamo au mtazamo kuhusu masuala Fulani ya kimaisha , dini , imani , uongozi na mengine mengi hapa kwenye itikadi ndio makundi mengi ya kigaidi yanachipukia na kupata watu wa kujiunga nao wakifuata mtizamo na misimamo ya imani yao . vyama vya siasa navyo vinapata wafuasi wao kutokana na hili la itikadi ingawa wengine wanaweza kuwa sio wasomi wa itakadi wala kuielewa wanafuata mkumbo mpaka wanapoumizwa au kuumiza wengine ndio wanashtuka kitu ambacho wanakuwa wamechelewa .

Kwahiyo ili uwe mpelelezi mzuri wa kundi la kigaidi lazima uelewe itakadi yao , nchi , vikundi au vyama vya siasa na vikundi vingine vya siri .

Ili serikali na wadau wengine waweze kukabiliana na vikundi vya kigaidi ni vizuri kuwekeza sana kwenye suala la kujua itikadi za vikundi wanavyopambana navyo .

Hapa kwenye itikadi ndipo uzalendo unatakiwa kujengwa kwa vijana , watoto na wengine kwenye taasisi za elimu ili wasiweze kuangukia kwenye mikono ya wahalifu na maadui wengine kutokana na itikadi zao mfano china wana ukomunisti , nchi za magaribi wana itikadi zao na mengine mengi .

Wakati mwingine watu au mtu anaweza kuingia kwenye makubaliano na adui baada ya kukamatwa akifanya upelelezi au hata kabla lakini adui anaweza kuona yeye anafaa akampa mafunzo na mbinu nyingine ili aweze kupelelezi kwa niaba ya adui huyo mwisho wa makubaliano kama haya mara nyingi ni watu kuuwawa na hujuma nyingine nyingi dhidi ya nchi yake au watu wake wa karibu .

Mmoja wa wapelelezi maarufu kwenye suala hili anaitwa Kamanda Zig Zag , yeye alikua mfungwa kwenye gereza la uingereza kwenye kisiwa Fulani kisiwa hicho kilivyotekwa na wajerumani yeye akaandika barua kutaka kujiunga na jeshi la kijerumani baada ya muda alipelekwa ufaransa kwa mafunzo kisha akatumwa uingereza ili akalipue kiwanda cha kutengeneza ndege za kivita . Alivyotua uingereza akatoa taarifa kwa mamlaka za uingereza sasa akawa upande wa uingereza tena akatengeneza mlipuko bandia na kuaminisha wajerumani kwamba kweli kimelipuliwa kisha waingereza wakamtuma arudi ujerumani kwahiyo akawa mpelelezi wa uingereza ndani ya ujerumani .wajerumani walimtuma maeneo mengi ulaya kwa kudhani anawasaidia kumbe taarifa zote zilikuwa zinaenda kwao uingereza .

Kuna wakati mtu analazimika kufanya upelelezi dhidi ya mtu au watu baada ya nguvu kutumika au kulazimishwa ili labda asiuwawe au ndugu zake wa karibu asiuwawe mara nyingi wanaweza kutumika wapenzi na wapendwa wengine ili mtu afikie muafaka wa kufanya upelelezi dhidi ya nchi , kampuni , washirika na wengine wa karibu .

Hapa kwenye nguvu wakati mwingine mtu anaweza kusingiziwa kitu au kuingizwa kwenye kashfa au kutengenezwa uwongo ili akubali kufanya upelelezi dhidi ya wengine lakini sio kwa hiari yake .

Pia kuna suala la umuhimu au umaarufu wa mtu au uzuri wake , kuna watu wengi maarufu kama wanamuziki au wacheza mpira na warembo wanatumia fursa hiyo kufanya upelelezi dhidi ya maadui wa nchi zao au washindani wa kibiashara wanajua kwa kutumia njia hiyo wanaweza kuingia chumbani , kulala na wanaume au wanawake , kuchungulia simu au kuweka vinasa Sauti , kujua marafiki au ndugu wa karibu , mipango ya biashara na mengine mengi .

Baadhi ya watu haswa vijana wanajiingiza au wanaweza kuingizwa kwenye shuguli za kipelelezi kwa wao kupenda vile wanavyoona kwenye sinema au kusoma vitabu au kuhadithiwa na wao wanaamua kujihusisha na upelelezi lakini bila kuwa na mafunzo au mtu yoyote anayemuongoza kwenye mambo mbalimbali anayotakiwa kufanya .

Wengine wanaweza kuwa wapelelezi wazuri ndani ya polisi , majeshi na kampuni lakini hawalipwi vizuri au hawaridhiki na baadhi ya vitu matokeo yake ni kuuza siri na mikakati mengine kwa wapinzani au maadui ili kuweza kuleta mabadiliko na mengine ndani ya taasisi yake au kuiua kabisa isiwepo .

Mahusiano binafsi kati ya watu au mtu ni moja ya kichocheo kikubwa cha watu kuweza kufanya upelelezi mara nyingi yanaweza kuwa mahusiano ya kifamilia kuoleana , kuowa au kuolewa hii maarufu inaitwa HONEY TRAP na hii ni ngumu kugundulika kwa sababu ni mambo binafsi sana na yanaweza kuchukua muda mrefu kwenda vizazi na vizazi viongozi na viongozi .

Kama nilivyosema hapo juu upelelezi umeanza siku nyingi na kila jamii inategemea upelelezi ili iweze kujua mwingine ili kuweza kupambana au kushindana nae ili aweze kuwa juu kwenye mambo mbalimbali na upelelezi umebadilika kwa kiasi kikubwa sana .

Ni vizuri taasisi zetu kuwekeza vizuri kwenye upelelezi kupata vijana hodari , wapewe mafunzo ya kutosha , mishahara , motisha , vifaa na kuzidi kuwaongezea ujuzi ili kuweza kupambana katika dunia ya sasa ya sayansi na tekilologia .

Upelelezi usiishie ndani ya jeshi la polisi au JKT , au Usalama wa Taifa tu , hata vyuo vinatakiwa kuwa na wapepelelezi , kampuni za nchini zinatakiwa kuwa na wapepepezi , mashirika ya umma yanatakiwa kuwa na wapelelezi , viwanda vya ndani vinatakiwa kuwa na wapelelezi na wote hawa wanatakiwa kufanya kazi pamoja ili kuleta maendeleo kwa jamii ya watanzania .

Nchi za wenzetu zinaendelea na kuendeleza ushindani mkubwa kwenye nyanja hii , uchina ilishtuka ikapeleka wapelelezi nchi nyingi ili wakalete tekinolojia na maarifa kwao sasa wako mbali , wakati wa vita kuu ya dunia wamarekani waliiba wanasayansi wengi wa ujerumani ambao walisaidia kujenga uwezo mkubwa wa jeshi la marekani na taasisi nyingine ndio maana ikawa mbabe wa dunia kwa kipindi kirefu .

Kumbuka kazi za upelelezi ni ngumu na zenye siri nyingi na kubwa sana , wapelelezi wengi pia wana mafunzo ya kujilinda , kupambana na kushambulia usijaribu kupambana nae kama una uhakika ni bora kutoa taarifa kwa vyombo husika wamshugulikie .

Mwisho upelelezi usitumike katika kutafuta taarifa mbaya tu , hapana , kuna taarifa nyingine nzuri zinaweza kutumika vyuoni , wizarani , kwenye majeshi na sehemu nyingine kwa ajili ya kuboresha au kujenga zana na vifaa vya kisasa

LENGO LA MAELEZO HAYA NI KUFUNDISHA, UKIKAMATWA KWA KAZI HIZI UNAWEZA KUUWAWA , KUTESWA NA KUPOTEZA MENGI

By Yericko Nyerere

Kuanzishwa kwa shirika la Ujasusi Israel MOSSAD na nguvu yake duniani.

By:

Yericko Nyerere:

Watu kutoka miji mbalimbali ya Tel Aviv, Haifa na vijiji vya karibu ya bahari ya Galilaya ambapo wazee kwa vijana, wafanyabiashara, waalimu wa sheria za kidini na watu wa aina mbalimbali walipokuwa wamekusanyika katika hekalu la Herod the Great II katika mji wa Jerusalem katika moja ya kuta zinazoogopwa zaidi ulimwenguni, ambapo kwa wahayudi ni sehemu takatifu kwao kwa ajili ya kufanyia ibada na maombi, ukuta huo unaitwa Wailing Wall au Western Wall (The holiest shrine of the Jewish World). Katika karne nyingi zilizopita utamaduni huu umekuwa unafanywa mara kwa mara na wayahudi toka enzi za mababu zao.

Wakiwa wamevalia mavazi ya rangi nyeusi, kila mtu akiwa na kitabu chake cha maombi ambapo walikuwa wakipitia maandiko kadhaa katika vitabu vyao huku wakifanya maombi mbele ya ukuta huo, sabato hii haikuwa kama sabato nyingine zilizo zoeleka, sabato hii ilifanyika Septemba 1929 na ilikuwa ya tofauti kidogo, waalimu wao wa dini (rabbis) waliwataka watu wakusanyike kwa wingi, sio kwa sababu tu ni haki yao kufanya hivyo bali kuonesha alama ya umoja wao na uyahudi wao na kuwakumbusha waarabu waliokuwa wamewazidi kwa idadi kuwa licha ya wingi wao hawataweza kuwatawala wala kuwaonea. Na kwa miezi kadhaa nyuma jamii ya waislamu miongoni mwa waarabu walikuwa na wasi wasi na hasira juu ya kile walichokiona kupanuka na kusambaa kwa uyahudi katika eneo hilo, na wasi wasi huo ulikuja kutokana na na azimio la Balfour (Balfour Declaration) lililonesha kuwepo kwa makazi rasmi ya wahayudi katika ardhi ya Wapelestina. Waraabu hawa walikuwa na wasiwasi kuwa ardhi waliyoilima kwa kipindi kirefu inaweza kuangukia mikononi mwa wayahudi na kupoteza haki ya umiliki wake na waarabu hawakutaka hili litokee hata kidogo.

Huku Jerusalem wayahudi wakiwa katikati ya maombi mara kulisikika tafrani ambapo walianza kurushiwa mvua mawe na chupa zilizovunjwa na baada muda kadhaa pia milio ya risasi ilisikika kutoka kwa washambuliaji hao. Rapsha hiyo ilisababisha watu kuanza kukimbia hovyo na kukanyagana kila mtu akiwa katika harakati za kukimbia ili kukwepa shambulio hilo na kuokoa uhai wake, kwa bahati nzuri hakuna mtu aliyekufa ila kulikuwa na majeruhi lukuki. Usiku uleule viongozi wa Yishuv, (Yishuv ilikuwa ni jamii ya wayahudi waliokuwa wanaishi maeneo ya Palestina) walijadiliana kwa kina kuhusu maandamano waliyoyapanga na kuyafanya kwa umakini mkubwa na ujumbe waliokuwa wanataka kuutoa kuwa haukuzingatia tishio la wapalestina kuweza kuja kuwashambulia katika eneo lao hilo takatifu la kufanyia ibada.

Kutokana na kipindi hicho watu wa Israel na Palestina wote walikuwa chini ya utakuwala wa kiingereza na wote wakitegemea ulinzi kutoka kwa mtawala wao huyo, kwa tukio la Israel kushambuliwa na waarabu wa kipalestina, wayahudi waliona palikuwa hakuna haja tena ya kutegemea ulinzi huo ulioshindwa kuwalinda katika eneo lao takatifu hivyo wakaamua kuanzisha kikosi chao cha ulinzi kilichojulikana kama Hanagah neno la kiebrania linalo maanisha ulinzi, ili kuwalinda wayahudi na nchi yao sababu waliona kabisa kuwa hawataweza kuacha kufanya ibada na maombi katika sehehemu yao hiyo takatifu ya Wailing Wall. Hanagah kama taasisi ya ulinzi na pia ya kijajusi ilikuwa inafanya kazi ya kuhakikisha inapata taarifa zote muhimu kuhusu aina yeyote ya hatari inayoweza kufanywa na waarabu na maadui wengine katika ardhi yao, ndipo kwa umakini mkubwa walifanya kila wanaloweza na walifanikiwa kuwa recruit baadhi ya waarabu wa kipalestina wafanye kazi hiyo kwa uhai wa taifa lao. Waalimu, wanafunzi na wafanya biashara wa kiyahudi waliokuwa katika aridhi ya wapalestina na vijana wa mtaani waliokuwa wanafanya kazi ya kusafisha viatu (shoe shines) vya maofisa wakubwa wa kipalestina nao walikuwa watu potential sana katika upatakanaji wa taarifa mbalimbali kwa Hanagah.

Katika kikao kilichofanywa na David Ben-Gurion and Yitzhak Rabin (Waanzishaji wa Hanagah) katika mji wa Haifa mwaka 1942, walikubaliana kuwa ilibidi wahanga waliokuwa wanapata mateso chini ya utawala wa Nazi ulioongozwa na mbabe aliyefahamika kama Adolf Hitler nchini Ujerumani kuwa inabidi ifanywe mipango na warudi nyumbani, hakuwa na uhakika ni idadi gani ya watu itawasili katika viunga vya miji yao ila cha msingi ilikuwa ni kuwarudisha watu kwenye nchi yako ili kufanya kile walichokiita ‘’kupigania uhuru wao’’. Katika kipindi hiki Hanagah ilikuwa ni moja ya shirika la kijasusi makini sana katika ardhi hiyo takatifu ulimwengun katika nchi zote za mashariki ya kati. Na katika mwaka 1945 Hanagah chini kitengo chake kinachohusika na upatikanaji wa silaha, kilifanikiwa kupata silaha nyingi Kaskazini mwa Afrika katika vita kuu iliyokuwa inaendeshwa na Italia na Ujerumani, siliha hizo kwa umakini chini ya wanajeshi wa kiyahudi zilipelekwa na kufichwa katika mapango Israeli katika eneo linalodaiwa kuwa shetani alimjaribu Yesu mara tatu lakini akashidwa.

Baada ya kupigwa kwa Japan mwaka 1945 makomandoo wa Israel waliokuwa vitani kipindi hicho walirudi nchini kwao kuongeza nguvu na ujuzi wao kwa Hanagah. Mwaka 1946 chini ya Ben-Gurion ilitoka amri kuwa sasa ni wakati kuwa na utawala kamili wa aridhi yao kwa kupigana na yeyote atayegusa maslahi yao na hapo walidhamiria kupigana na waarabu na waingereza wote kwa pamoja. Japo waisraeli walijua kuwa ni karata ya hatari kuicheza ila waliona hakuna budi kufanya hivyo kwa ajili ya uhai wa taifa lao. Katika vita hiyo wanajeshi wengi wa Uingereza waliuwa na vijiji vingi vya wapalestina vilipigwa kiberiti na wakabaki wanashangaa wingi huu na nguvu ya wa Israeli imetokea wapi?

Waingereza na waarabu katika eneo hili walikunatana na nguvu wa wayahudi ambayo hawakuitarajia na wasingezewa kuhimili hali ile zaidi na mnamo mwaka 1949 waingereza waliamua kuondoka eneo hilo la mashariki ya kati na kurudi kwao na masuala yote ya usimamizi wa nchi hizo yakaachwa chini ya usimamizi wa umoja wa mataifa (UN). Kutokana na maadui sasa kuwa mbali kidogo ndipo Ben-Gurion alipoamua kutengeneza shirika la kijasusi imara litakalo kuwa na watu makini na wenye akili katika kulinda na kutetea maslahi ya Israel. Kutokana na kwamba Hanagah ilikuwa kama imegawanyika kutika harakati zake nje ya mipaka ya Israel, ambapo mawaziri na mabalozi wake walipendekeza vitu walivyopenda wao ndio vifanywe na shirika hilo. Hali hiyo ilionesha kuwa ya hatari kwa uhai na maslahi ya Israel ndipo mnamo March 2, 1951 kiongozi wao huyo alisikliza mapendekezo yote na akaamua kuwa nchini Israel kutakuwepo na shirika moja imara, litakalo fanya kazi kwa umakini na ustadi wa hali ya juu kuiweza nchi kuishi milele katikati ya msitu wa maadui ambao umewazunguka na shirika hilo la kijajusi litailinda Israel kwa njia yeyote ile na shirika hilo litaitwa Ha Mossad le Teum, “the Institute for Coordination.” Maarufu kama Mossad.

Itaendelea….

By Yericko Nyerere

Kilele cha Kejeli: Kikwete Umenikwaza… “Barua ya Mkosaji”

By: Mzee Mwanakijiji
Mheshiwa Rais tafadhali.

Kwa kweli umenikwaza na ninajisikia nimeumia sana moyoni na mawazo yangu yako kama sufuria lililoandaliwa kwa kupikia pilau; mchele hauwekwi yanachemka mafuata na viungo. Harufu tu kwa mbaali vya kupikwa havipikwi nimebakia kula kwa harufu. Umenikwaza kwa sababu nilitarajia safari hii na mimi ungenikumbuka kama ulivyowakumbuka na wale. Teuzi zako za hivi karibuni za wakuu wa mikoa, mawaziri, manaibu waziri na sasa wakuu wa wilaya umenifanya niamini kuwa ama umenisahau, umenipuuzia au hujaona mchango wangu mkubwa.

Mheshimiwa Rais kumbuka mimi nilikuwa na nimeendelea kuwa mtetezi wako mkubwa wa utawala wako hata pale ambapo watetezi wako wengine walipogeukua kuwa walalamikaji wako. Nimekutetea hata kwenye visivyoteteeka na hata vilivyotetereka nilijaribu kuvitetea! Nimejitahidi kwenda nao mano a mano na wale wote ambao walikuwa wakikurushia madongo au kukulaumu wewe kwa madudu ambayo yamekuwa yakitokea chini ya utawala wako. Lakini naona umenisahau.

Nimebaki na maswali mengi hata Mama Chanja amenishangaa leo sijala – anadhani nimefunga Kwaresma! au nawaunga mkono Wakristu kwenye Jumatano ya Majivu! Kumbe mwenzie nimeghafilika moyoni na kwa kweli nimekwazika. Nimejikuta niko kama yule Waziri wako fulani ambaye ulimtupa nje akalazimika kujiuzulu kwa kashfa pale Bungeni. Maneno yake yale naweza kufanya yangu; “Nimeumia sana, nimekwazika sana”.

Kumbuka Mheshimiwa Rais – Dakta wa madaktari, Profesa wa Maprofesa – mimi nilikutetea tangu wakati wa ile kashfa ya kwanza kabisa; ya mapanki na ndege za Warusi. Wakati ulipojitokeza na kusema kuwa watu wetu hawali mapanki na kuwa filamu ile ya Hubert Sauper ilikuwa imelenga kukashfu jina zuri la nchi yetu. Wengine waliwaunga mkono wale watengenezaji filamu na hawakuweka uzalendo wa kutetea nchi hata ikiwa imechafuka. Nilikuwa mmoja wao wa waliosema “nchi yangu kwa ubaya au kwa uzuri”. Nilitetea na niliunga mkono lile tamko la Bunge kukuunga mkono; ningepitwaje vile; nichekwe? Nilijua siku ikifika na mimi utanikumbuka.

Hata ilipokuja ile kashfa ya Richmond wakati wengine walikuwa wanajaribu kukuunganisha wewe na kashfa ile na uongozi wako mimi nilikutetea hata kichinichini. Sikutaka kabisa uonekane kwa namna fulani ni sehemu ya tatizo lile. Na Sikuishia kwenye Richmond tu; nilikutetea kwenye Poormond, Failmond ya shule zetu na hata hivi majuzi mlivyowatumia wasanii kuuza uzuri wa chama chetu/nu nilikutetea kwenye suala la Diamond!

Mheshimiwa Rais nimekutetea katika jua na mvua, baridi na joto hata ilipodibi kuupindisha ukweli a.k.a kuongopea – nilijaribu ilimradi Rais wangu ujue kuwa tuko baadhi yetu tunaokuamini uongozi wako maridhawa na kuwa kama shukrani yako kwetu utatukumbuka na sisi wengine. Kama uliweza kumkumbuka Adadi Rajab, washikaji zako wa Imma na hata yule Generali Shimbo na vijana kama kina Mrisho Gambo nilijua tu siku yangu itakuja na mimi nitakumbukwa.

Yaani umeweza kumbuka Makonda na hata yule jamaa aliyewahi kuwa Konda lakini umeshindwa kweli kunikumba na mimi? Hivi kweli unaweza kulinganisha michango yangu kwenye JamiiForums, Twitter, Facebook, Eastergram na hata Whatsap na michango ya hawa wengine? Kwa vile ni wazi nafasi hizi hazihitaji ujuzi fulani maalumu – kitu ambacho na mimi ninacho – kweli umeshindwa na mimi kunirusha mahali fulani japo angalau na mimi niwemo kwa wenye kuwemo? Yaani Makonda yumo mimi simo? Yaani jamaa wa Mpira umemkumbuka lakini mimi nisiye na masihara umenitupa?

Sasa, mheshimiwa; mimi nina pendekezo. Nitaendelea kukutetea na kuutetea utawala wako dhidi ya wale wote wenye kuutaka uonekane ni utawala wenye upendeleo, wenye kuzawadia uzembe na kulinda wabovu. Nitakutetea dhidi ya yale wote wanaotaka ukumbukwe kwa jini gani utawala wako unaweza kuliacha taifa katika hali ile ile uliyoikuta (mwamko mpya wa ujambazi! na kashfa). Nitajitahidi kukutea hata pale ambapo sera za chama zinaweza kufanywa zionekane zimefeli kwa kila kipimo nikiwakumbusha kuwa sera zetu hazijafeli kama za tawala tatu zilizotangulia; zimefeli kidogo zaidi kulinganisha na wao. Nitaendelea hivi kwani nina imani ya kwamba utanikumbuka.

Mheshimiwa umebakiwa na miezi michache tu; sasa unapowazawadia hawa wengine ambao si chochote wala lolote na hawajatoa mchango mkubwa kama wa kwangu na nyumba yangu. Unajua hadi mapazia yangu yana picha yako; wanangu wanavaa tsheti zile za uchaguzi hadi leo. Watu wanatujua kuwa sisi ni wakereketwa wa Kikwete. Kila unapoenda nje kupewa tuzo na sisi nyumbani kwangu tunafanya sherehe na tunatangazia jamii (nikitarajia neno litakufikia).

Sasa chonde ewe kipenzi chetu eh; wewe uliye na madaraka yote na mwenye uwezo wote wa kuwakumbuka unaotaka kuwakumbuka. Nakuomba na mimi unikumbuke. Ila hata kama ukinikumbuka miye inaweza kuwaletea nongwa wengine basi mkumbuke hata mke wangu. Unajua naye anakupenda sana wakati mwingine hadi mwenyewe nasikia wivu sijui anakupendea nini. Ila nna uhakika ukimkumbuka na yeye basi na miye nitahemea humo humo si umewakumbuka na wake za wenzangu wengine hata ubalozi. Mama Chanja anasema hata ukimpa Ubalozi wa Zimbabwe atashukuru!

Ninachokuomba na mimi unikumbuke. Unikumbuke na mimi nisije kuadhirika. NImekuwa mwaminifu sana kwa utawala wako kiasi kwamba hata wapinzani wamejaribu kuninanga sana lakini wamekwama. Naomba unikumbuke ili niwakate kizabizabina kabla hujaondoka maana ukiondoka ikifika Oktoba. Sisi wengine tutaumbuka.

Na kimbelembele chetu cha ushabiki.

Ni Mimi Mkosaj

By Yericko Nyerere

Tanzania Intelligence agency

By: Wikileaks Spy

INTRODUCTION

TPSC uses specialist intelligence teams who are able to procure information for private and corporate clients. The methods employed by us are extremely discreet, legal and very effective.

Our agents are able to gain useful information about individuals, and companies and their employees. We are able to trace and monitor their movements, communications, contacts, financial deals and assets.

For corporate operations we are able to obtain information about companies, competitors, directors, company’s future and present plans as well as finance, hidden deals, mergers acquisitions and also staff.

Corporate intelligence services

When a company needs to make an important commercial decision, they need to rely on facts, information data and knowledge of outside influences. If the information available at the time of making a decision is inaccurate or there are vital details missing the result can be at the least embarrassing, but could also be catastrophic for the company concerned.

Tanzania Private Investigation agency team of intelligence agents are able to provide accurate information that is needed to make an informed decision.

They will work quietly and effectively to ensure that all the facts are extracted and validated, before being passed discreetly on to the client. Tanzania Private Investigation agency professional intelligence service can also be extremely beneficial to a company wishing to gain the “informed advantage” over another competitorPrivate intelligence services

Our agents also have experience in obtaining personal information on individuals in a highly discreet and covert manner. They can search into someone’s background to reveal truths about their past and present.

We can investigate the movements of a partner, we can access data at almost any level to establish the facts, we can investigate calls and communications, purchases, travel, applications, and validate the information we gain before passing it back to the client

Counter Intelligence.

As part of our corporate services, it may be necessary to ensure the security of our clients privacy. This is carried out by our counter intelligence team and can be a one off service or part of an ongoing security measure.

What we offer

General investigation, Missing PersonTracing DebtorsChild abuse or molestationCheating SpousesInsurance InvestigationCriminal InvestigationArson and Fire loss Investigation,Unsolved crime InvestigationSurveillance, Private ClientsCorporate ClientsComputer forensics InvestigationUndercover InvestigationsWhite-collar Crime,Intelligence Services, photographic evidence, Fraud Prevention, criminal and civil legal cases, fraud, theft, stolen or counterfeit goods

By Yericko Nyerere

Ujasusi wa Ali Abdoul Saoud Mohamed, na funzo kwa majasusi wa kileo

By: Yericko Nyerere


Ali Abdoul Saoud Mohamed alikuwa double agent wa CIA na EIJ( Egyptian islamic jihad) ambayo ndio ilipelekea kuundwa kwa ALQAEDA huku yeye akiwa mwendesha mafunzo wa mbinu za kivita na kijasusi wa kwanza kwenye kambi zao kwa ajili ya kuwaandaa na mapambano dhidi ya utawala wa kisovieti nchini Afghanistan miaka ya 90. yeye ndiye mwalimu wa kwanza wa Osama bin Laden na Ayman Zawahiri( kiongozi wa sasa wa Alqaeda)

Ali anaelezwa kuwa mtu mwenye uzito wa kilo 90, urefu futi 6 huku akielezwa mtu aliye fiti kimwili, aliyebobea kwenye sanaa za mapigano( martial art),mwenye ufahasa mzuri wa lugha za kiingereza,kifaransa,kiyunani na kiarabu. alikuwa mwenye nidhamu ya juu, mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri, mwenye kujichanganya na watu na uwezo wa kupata marafiki kwa urahisi. 


Ali alikuwa major katika kitengo cha ujasusi katika jeshi la misri kabla ya kuachishwa kazi mwaka 1984 kwa tuhuma za kusika katika harakati za udini dhidi ya utawala wa Anwar Saadat wa misri, harakati zilizopelekea kuuawa kwa Saadat


Uhusiano wake na CIA
kwa mara ya kwanza aliingia marekani kama mkalimani wa Ayman Zawahiri( kiongozi wa sasa wa alqaeda) wakati alipoenda kuchangisha michango kusaidia wana mgambo katika harakati za kuutoa utawala wa wasovieti Aghanistan.kwa maelezo inasemekana Zawahiri alimshauri a-infiltrate marekani, mwaka 1984. Ali anaelezwa aliweza kuingia kwenya kituo cha CIA Cairo,Egypt kwa urahisi na kuweza kuongea na mkuu wa kituo kuhusu ofa yake ya kufanya nao kazi.hatimae akawa recruited kama junior intelligence officer. kazi ya kwanza aliyopewa ni kupenya ndani ya msikiti mmoja mjini hamburg ujerumani uliosemekana kuwa na mahusiano na wanamgambo wa Hizbollah wa nchini Lebanon lakini cha ajabu akawataarifu viongozi wa msikiti kuwa yeye ni jasusi wa CIA na ametumwa kuchukua taarifa, kwa kuwa katika ule mkusanyiko alikuwepo jasusi mwingine wa CIA, taarifa juu ya alichokifanya Ali zikawafikia mabosi CIA. Kwa mujibu wa mwandishi maarufu wa jarida la New Yorkers na mshirika wa kituo cha sheria na usalama New York University of Law bwana Lawrence Wright ni kwamba ulitumwa ujumbe wa kimawasiliano kutoka CIA ukitaarifu kuwa Ali sio mtiifu tena na ameshadhibitiwa, lakini mda huo taarifa inatumwa tayari Ali Mohamed alikuwa mjini Carlifonia kushiriki program maalum ya kuwapatia ruhusa ya kuingia marekani bila kuwa na visa kwa ‘Valuable assets’ waliolifanyia taifa la Marekani utumishi wa hali ya juu, program ambayo yenyewe pia ilikuwa ikifadhiliwa na CIA. Ali akafanikiwa kuoa mmarekani Linda Sanchez na baadae kidogo akachukuliwa kwenye special forces na akapangwa katika kambi kubwa ya Fort bragg kama drill commander( sijui kwa kiswahili wanaitwaje, yani wale ambao wanawapokea makuruta na kuwafundisha maisha ya jeshini, taratibu na nidhamu) pia alishawishiwa na CIA kusomea masomo ya dini ya kiislamu ili akafundishe mashariki ya kati


mnamo mwaka 1988 Ali aliwataarifu wakuu wake jeshini kuwa anachukua likizo fupi kwa ajili ya kwenda nchini Afghanistan kupambana na wasovieti( huko ndio akawa anatoa mafunzo kwa wanamgambo waanzilishi wa Alqaeda). Huku nyuma afisa mwandamizi wa Ali, Lt. Col Robert Anderson aliandika ripoti ya kina ikilenga kutaka idara ya ujasusi ya jeshi kumchunguza Ali na kumfungulia mashtaka lakini taarifa yake hiyo ilipuuzwa. anaeleza kuwa ” Kuwa na mwanajeshi mmisri, aliyehusika na mauji ya rais wa zamani wa misri Saadat, alafu akapata visa ya kuja kuishi marekani na kuchukuliwa kwenye vikosi maalum vya jeshi(special forces) inashangaza, haya mambo hayatokei tu hivi hivi” anaendelea kueleza kuwa ilikuwa ni vigumu kuamini kuwa mwanajeshi wa kawaida wa Marekani kupigana vita katika jeshi la nje bila kuadhibiwa. akaendelea kusema anaamini atakuwa anafadhiliwa na shirika la kijasusi la kimarekani.



Ali aliendelea kutoa mafunzo kwa wana mgambo wa kiislamu wa Maktab al-Khidamat (iliyoanzishwa na Abdullah Azzam ambayo baadae alijiunga Osama, wakagombana hatimae Osama akaigeuza kuwa ALQAEDA baada ya ku-win popularity over Azzam)nchini marekani kupitia Kambi ya Al Kifah iliyokuwepo mjini brooklyn iliyokuwa akisapotiwa na Marekani kwa ajili ya kuwawaezesha kuutoa utawala wa kisovieti nchini Afghanistan


miaka ya 90 akarudi tena Afganistani ambako alitoa mafunzo ya kijasusi ikiwemo, kuteka watu, kuteka ndege, jinsi ya kuua n.k na inasemekana katika wanafunzi wake wa kwanza kabisa ni Osama bin laden, Ayman Zawahiri(kiongaozi wa sasa wa Alqaeda) na viongozi wengine wa Alqaeda kwa mijibu wa FBI special agent Jack Cloonan


mwaka 1993 akiwa ndani ya Alqaeda akawa informant wa FBI, na mmoja wa wapigaji wa ALQAEDA Mohamed Atyf aliyepewa jukumu la kufanya survey katika ubalozi wa marekani nchini kenya(uliolipuliwa mwaka 1998) alikataa kumtajia Ali passport namba yake kwa kuwa alikuwa na mashaka kuwa Ali alikuwa ni mshirika wa Marekani


wiki mbili baada ya balozi za marekani nchini Kenya na Tanzania kulipuliwa, FBI walisachi makao ya Ali na kukuta nyaraka mbalimbali zenye ushahidi juu ya kuhusika kwa na milipuko nchini Kenya na Tanzania na akakamatwa. Ali alikubali makosa ya kigaidi na akaeleza mwanzo mwisho kuhusu ushiriki wake katika kundi la Al qaeda, akakiri makosa ili apate kifungo cha maisha jela bila msamaha wowote ule


mwaka 2001 gazeti la Raleigh News and Observer lilitaarifu kuwa Ali anatoa ushirikiano kwa serikali ya marekani, anaeleza kamanda mstaafu wa Delta force katika kitabu chake cha The Mission,The Men and Me:Lessons from former Delta Force Commander,bwana Pete Blaber ”Mawakili wa utetezi wanaamini kuwa Ali hajahukumiwa na anasirikiana na serikali japo serikali haijathibitisha hilo,akihukumiwa anaweza akahukumia kifungo kidogo, kama miaka 25 kwa mujibu wa makubaliano yao”

mwaka 2006, mke wa Ali Linda Sanchez alisema kuwa mumewe bado hajahukumiwa na haruhusiwi kuzungumza na yeyote “yani wamemshikilia kiusiri sana, ni kama vile amepotelea kwenye hewa”

By Yericko Nyerere

CIA Says ‘Oops. Sorry.’ Capitulates on Intelligence Committee Spying Probe

.  By Jeff Stein from Spytalk

 

 

  Now they say they’re sorry. But last spring CIA Director John Brennan and his aides were telling anyone who would listen that the agency’s sleuths were justified in spying on Senate Intelligence Committee staffers investigating the CIA’s detention and interrogation program because they had “stolen” privileged documents.

Indeed, in a private letter to Senate Intelligence Committee chair Dianne Feinstein back in January, Brennan said he was “concerned that there may have been a breach … in the system for housing highly classified documents,” in particular relating to what the panel’s staffers had unearthed about his predecessor Leon Panetta’s knowledge of excesses in the interrogation program. Suggesting that the staffers might have committed a crime, Brennan referred the matter to the Justice Department for investigation, provoking a thunderous denunciation on the Senate floor by the panel’s chairman, Sen. Dianne Feinstein (D-Calif.).

Yesterday, however, Brennan was up on Capitol Hill hat in hand, apologizing to Feinstein and her Republican counterpart, committee Vice-Chair Saxby Chambliss (R-Ga.). The CIA’s inspector general, it turned out, had concluded that the agency’s sleuths had gone too far. “Some CIA employees,” the IG found, according to CIA spokesman Dean Boyd, “acted in a manner inconsistent with the common understanding reached between SSCI (Senate Select Committee on Intelligence) and the CIA in 2009.” Brennan, Boyd said, personally apologized to Feinstein and Chambliss “for such actions by CIA officers as described in the OIG (Office of Inspector General Report).”

The vehemence of CIA denials last spring leaves open the possibility that Brannan and his aides were misled by their subordinates, in which case there could be blood on the floor when further investigations are conducted. Boyd said the agency was setting up an “accountability board,” to be led by retired  Sen. Evan Bayh, an Indiana Democrat  who served on the Senate Intelligence Committee.

“This board will review the OIG report, conduct interviews as needed, and provide the director with recommendations that, depending on its findings, could include potential disciplinary measures and/or steps to address systemic issues,” Boyd said.

The kerfuffle is only the latest chapter in a long and often sulfurous struggle over the committee’s investigation of  the CIA’s so-called rendition, detention and interrogation program. An impending release of a summary of the report is expected to show that the agency officials withheld key details on what its operatives were doing and exaggerated their successes. According to the New York Times, former CIA Director George Tenet, who led the agency at the time of the 9/11 attacks, and other former agency officials have been furiously lobbying behind the scenes to refute the committee’s findings.

 

By Yericko Nyerere

Ripoti hii inathibitisha kuwa Tanzania na Rwanda zilishapigana vita.

By Wikileaks1 Spy

 

 

Baada ya kupitia ripoti nzima nikaona mambo mengine ya muhimu zaidi kwa Tanzania kuliko hilo. Naweza kuwa nakosea lakini sidhani kama mtanzania halisi mwenye mapenzi mema na nchi yetu anaweza kupitia ripoti hii na jambo pekee la kujadili atakaloliona likawa Mtikila na FDLR badala ya hili lililo wazi zaidi kuwa Rwanda iliishambulia Tanzania (pamoja na nchi nyingine) kinyume cha sheria za kimataifa. Labda zilikuwa jitihada za kujihami (pre-emptive strike) kuhamisha mada ya ripoti kwenda kwa mtikila, ili kutojadili haya mengine maana watanzania wengi hawapendi kusoma mambo marefu kama ripoti. Mimi kwangu la muhimu hapa ni haya.

 Samahani kwa kuchanganya lugha na vile vile labda thread hii inaweza kuwa ndefu, lakini ni vyema kuangalia kwa makini haya mambo yaliyoibuliwa na hii ripoti kuhusu uhusiano wa Rwanda na M23 na uhusiano wake na hizi cheche za sasa kati yetu na Rwanda.

 Ripoti nzima inapatikana hapa:Final Report of the Group of Experts on the Democratic Republic of Congo.pdf courtesy ya ndugu EMT.  pia nyingine inapatikana hapa: Inner City Press: Investigative Reporting from the United Nations

 Mambo niliyoona ni muhimu ni haya:

 

Executive summary:

 

· Wachunguzi wa UN WAMETHIBITISHA kuwa kundi la M23 limekuwa likipata misaada mbalimbali toka ndani ya Rwanda. Misaada hii inajumuisha: silaha, ammunition; yaani risasi, mabomu na vifaa vingine vinavyotumika na silaha, recruitment; yaani uandikishaji wa askari wapya wa M23, reinforcement; hii inamaanisha chochote kuanzia chakula, askari wa ziada etc, pamoja na fire support; Ripoti inasema kuna wakati askari wa Rwanda ndio waliokuwa wanapigana vita hivi moja kwa moja na majeshi ya UN (Tanzania ikiwamo) bila kificho cha kujifanya M23!

· Wamethibitisha kuwa viongozi waliowekewa vikwazo na Umoja wa mataifa wamekuwa wakiishi na kutembea kama watu huru nchini Uganda, na vile vile M23 wamekuwa wakijijenga upya kwa kuongeza wapiganaji wapya nchini Rwanda.

 

·  Kwamba vikundi mbali mbali vya waasi vimekuwa financed na biashara haramu ya madini hasa dhahabu. Uchunguzi umesema kuwa takribani asilimia 98 ya dhahabu yote inayozalishwa DRC inatoroshwa kiharamu. Ingawa dhahabu hii imekuwa ikitoroshwa kupitia nchi jirani za Tanzania, Uganda na Burundi karibu dhahabu yote imekuwa ikitoroshwa kupitia Uganda.

 

Standard of evidence: · Wataalamu hawa wa uchunguzi toka UN waliomba ushirikiano toka serikali za nchi mbalimbali na makampuni kusaidia uchunguzi, lakini katika kipindi chote cha uchunguzi wao serikali ya Rwanda ilikataa kuruhusu wachunguzi hawa wa UN kuingia Rwanda kwa shughuli hii. (page2).

 

M23:

· March 2013, kufuatia kumeguka vipande viwili kwa kundi la M23 kutokana na vita vya ndani (Bosco ntaganda vs Sultani Makenga) kamanda Bosco Ntaganda na kundi la wapiganaji wake 788 walikimbilia nchini Rwanda.

· Wachunguzi wamethibitisha kundi hili kupata ufadhili toka Rwanda mpaka mwisho wa October 2013, ikiwamo kuwasili kwa askari wa jeshi la ulinzi wa Rwanda (Rwandan Defence Forces) nchini DRC mwezi August, kuwasili kwa silaha mwezi juni, july na august. Wachunguzi wa UN waliandika barua kwenda serikali ya Rwanda kuomba maelezo juu ya masuala haya lakini mpaka ripoti hii inaandikwa, serikali ya Rwanda haijajibu. · Ingawa M23 imesema ilisema imesitisha uasi mwezi November tarehe 5 2013, wachunguzi wa UN wana taarifa za uhakika kwamba masalia na washirika wa M23 bado wanajijenga upya nchini Rwanda.

 

Vyanzo vya taarifa:

 

· Taarifa zimepatikana kutoka kwa waliokuwa wapiganaji wa M23 waliojisalimisha, askari walioasi jeshi la Rwanda (RDF), wakazi wa maeneo yaliyotekwa na M23, viongozi wa jamii eneo la kivu kaskazini, viongozi wa serikali ya congo, pamoja na maofisa wa UN. Wachunguzi waliandika barua 13 kuomba taarifa za M23 kwa serikali mbalimbali na mashirika, walipata picha za maeneo ya M23, walijionea wenyewe hali halisi katika maeneo ya M23 na maeneo jirani, walipitia ripoti za taasisi za UN, na vile vile walipitia taarifa zilizopatikana kutoka maeneo yaliyoshikiliwa na M23 baada ya M23 kukimbia. · Waliokuwa wapiganaji wa M23 (former M23 combatants) wanane (8), waliwaambia wachunguzi wa UN kuwa askari wa Rwanda waliokuwa wanauawa kutokana na vita hivi walikuwa wanarudishwa Rwanda kwa maziko au kupatiwa huduma za matibabu.

 

Mashambulizi maeneo ya raia nchini Rwanda na congo:

 

· Mwezi august, Serikali ya Rwanda ilidai kuwa risasi zilikuwa zinapigwa na askari wa congo (FARDC) kuingia nchini Rwanda, na ilitishia kupeleka jeshi lake RDF nchini DRC kutokana na hali hiyo. Lakini askari wa zamani wa jeshi la Rwanda pamoja na Monusco walifahamisha wachunguzi kuwa risasi zote kwenda Rwanda zilipigwa na M23. Pia ripoti ya October 1 ya EJVM kuhusu matukio hayo ya august ilitoa uhakika wa asilimia 80 kuwa risasi hizo zilitokea maeneo ya kibati-kibumba ambayo yalikuwa yanashikiliwa na M23 wakati huo. Hii inaonyesha wazi kuwa M23 na Rwanda walikuwa wanapanga mchezo mchafu. Kwa bahati mbaya mchezo huu mchafu ulimtoa kafara mama mmoja na kumuumiza vibaya mwanae kijiji cha Ihumure Rwanda. Yote hii ni katika kutaka kuhalalisha Rwanda kuingiza majeshi yake DRC ili kupigana kwa niaba ya M23 dhidi ya majeshi ya UN yakiongozwa na Tanzania. · Kati ya august 22 na 30, M23 walishambulia maeneo ya raia maeneo ya Goma yakiwemo kambi za wakimbizi, shule, baadhi ya nyumba, ambulance za UN na makazi ya askari wa UN.

 

Kuvunjika kwa M23:

 

· M23 walitumia fursa ya kusitishwa kwa mapigano kutokana na mazungumzo kujiimarisha kwa kupeleka silaha nzito frontline ikiwamo mizinga. Yaani wakati dunia inajua M23 wanataka amani kupitia mazungumzo, wao walikuwa wanatumia hiyo kama half-time break! October 18, M23 walizuia msafara wa timu ya EJVM ya UN kwenda kukagua ghala la silaha za M23, pia October 18, M23 walishambulia helicopter za South Africa (sehemu ya jeshi la UN), eneo la Kanyamahoro.

· Asubuhi October 25, M23 waliji-position strategically (kimkakati) katika eneo la mpaka wa DRC na Rwanda eneo la Kabuye na mlima Hehu, kitu ambacho kilifanya vigumu kwa jeshi la Congo kuwashambulia bila risasi kuingia Rwanda. Toka October 25 mpaka 27, M23 walisaidiwa moja kwa moja na vifaru vya jeshi la Rwanda mpakani mwa Rwanda na Congo eneo la Kabuhanga-Kabuye.  Kwa maana nyingine vita sasa ilikuwa ni UN (including Tanzanian forces) + FARDC vs M23+Rwandan Defence Force! Kwa lugha rahisi ni kuwa kimsingi Tanzania na Rwanda zilishawahi kupigana!

 

· Ingawa baadhi ya M23 walijisalimisha nchini DRC, na wengine wakakimbilia Rwanda, wengi wao chini ya sultani Makenga walikimbilia Uganda. Kumbuka kuwa wale wengine chini ya Bosco Ntaganda walishakimbilia Rwanda, kufuatia kutokuelewana baina ya viongozi hawa wawili.

Nov 19 serikali ya Uganda ilijibu kwa wachunguzi wa UN kuwa wapiganaji 1,445 wa M23 waliingia Uganda wakiwamo sultani makenga na Innocent kaina (viongozi). Pia serikali ya Uganda ilidai kuwa M23 walisalimisha silaha zao. Uganda inawahifadhi M23 katika eneo linaloitwa Hima ( kwa mnaofuatilia historia hili jina lina uzito wa kipekee ukizingatia kabila la wapiganaji wa M23, nikumbushe tu kuwa hizi si porojo hii ni ripoti ya UN! ), wilaya ya Kasese. Serikali ya Uganda iliombwa orodha ya wapiganaji hawa lakini mpaka ripoti inaandikwa hakuna jibu lililotolewa!

 

Wapiganaji:

 

· Wachunguzi wa UN wamesema kuwa raia walijiunga na M23 kwa njia tatu: kulazimishwa kwa nguvu na aliyekataa alipigwa risasi, kuahidiwa kazi au pesa.

· walihojiwa watu 31 (M23) toka DRC, Burundi na Uganda ambao walisema kuwa wote ni raia wa Rwanda waishio nchi hizo au wakimbizi toka Rwanda waishio nchi hizo (hongera tena kikwete kwa operesheni kimbunga)! (page 7). Ripoti hii imeonyesha wazi wazi kuwa kumbe M23 ni kundi la wanyarwanda na si la wacongomani wenye asili ya Rwanda kama Rwanda inavyotaka tuamini. Hivyo kuendelea kuwa na wakimbizi haramu katika nchi yetu ya Tanzania ingeweza kuleta mambo kama haya, lingeibuka kundi la kikabila “linalodai haki zake” maeneo ya kagera kule halafu tungeshangaa mbona “jeshi la waasi “ linakaribiana ukubwa na JWTZ, kumbe tunapigana na wooote toka Rwanda, congo, Burundi…!

· Wachunguzi wamethibitisha pia kuwa baadhi ya M23 toka Rwanda walikuwa ni askari wa Rwanda (RDF). Ninanukuu: “Former M23 officers and soldiers told the Group that demobilized RDF soldiers served in M23 as trainers and operators of heavy weapons. Four ex-M23 combatants told the Group that Maj. Kalissa Rwema is one ex-RDF officer who served as a trainer for M23 at Rumangabo. UN sources and two ex-M23 officers told the Group that an ex-RDF soldier known only by his nickname “Kifaru” was a crewmember in the T-55 tank that M23 used in combat (see S/2013/433, annex 5)”

Msaada wa Rwanda: nukuu mbalimbali toka kwenye ripoti:

 

· The Group has documented that M23 received continued support from Rwandan territory. The most consistent forms of support were through recruitment (see above) and provision of arms and ammunition, particularly during periods of combat. M23 also received direct troop reinforcement by Rwandan soldiers in August. During the October fighting, Rwandan tanks fired into DRC in support of M23.

 

· In August, RDF soldiers crossed into DRC for short periods of time to join M23 and participate in combat operations. Ten local residents in Kibumba, and four ex-M23 combatants told the Group they witnessed these arrivals during the fighting in August, including between 22 and 24 August and on 27 August. Troops came notably through Rwanda’s Kabuhanga border post. In addition, a Rwandan Special Forces soldier – who previously served with the RDF in Darfur as part of the UNAMID peacekeeping force (see annex 18) – told the Group he deployed in August from Mudende as part of a reinforcement operation. While some RDF soldiers directly joined M23, he escorted a commander to the slopes of the Karisimbi volcano, from where they had visual surveillance of the M23-controlled area and communication links with RDF forces operating with M23. RDF reinforcements were also confirmed by two additional RDF deserters, one demobilized RDF officer, FARDC officers as well as MONUSCO sources.

 

· Swali gumu: rejea paragraph hiyo juu. Tulipoteza askari wetu wa kulinda amani Darfur kwenye mazingira tata. Hapa tuna ushahidi usiopingika kuwa askari wale wale tunaopigana nao DRC wakijifanya M23, ndio wale wale “tunashirikiana” nao Darfur….haiwezekani tukawa tumefanyiana hujuma?

· The Group documented that during the final combat, RDF tanks were present at the Rwanda-DRC border, in Kabuhanga, Rwanda and Kabuye, DRC. Numerous eyewitnesses in Kabuye pointed out to the Group where, on 25 October, two RDF tanks had crossed the border and entered Kabuye; additional RDF tanks were positioned just on the other side of the border, in Kabuhanga. According to corroborating testimonies from 15 people displaced from the border area to Goma, and 10 local residents who stayed at Kabuye, on 25 October, the RDF tanks in DRC and Rwanda fired toward FARDC positions. In addition, FARDC commanders and troops, a foreign journalist on the ground, and a diplomat confirmed that RDF tanks had fired from the border at Kabuhanga and Kabuye starting on the afternoon of 25 October and continuing until 27 October. The tank fire prompted most of the population of Kabuye and other border villages to flee to Goma and to neighbouring villages in Rwanda.

· On 6 November, the Group wrote to the Government of Rwanda to clarify this event; however, as of the writing of this report, the Group has not received a reply.

 

· Twenty-eight former M23 combatants, local people living in DRC close to the Rwandan and Ugandan borders, Congolese authorities, and UN sources told the Group that M23 had received deliveries of arms and ammunition through the Kabuhanga-Kabuye border crossing with Rwanda and the Bunagana border with Uganda. These sources stated 10 that ammunition usually came at night in trucks, and included rifle and machine gun ammunition, 12.7 mm rounds, anti-tank rounds and rocket-propelled grenades. Six ex-combatants told the Group they saw white trucks bringing ammunition through the Kabuhanga border crossing from Rwanda during June, July, and August. Several former M23 combatants told the Group they personally ferried ammunition from Kabuhanga, Rwanda into Kibumba, DRC.

 

Hitimisho Langu:

1. Kwa ushahidi huu wa ripoti ya UN tunajua kuwa Rwanda imehusika moja kwa moja kwa vifo vya askari wetu DRC. Serikali yetu itafanyaje kuhakikisha Rwanda inakuwa held accountable kwa haya maovu iliyofanya? Waziri Membe atasema haya? Wawakilishi wetu UN watashitaki New york? Waziri wetu wa EAC atasema haya bunge la Afrika mashariki? Au wote watafutika vichwa chini kama mbuni na kutumaini kuwa tukizidi kumpenda kagame, kagame atabadilika? Askari wetu ndio wamepotea hivi hivi? Habari za Rwanda kuwa wao ndio M23 hazitoki Tanzania wala FDLR, je si marekani na uingereza zilizosimamisha misaada kwa Rwanda ajili ya taarifa hizi kabla hata ya ripoti hii ya UN kutoka? Sasa ripoti ya UN imetoka na imehakikisha yote kuwa ni kweli. Je mpaka nini kitokee ndio Rwanda ishitakiwe UN? Waziri Membe atayasema haya au ataona haya? yetu macho!

2. Tunatakiwa tuangalie kwa umakini propaganda zinazoenezwa na vyombo vyenye uhusiano na serikali ya Rwanda ambavyo vinajenga picha hasi dhidi ya Taifa letu la Tanzania: kuwa rais wetu ana kisasi na Rwanda kwa kuwa mkewe ni nduguye marehemu Habyarimana, nchi yetu inafadhili majeshi ya FDLR na kadhalika. Hapa nitoe angalizo kuwa tusiiangalie Rwanda kama nchi ndogo. Silaha kubwa wanayotumia Rwanda ambayo watanzania wengi hatuijui si wingi wa askari bali propaganda za uchafuzi kama hizi.Tuhuma kuwa nchi yetu ni kimbilio la watu walio chini ya vikwazo vya kusafiri vya UN ni tuhuma nzito, tuhuma zinazobidi kujibiwa mapema, na vile vile kurudisha mapigo (kisheria) kwa yoyote anayezitoa bila ushahidi.

 Taswira yetu ikichafuliwa vya kutosha itaonekana ni vita kati ya Daudi (Rwanda) na nduli/dhalimu goliati (Tanzania). Watapata misaada toka nchi kubwa, wataungwa mkono na jumuiya za kimataifa, tutawekewa vikwazo, tutatengwa n.k matokeo yake tutaanguka kama mbuyu unavyoangushwa na shoka, huku tukiendelea kujisifu kuwa tuna jeshi kubwa. Tukumbuke jinsi utawala wa sasa wa kagame ulivyoingia madarakani. Kagame na jeshi lake hawakuwa tishio sana kwa Rwanda mwaka 1990. Lakini kupitia propaganda na manipulation ya jumuiya za kimataifa waliweza kujenga picha hasi ya utawala wa Habyarimana (na sisemi kwamba Habyarimana alikuwa malaika, la). Uchumi wa ndani ya Rwanda ukaporomoka, kukawa na matatizo ya kisiasa ndani ya Rwanda. Wananchi wakakosa umoja. Baada ya uchafuzi huu dunia nzima ikasahau kuwa Kagame alikuwa muasi aliyeshambulia kijeshi nchi huru ya Rwanda kwa miaka minne toka mwaka 1990 mpaka mwaka 1994 (kama ambavyo M23 ilivyofanya), badala yake ikahamisha focus kwenye genocide ya siku 100 tu, kana kwamba waliouawa miaka yoote hiyo walikuwa ngedere!

3. Tukumbuke kuwa huku Afrika nchi zenye baraka kama Tanzania zenye gesi, mafuta, madini ya urani, n.k hazitakiwi kuwa na amani. Si porojo kuwa nchi kubwa zitakazotuwekea vikwazo na kuvuruga stability ya ndani kwetu ni wale wale wanaotuchekea leo na kutuita marafiki. Kutokuwapo kwa amani nchini DRC hakujawahi kuzuia maslahi ya marekani, ubelgiji, n.k. Paul Kagame kapindua serikali ya Uganda (chini ya NRM), kapindua serikali ya Rwanda (chini ya RPA/RPF), kapindua serikali ya Congo DRC na anaendeleza uasi wa M23 mpaka leo (rejea ripoti), lakini ukiwauliza nchi kubwa leo hii nani Rais bora Afrika usishangae kusikia ni kagame huyo huyo

 Mwenye masikio na asikie!

 

 

 

By Yericko Nyerere

Itikadi ya CHADEMA

3.1.1 CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI (center party).  3.1.2 CHADEMA ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao.

 3.1.3 CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.

 3.1.4 CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboresha huduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote.

 3.1.5 CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri.

 3.1.6 CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki.

 3.1.7 CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa.

 3.1.8 CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu ya kijamii.

 3.1.9 CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola.

 3.1.10 CHADEMA inaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu.

 3.1.11 CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha uchumi.

 3.1.12 CHADEMA inaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.

 CHANGIA M4C tuikomboe Tz dhidi ya mkoloni mweusi ccm

By Yericko Nyerere

Revealed: Seven Tanzania-tycoons-with-offshore-accounts

By Wikileaks01 Spy

Seven Tanzanians have about $40 million (TSh64 billion) stashed in offshore accounts in British Virgin Islands and Jersey, The Wikileaks01 can reveal today.

 The revelation comes in the wake of reports that the committee set up by the Tanzanian government to trace the owners of the $196.87 million allegedly kept in Swiss banks has failed to come up with adequate evidence.

 According to leaked offshore data obtained by the UK’s Guardian newspaper in collaboration with the International Consortium for Investigative Journalists (ICJ) and analysed by over 110 journalists worldwide, seven Tanzanians operate offshore accounts.

 The ICIJ’s exploration of offshore secrets began when a computer hard drive packed with corporate data arrived in the post. Gerard Ryle, the ICIJ’s director, obtained the small black box as a result of his three-year investigation of Australia’s Firepower scandal, a case involving offshore havens and corporate fraud.

 The hard drive contained more than 260 gigabytes, the equivalent of half a million books. Its files included two million emails and four large databases. There were details of more than 122,000 offshore companies or trusts, and nearly 12,000 intermediaries (agents or “introducers”).

Unlike the smaller cache of US cables and war logs passed in 2010 to WikiLeaks, the offshore data was not structured or clean, but an unsorted collation of internal memos and instructions, official documents, emails, databases and spreadsheets, scanned passports and accounting ledgers.

 The leaked data, also seen by [private daily] The Citizen, could shed light on how the offshore account holders operate to avoid being detected by relevant authorities.

 The Citizen understands that there are legitimate uses for offshore companies and trusts. This being the case, the revelation of Tanzanians operating offshore accounts does not intend to suggest or imply that the individuals have broken the law or obtained their billions illegally.

 According to the leaked data the seven individuals, listed as officers and master clients, all have addresses in Dar es Salaam.

 They are Mr Andre Schmid, Mr Kaniz Mehbub Manji, Mr Mehbub Yusufali Manji, Mr Rameshchandra Chotalal Somani, Mr Stuart Hugh Macdonald and Mr C Rameshchandra Somani.

 It is not clear whether these Tanzanians acted as underlying officers in offshore banking or are the real owners of the billions wired into their accounts in Virgin Islands.

 

By Yericko Nyerere

LEMA: Mh Rais Kikwete, mbona umeamua kuangamiza Taifa?

By
Godbless J Lema

Mh Rais, nakusalimu!

 Kauli yako iliyonukuliwa na vyombo mbambali mbali vya habari wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wako wa NEC (CCM ) ni kauli hatari na yenye laana kubwa sana ya damu za Watu wengi katika Taifa letu. Ninaona wakati mgumu mwingine ambao Taifa letu linaingia kwa sababu ya kauli yako ambayo sasa imetangaza mauaji rasmi yatakayoongozwa na Viongozi mbali mbali wa CCM Nchi nzima huku Polisi wakiendelea kusimamia kama kawaida yao.

 Mh Rais , Kwa mujibu wa maneno yako umethibitishia Umma wa Watanzania kuwa mmejadiliana kwenye kamati Kuu na kukubaliana kuwa sasa yale mambo mliyokuwa mnayafanya kwa kificho sasa yamethibitishwa na Kamati Kuu ya Chama chako na kutangazwa na wewe mwenyewe kuwa , kuumiza , kuua , kutesa na kudhalisha sasa imekuwa sera rasmi ya CCM na umeithibitisha kauli hiyo mbele ya Wajumbe wa Baraza Kuu la CCM ( NEC).

 Mh Rais , kwa kauli hii naomba nikuambie kuwa umeamua kumalizia kipindi chako kwa mikono iliyojaa Damu na Roho za Watu . Nafasi uliyonayo ni kubwa sana sio jambo jepesi kuona makosa makubwa au madogo na kutubu , wapambe ni wengi ambao kwa kumsifu Mfalme hata kwa ujinga maisha yao na ya watoto wao yataendelea kuwa bora , lakini nakuhakikishia kwa kauli hii iko siku utajuta na kulaani ni kwanini ulitoa kauli mbaya na yenye hatia kama hii kwa Kiongozi mkubwa wa Nchi kama wewe . Vijana wa CCM sasa wamejipanga kuua na kuchinja hadharani kama ambavyo umeagiza wafanye na Polisi watakuwa Kimya kabisa kama ambavyo siku zote wamekuwa lakini mara hii watasaidia wazi wazi kabisa unyama wote utakaofanywa kwani wao pia wamesikia Amri yako na wewe ndio Mkuu wa Nchi hii.

 Mh Rais, mambo mengi yanachangia kuvurugika kwa Amani lakini moja kubwa ni pale Polisi na Mahakama zitakaposhindwa kutenda wajibu wake katika kutenda haki haswa pale uonevu unapokuwa dhahiri . Naweza kutambua matendo yote mabaya yanayotokea wakati wa Uchaguzi kuwa yamesababishwa na Upendeleo wa Jeshi la Polisi kwa Wanachama wa CCM pindi wanapofanya uhalifu dhidi ya wenzao wa Vyama Vingine vya Siasa. Mwaka jana 2013 wakati wa uchaguzi wa marudio wa Madiwani wa kata nne Arusha Mjini watu zaidi ya 16 waliumizwa vibaya na Green Guard na matukio yote yaliripotiwa lakini mpaka leo hakuna Mtu aliyefikishwa mahakamani kujibu mashitaka, lakini unakumbuka na unajua kuwa mkutano wetu wa kufunga Kampeni hizo za Udiwani ulipigwa BOMU na Watu Wanne waliuuwa na Zaidi ya 100 kuumizwa vibaya na wengine wamebaki na Vilema hata leo na tumekuomba uunde tume ya Kimahakama ili tukuletee Wauaji wa watesaji wa tukio hilo lakini mpaka leo umegoma na badala yake zimekuwepo jitihada nyingi zinazofanywa na Jeshi la Polisi kubambikia Watu kesi nikiwemo mimi na kutesa watu kwa kiwango ambacho hakielezeki.

 Mh Rais, Watu wameteswa na wanaendelea kuteswa sana katika Nchi hii na kazi hiyo inafanywa na Polisi na ccm na hapa ndipo mashaka katika jamii yanatokea na Jamii kuona ulinzi wao huko mikononi mwao na sio mikononi mwa Polisi na sheria za Nchi. Sasa umetangaza Watu wapigwe na wachinjwe hadharani , jambo ambalo nina uhakika nalo ni kwamba umeamua kuangamiza Nchi uliyoapa kuitetetea na ulioagiza wapigwe sina uhakika kama watakua wamelala chini wakati wanapigwa au wamefumba macho wakati wanateswa na kama itakuwa kinyume maana yake kutatokea Ugomvi ambao madhara yake mimi kwa sasa sielewi ila wewe MKUU uliyotoa amri utakuwa unajua.

 Mh Rais, Wewe wewe ndiye Amiri Jeshi Mkuu umeshindwa kuamrisha Polisi walinde Raia na mali zao na sasa umeamua Watu wachinjane? kwa kauli hii unasubiri nini Ikulu ? Hata hivyo Nguvu ulizonazo sio Imara sana kama Nguvu alizonazo Mwenyezi Mungu . Mateso na Damu iliyomwagika katika Taifa hili kwa uzembe wa utawala wako hakika utalipa kama sio wewe Watoto wako na Wajukuu zako elewa kuwa hakuna dhambi itakayopita bila kulipwa. Kauli yako hii inaleta hofu kubwa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015 lakini hatutaogopa kufanya kampeni kwa sababu Rais ameruhusu tupigwe na tuchinjwe, tutasonga mbele kutafuta haki tunayoamini kama ambavyo pamoja na matangazo mengi ya malaria kuua lakini hatujawahi kutembea huku tumevaa chandarua .

 Mh Rais wewe sio Mungu , hata hivyo unamkumbuka Jean Kambanda aliyekuwa Waziri Mkuu wa Rwanda mwaka 1994 alishatakiwa kwa kutoa kauli kama yako na kugawa mapanga kwa Vijana wa Nterahamwe na kusababisha mauaji makubwa sana Rwanda na tarehe 18/7/1997 alikamatwa Nairobi na baadae alishitakiwa na kufungwa Maisha kwenye mahakama ya ICTR Arusha na hii ilikuwa tarehe 4 sept 1998, sikufundishi uoga hata kidogo ila ni muhimu kujadili historia muhimu kulingana na wakati.

 Mh Rais thamani yako haitatokana na kusababisha CCM iwe madarakani tena bali Haki kuwa madarakani katika kipindi ulichotawala ni hekima ngumu kuielewa lakini ni lazima tuiseme. Tunaenda Kalenga kupigwa na kuchinjwa kwa sababu tu umewapa Watu wako ujasiri wa kufanya hivyo lakini elewa kuwa kila tukio litakalosababishwa na kauli zako ni tukio ambalo utalipa gharama zake. Makala zangu kama hizi uwezi kuzipenda sana Mh Rais, Wapambe watakuambia huyu kijana ni muhuni na maneno mengi ya kejeli lakini elewa kwamba anayekupenda ni anayekuambia ukweli, kwani ukweli thamani yake ni kubwa mno hata kama una madhara ya muda.

 Mh Rais, Ninapata hofu ninapoandika waraka huu kwani kama ni kwazo basi unaweza kuamua kufanya chochote dhidi yangu lakini napata faraja kuwa kifo kipo tu hata kama utafuti haki na ukweli kwani Bibi yangu kule Machame hakufa kwa kuwa aliandika waraka bali ni umri tu ulimuondoa. Mh Rais ukweli nakuambia usipofuta kauli yako yenye lengo baya kwa Nchi yetu basi nimemuomba Mungu afanye jambo muhimu dhidi yako na jambo hilo muhimu liko wazi kuwa kama wewe ni chanzo cha Taifa kuharibika kwani nini anaendelea kukupa pumzi? Hapa nitaonekana muhuni tena lakini Mh Rais wema wako ni katika haki na sio sifa.

 Mwisho, Mh Rais, Mamlaka yana tabia ya kudanganya akili nikuombe Rais wangu usikubali mamlaka ikudanganye hata kidogo, futa kauli yako, watakaokuona mjinga wao ndio wajinga. Najua Polisi na Jeshi wanakutii wewe lakini Dhambi na hila iko mbali na MUNGU.

 Godbless Lema (Mb)

By Yericko Nyerere

Vita vya YOM-KIPPUR na funzo kwa dunia

By

  Yericko Nyerere

 

Tupokwenye miaka 40 toka vita vya YOM-KIPPUR kuanza vita hii ilianza tarehe 06-10-1973 nchi za kiarabu zilijipanga vilivyo ili tu kurejesha ardhi zao walizopoteza katika vita vilivyovunja record ya Dunia vita vilivyopiganwa kati ya nchi za Ki-arabu na Israel kwa mda wa siku sita Mwaka 1967 na majeshi ya nchi za Ki-arabu kusalimu Amri na kuacha ardhi zao kutekwa na askari wao kwa mamia kupoteza maisha yao na Maelfu kutekwa.

 Vita hii iliacha maumivu na makovu makubwa sana katika ulimwengu wa Kiarabu hata kupelekea nchi hizo hasa Misri na syria kuanza mikakati ya kukomboa ardhi zao zilizotekwa na Mjeshi ya Israel,kwa maana syria milima ya Ki-mbinu ya Golan ilikuwa imetekwa na kwa upande wa Misri ilipoteza Jangwa lote la sinai ikiwa pamoja na Mfereji wa Suez nchi hizi zilikuwa na machungu sana hasa ikichukuliwa kuwa nchi iliyowashinda ni ndogo sana hivyo mipango iliyofanywa mwaka 1973 ni kuzikomboa ardhi zilizotekwa baadaye kuifutilia mbali Israel katika uso wa Dunia.

 Mipango ya kuivamia Israel ilipangwa ifanyike siku ya Jumamosi ambapo kulikuwa na sikukuu ya Kiyahudi inayojulikana kama YOM-KIPPUR,Siku hiyo Israel ilipata changamoto kubwa ambayo katika historia ya nchi hiyo Kivita haijawahi kutokea, maana siku hiyo Maelfu ya vifaru na Makumi elfu ya Majeshi na ndege za kijeshi zilifanya shambulizi la kushitukiza na kwa pamoja katika mipaka ya Israel ya kusini na kaskazini hii ilikuwa Ishara tosha kuwa Syria na Misri zilikuwa zinataka kurudisha ardhi zao zilizotekwa katika vita vya siku sita vya mwaka 1967.

 CHANZO CHA VITA YA YOM-KIPPUR.  Baada ya Israel kushinda vita vya 1967 Israel ilipata ardhi kubwa ambayo ilipaswa kulindwa kwa gharama yoyote ili kupata Muafaka wa kisiasa kati ya nchi hiyo na nchi za Kiarabu kwa upande wa Misri Israel ilichukua Sinai na Suez canal hivyo Jeshi la Israel lilipata changamoto kubwa sana kulinda mpaka wote wa sinai na Mfereji wa Suez,Majeshi ya Israel yaliweka vituo vya ulinzi vilivyojulikana kama BAR-LEV line,na kwa upande wa Syria Israel ilichukua Milima ya Golan ambayo kwa Israel lilikuwa eneo jipya lililotakiwa kulindwa kwa nguvu zote maana Ki-Jeshi lilikuwa ni strategic la kimbinu sana Maana milima hiyo ya Golan iko kwenye mwinuko kwa hiyo eneo hilo likishikiliwa na Syria ina maana Majeshi ya Syria yana Uwezo wa kumiliki Kijeshi ndani ya Israel kilomita zaidi ya 25 na wakati huohuo Israel haingekuwa na uwezo wa kupata target Shabaha nzuri kupiga majeshi ya Syria yaliyoko kwenye milima hiyo ya Golan na ndiyo maana mpaka leo Israel haiwezi kuiachia milima hiyo maana kufanya hivyo ni sawa na kujitoa MHANGA kwa jeshi la Israel,Badala yake Inataka kuirudisha milima hiyo kwa kubadilisha na AMANI na Syria ili wawekeane mkataba wa AMANI na kutoshambuliana na Israel ili iweze kupata uhakika wa kutoshambuliwa toka milima hiyo ya Golan.

 Baada ya vita vya 1967 Msri na Syria zilianza kujenga majeshi yao ili waweze kukomboa ardhi zao zilizotekwa, Nchi hizo zilihitaji zana za kivita zaa kisasa ili kuweza kummaliza adui yao Israel walihitaji sana kupata silaha toka Urusi wakati huo USSR Walihitaji kupata Ndege aina ya MIG na vifaru aina ya T-62 Vilevile makombora ya kuangushia ndege aina ya SA-2,3,6 na SA-7 pamoja na silaha za kubomolea Vifaru aina ya SAGGER ANT-TANK GUIDED MISSILES.

 Kufikia mwezi October 1972 Rais wa misri wakati huo Anwar Sadat aliwahi kuongea na makamanda wake kuhusu kuishambulia israel na ilipofikia mwezi may 1973 vyombo vya kijasusi vya Israel vilikuwa vimepata habari kuwa Misri itaishambulia Israel kupitia mfereji wa Suez Misri walikuwa wanajua kuwa kama Misri itaishambulia Israel basi Syria nayo ingejiunga na kuishambulia Israel kutokea Kaskazini. Vilevile Israel walidaganyika kuwa Misri itaishambulia Israel mara tu itakapopokea ndege aina ya MIG-23 na SCUD-D toka Urusi Jeshi la Israel lilijua kuwa Misri haijapokea silaha hizo toka Urusi hivyo iliamini Misri haiwezi kuanzisha vita hivyo kabla ya kupokea silaha hizo toka Urusi.

 Mwezi May na Mwezi August 1973 Majeshi ya Misri yalifanya mazoezi makubwa ya kijeshi katika eneo la mpaka na Israel,Israel nayo ilipoona hivyo ilianza kukusanya askari wake kwa maandalizi ya vita lakini baada ya pale hakukuwa na harakati zingine za kijeshi katika eneo hilo la mpaka hivyo Jeshi la Israel liliona kuwa hiyo ilikuwa kawaida tu yaani waliona kama yalikuwa mazoezi ya kawaida tu.

 Septemba 25,1973 Mfalme hussein wakati huo alikutana na waziri mkuu wa Israel wakati huo Mama Gold Meir wakati huo Mfalme Hussein alishakutana na Rais Sadat na Assad wa Syria na alimwonya waziri mkuu wa Israel kuhusiana na kukalia eneo la Syria la milima ya Golan na Sinai eneo la Misri,Baada ya kumalizika kikao hicho na Mfalme Hssein waziri mkuu wa Israel pamoja na waziri wa ulinzi wa Israel wakati huo MOSHE DAYAN pamoja na vyombo vya Kijasusi vya Israel waligundua moja kwa moja kuwa Misri ingewashambulia wakati wowote.

 Masaa machache tu kabla ya Misri kuishambulia Israel tarehe 06-10-1973 waziri mkuu Golda Meir na waziri wa Ulinzi Moshe Dayan na Mkuu wa utawala jeshini Gen.David Elazar kwa pamoja waliamua kuwaita wanajeshi wa anga wale wa akiba na wale wa vifaru wale wa akiba maana walijua hapo sasa vita haiepukiki.

 Kabla ya vita siku hiyo majeshi ya pande zote mbili yalikuwa na zana zilizokuwa zinakisiwa kuwa hivi:

 ISRAEL               

 Ndege za kivita 358 

 Vifaru 2100

   Meli za kivita 37

MAADUI ZAKE

Ndege za kivita 998

Vifaru 4350

Meli za kivita 137

 

 

 Ilipofika saa nane kamili mchana majeshi ya Msri na yale ya Syria yalianza kumimina makombora kuelekea katika sehemu zilizokuwa zinakaliwa na Israel,Misri na Syria zilichagua siku ya jumanosi maana ilikuwa ni sikukuu ya kiyahudi ya YOM KIPPUR waliona siku hiyo wayahudi wote huwa wanasherehekea hivyo ilikuwa upenyo mzuri sana kwao.

 Kwa upande wa Sinai majeshi ya Msri yaliweza kuvuka mfereji wa Suez kupitia sehem tano tofauti na kwa upande wa mizinga Misri iliweza kukipiga kituo cha wanaanga wa Israel waliokuwa Refidim katika jangwa la sinai na vikosi vingine vya mizinga vya Israel vilishasmbuliwa na mizinga ya Misri,na kufikia saa 11 jioni maelfu ya Wanajeshi wa misri walikuwa wamefika upande na kulikamata eneo lote la mashariki mwa mfereji wa Suez na wakati wa usiku vikosi vya vifaru vilivuka mfereji wa Suez hapo ndipo hali ya uwanja wa vita ilibadirika kabisa kwa Israel uwepo wa askari wa miguu wa Israel na mizinga yao hakukuweza kuyasimamisha majeshi ya Misri. Division ya 252 na Brigedi ya 14 ya kikosi cha vifaru viliadhirika vibaya sana asilimia kubwa ya vifaru vyao vilikuwa vimeangamizwa na silaha aina ya SAGGER ANT-TANK GUIDED MISSILES toka Misri.

 Jeshi la anga la Israel lilipoitwa ili kudhibiti majeshi ya Misri,Ndege hizo zilijikuta zinaangushwa na mizinga ya kuangushia ndege, Misri iliweza kuzitungua ndege za Israel kiasi cha kuzimalizia uwezo wa kushambulia na baada ya kujipanga vizuri na kujua namna ya kukwepa makombora ya kuangushia ndege aina ya SA-7 ndege za Israel ziliweza kuziangamiza helcopter zilizokuwa zimebeba Makamandoo wa misri na kuweza kuzitungua ndege 7 aina ya MIG kwenye uwanja wa mapambano. mapambano hayo yalifanyika kusini mwa mfereji wa Suez ndege hizo ziliangushwa na ndege za Israel aina ya PHANTOM.

 Kwa upande wa milima ya Golani majeshi ya Syria yaliweza kusonga mbele huku mizinga na vifaru pamoja na askari wa miguu waliweza kumiminia mizinga,risasi majeshi ya Israel kwa saa nzima mfululizo wakati huo Israel ilikuwa na Brigedi mbili za vifaru Division ya 36th ndiyo ilikuwa mstari wa mbele na Brigedi 188th nayo ilikuwa na jukumu la kulinda sehemu ya kusini ya mlima wa Golani na Brigedi ya 7th ilikuwa na jukumu la kulinda sehemu ya kaskazin mwa mlima Golan hivyo vifaru vya Israel havikuweza kuvishambulia vikosi vya Syria sababu havikuwa kwenye RANGE ya kuweza kushambuliwa.

 Mapigano ya vifaru yalianza tu siku hiyo baada ya jua kuzama majeshi ya Syria yaliweza kupenya ngome za Majeshi ya Israel kwa kuwa walikuwa wanatumia NIGHT-VISION viona usiku hivyo vilisaidia sana majeshi ya vifaru vya Syria vifaru vya Israel vilivyokuwa upande wa kaskazini havikuweza kufua dafu mbele ya vikosi vya Syria,vifaru vya Syria viliweza kushika sehemu ya kusini mwa mlima Golan na ilipofika asubuhi ya tarehe 07-10-1973 vifaru zaidi ya 600 vilikuwa vimeingia ndani ya ardhi ya Israel na vilikimbilia kwenda kulishika Daraja mhimu la nto Jordan na kambi ya kijeshi ya Nafar,Israel pia ilipoteza mlima wa HELMON ambao ulikuwa wa kimbinu strategic nao uliangukia mikononi mwa majeshi ya Syria hili lilikuwa pigo kubwa kwa majeshi ya Israel.

 Kwa upande wa majini majeshi ya Israel yaliweza kuziangamiza boat zilizokuwa zinabeba makombora za Syria na miji yote iliyokuwa inazunguka milima ya Golan wakazi wake waliondolewa na majeshi ya Israel.na baada ya siku 18 Majeshi ya Israel yaliweza kujijenga upya na kuchukua tena eneo lote la milima ya Golan na mlima Hermon

By Yericko Nyerere

CHADEMA imeng’ara kwenye Uchaguzi na Itashinda 2015

By

 Yericko Nyerere

Inawezekana kauli yangu isiwaingie watu masikioni mwao kabisa, lakini nitawaeleza japo kwa kifupi.

 Katika siasa kuna kitu kinaitwa siasa za jumla (general politics) na siasa za kijiografia (geography politics)

 General politics inahusu mambo yanayohusu siasa za kitaifa bila kuchagua chama au itikadi na hizi mara nyingi husimamiwa kwa katiba, kanuni na sheria za nchi, hapa inahusiana pia na daftari la wapiga kura na tume ya uchaguzi,

 Geography politics inahusu siasa za eneo husuka, kuna international gp, na domestic gp,

 Katika hayo Chadema ime win kwenye Gp-D kwa asilimia zaidi ya 90%, hili linatokana na chama kushiriki uchaguzi kwa miaka yote huku mambo muhimu yanayopaswa kufanywa kwenye General Politics yakiwa doro kabisa, mambo hayo ni kama tume kuwa huru, daftari la wapigakura kuboreshwa, na dola kuvuruga chagizi nyingi kwa maslahi ya ccm.

 Takwimu za chaguzi hizi zinatoa sura stahiki ya ubora wa domestic political ya Chadema,

 Mathalani uchaguzi huu Chadema ilikuwa ikitetea kata 3, za Nyaisura, Kiborloni na Mikol.. Kigoma.

 Tumepoteza Nyaisura, na Kigoma, na Tumeipoka ccm kata za Sombetini na Njombe.

 Thamani ya kata ilizoshinda chadema nikubwa kuliko ccm, kubeba kata ya njombe ni turufu kubwa, vivyo hivyo kata ya sombetini Arusha ambapo sasa rasmi ccm inakuwa chama cha upinzani Arusha, CCM hawajaongeza thamani yoyote ya kata,

 Kwa lugha nyingine nikuwa CHADEMA 0-0 CCM, lakini CHADEMA wananafasi ya golden goal kwakubeba kata ya Njombe ambayo kwanza inafuta propaganda za ccm yakuwa chadema ni chama cha ukanda, sasa tunashuhudia Chadema sio chama cha ukanda tena bali chama cha kitaifa na kila pembe ya jamhuri hii kipo.

 Izingatiwe kuwa oparesheni M4C Pamoja Daima haikuwa maalumu kwaajili ya uchaguzi huu bali sehemu ya ratiba ya chama katika kutoa elimu ya umma kudai/kuhimiza uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

 Kuna wanaoamini kuwa Chadema kuwaadhibu wanachama wake waliovunja katiba ya Chama akina Zitto, Killa, Mwigamba eti ni “Mgogoro” uliochangia kwa 100% kutopata kata nyingi zaidi katika uchaguzi huu.

 Nikubaliane nao wale wafikirio hivyo lakini tupeane shule ya falsa ya siasa kidemorasia kwa ufupi ambayo ndio hutawala siasa za uwanda wa chama kinachojiandaa kushika dola.

 Niseme kuwa Chama cha siasa kilichokomaa na chenye wanachama wenye nguvu ya kitaifa kinapoamua kumuwajibisha mwanachama yeyote mwenye nguvu ya kitaifa aliyevunja katiba,itikadi,itifaki na falsafa ya chama hicho, kovu lake huwa halizibwi kwa miezi mitatu au sita tu, kisayansi itachukua hata mwaka kuirejesha nguvu ya chama katika mizani stahiki ya kisiasa.

 Hivyo Mwanachadema yeyote na mwanamageuzi ni lazima atambue kuwa uchaguzi wa Udiwani huu kwa kata 27 nchini, sio kipimo stahiki cha kufuta pengo la akina Zitto. Labda kwa mchambuzi wa siasa asiejua sayansi ya siasa tu na mwenye agenda ya kipropaganda ndie ataamini kufukuzwa akina Zitto ni chanzo cha kupata kushindwa kupata kura nyingi zaidi katika uchaguzi huu.

 Athari za kufukuzwa kwa Zitto na wenzie ndani ya chama zitapimwa baada ya miezi sita hadi mwaka mmoja kutoka sasa hii ikiwa na maana uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao ndivyo vitakuwa vipimo vyake, kwa sasa yanayotokea yalitarajiwa kwa 100% na yalipita kwenye chekecho la kimkakati la chama na kisha yakaamuliwa iwe hivyo.

 Kosa kubwa kwa Chadema ni kosa la kimkakati na hili ni lazima lifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo,

 Kwanza ieleweke kuwa daftari la wapiga kura ndio rungu lililoibeba ccm, ni lazima liboreshwe ikiwa ni pamoja na uingizaji wawapiga kura wapya ambao utafiti unaonyesha ni kundi kubwa la vijana wenye umri kati ya miaka 18-26 ambao hawakuwa na sifa ya kupiga kura 2010. Lakini hata hawa waliojiandikisha yaani wenye kupiga kura sasa, idadi kubwa ya wapiga kura hao hawakupiga kura kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuuza shahada zao.

 Pili Tume ya Uchaguzi, hii ni lazima juhudi za msksudi zitumike kuitoa mikononi mwa chama tawala, ni hatari kuiacha iendelee kuwa wakala wa ccm badala yakuwa tume huru.

 Tatu Vyombo vya dola, hapa ndipo panahitaji mkakati mkuu wa kisiasa, jeshi la polisi ni lazima tukabiliane nalo na ieleweke vema kuwa ccm haitakoma kulitumia jeshi la polisi ama vyombo vya dola kwa ujumla mpaka siku inakata roho kabisa, hivyo njia mbadala ni muhimu sana tunapoelekea kushika dola hili la Tanzania mnamo octobar 25, 2015.

 Kwanza uundwe mkakati wa uhusiano mwema na vyombo vyote vya dola nchini, hili linaweza kuwa gumu kidogo na linaweza kuifanya serikali ianze kupata mafua ya msimu na kujikuta tunaingia kwenye mgogoro unaoweza kutumiwa na wakware wa akili wa ccm kama akina Mwigulu na kufikiria uhaini, jambo la muhimu ni kuziangalia sheria za nchi hasa zinazoratibu vyama vya siasa na mienendo yake,

 Mathalani kiongozi wa kisiasa kuzuru makao makuu ya Polisi Tanzania na kusikiliza changamoto zinazowakabilli, hili halina zuio kisheria, ilimradi haendi kugawa kadi za chama hapo,

 Ni lazima tuitazeme upya sheria inayosema mtumishi wa umma asijihusihe na siasa, hii ni nzuru lakini iboreshwe ili iwe na tafsiri ya maslahi kwa nchi na hatimae taifa kuzaa siasa za kisasa na za kimaendeleo.

 Wanamikakati warejee chini wawafanyie utafiti wa kisayansi viongozi wa majimbo, mikoa na kanda, nilazima tuwapime kwa nyuzi 360 kiutendaji kwakuwa hizi chaguzi ndogo za kata na serikali za mitaa zinatakiwa wao wasimamie na kuonyesha uwezo wao na sio hivyo tu bali lipo ndani ya uwezo wao kikatiba, Chama lazima sasa kijikite kwa nguvu zote kwenye msingi (chadema ni msingi).

 Ni lazima tufanye utafiti wa kimkakati usio na unafiki wala haya,

 Tukiyatekeleza haya yote, uchaguzi wa serikali za mitaa utaanza kutupa majibu ya mkakati huu na uchaguzi mkuu ujao tutashinda!

 Yote kwa yote Chadema haijapoteza uchaguzi huu bali imeng’ara, kimkakati ni ccm ndio imepoteza.

By Yericko Nyerere

Rwandan fugitives relocate to Tanzania

 

By Times Reporter  February 10, 2014      

 

Renegade army Captains, Charles Sande and Christopher Busigo, who are wanted by the Government of Rwanda on charges of subversion, fled to Tanzania from Uganda where they are coordinating their activities contrary to media reports that they were kidnapped, The New Times has learnt.

 A Ugandan newspaper, The Daily Monitor, reported on Saturday, February 8, that the two dissidents had disappeared.

  “We are aware of their plans. They are faking kidnap to evade  justice,” an official who preferred anonymity was quoted saying.

 “We understand that RNC is shifting camp from Uganda to Tanzania, and that the Kayumba Nyamwasa group is using some Ugandan journalists for propaganda purposes,” the source added.

 This newspaper has also learnt that Busigo now uses a Tanzanian line; +255712526565 to communicate with his superiors and other people.  Efforts to talk to Busigo were futile as by press time he had declined to answer our repeated calls.

 Police spokesperson, ACP Damas Gatare, also dismissed the kidnap claims, adding that the police will ensure that all the criminal suspects hiding in and outside the country are arrested and brought to book.  Gatare said there have been several cases where criminal suspects faked their kidnap in order to qualify for asylum in other countries.

 They include that of terror suspect, Lt. Joel Mutabazi, who is said to have staged his own shooting in Uganda and blamed the Rwandan government.

 Others include the vice-president of a faction of PS-Imberakuri, Alexis Bakunzibake, who recently led it into an alliance with the FDLR, a terror group whose members are largely responsible for the 1994 Genocide against the Tutsi. He too faked his kidnap in 2012, only to resurface some months later.

 And this month, former communications secretary of the Democratic Green Party of Rwanda, Omar Leo Oustazi, also returned to the country after a year in exile and dismissed reports that he had been kidnapped.

He went on to accuse his former boss, Frank Habineza, of being behind an alleged plot to have him killed and blame it on the government.

By Yericko Nyerere

Walikubali Mchakato wa Katiba Mpya wakubali na Matokeo yake.

By Mwanakijiji

 

Hawazi watu kuamka sasa na kulalamika kuwa ati Bunge la Katiba litakuwa limejaza CCM na kuwa Katiba Mpya itakuwa ni ya CCM! Haiwezekeni watu wapate ufunuo leo hii baada ya kutangazwa kwa majina ya wabunge wa  Bunge la Katiba ati sasa wametambua kuwa Kikwete anawachezea akili ati kwa vile wameona majina ya makada na wana CCM maarufu kama kina Kingunge Ngombare Mwiru, Shamim Khan, Paul Kimiti, Sixtus Mapunda, na Dr. Zainab Gama nikiwataja wachache tu.

Kuna watu wanataka tuamini kuwa makundi yaliyogawanywa katika matangazo ya majina hayo watajadiliana kimakundi kwenye Bunge la Katiba; kwamba wakulima watakaa kama wakulima na kujadiliana, wavuvi kama wavuvi, wanasiasa kama wanasiasa n.k. Ukweli ni kuwa sheria ya Katiba Mpya haijaweka utaratibu wa mijadala ya Makundi au kulazimisha kupiga kura kwa makundi. Hivyo watu wasifikirie kuwa ati kwenye Bunge la Katiba makundi yataulizwa na kupiga kura ili kutoa msimamo wao kama kundi. Sheria inatoa uhuru wa maoni na mijadala kwenye Bunge la Katiba na hivyo wabunge hawa hawafungwi na utii au umoja wa makundi yao!

Lakini jambo ambalo liko wazi – na nililionesha miaka miwili iliyopita – ni kuwa Bunge litajaa watu wenye maslahi na CCM hasa kwa vile ‘magenius’ wetu walikubali kuwa wabunge wote na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa kutangazwa kwa majina haya watu wenye maslahi na CCM au ambao wamewahi kushika nafasi za uongozi ndani ya CCM wanaunda kundi kubwa zaidi (super majority) kwenye Bunge hili. Hili si jambo la bahati mbaya; siyo jambo ambalo linakuja tu hivi hivi na ukiangalia kwa karibu utaona kuwa ni jambo ambalo litahakikisha kuwa kile ambacho CCM wanataka wanakipata.

Sasa wapo waliokubali mchakato huu mbovu wa kuandika Katiba Mpya; walikubali kwa sababu waliamini – kwa makosa – kuwa utakuwa ni wa haki, wa wazi na ambao utawapa nguvu wananchi. Badala yake walikubali kumpa Rais wa JMT na Rais wa Zanzibar nguvu kubwa sana. Hivi kulikuwa na ubaya gani kwa taasisi kutaja wajumbe wake wa Katiba (wachaguliwe kwenye taasisi hizo kwa uhuru) badala ya kuachiwa Rais kuamua? Matokeo yake wapo baadhi ya wabunge hawa ambao wanamshukuru Rais leo hii kwa “kuwakumbuka” kwani wengine nyota zao za kisiasa zilishafifia!

Tulisema huu ni mchakato mbaya; na kama watu wanafikiri wameshaona ubaya wake wangoje mijadala ya Bunge hili itakavyoanza. Binafsi nitawakatalia wapinzani wakianza kulalamika kuwa wanaburuzwa au kuwa hawana imani na mchakato au na Rais! Hilo litakuwa ni kigeugeu kilichopitiliza! Yote ambayo yatatokea wapinzani wanajua na walishajulishwa na wakakaza shingo zao kuukumbatia mchakato huu haramu (ni haramu kwa sababu umevunja Katiba ya sasa).

Nitaendelea kuukataa na japo ninatamani sana kuona Tanzania inakuwa na Katiba Mpya nzuri na inayotokana na wananchi naamini kuwa mchakato huu hadi hivi sasa umewanyima Watanzania haki hiyo. Walioukumbatia toka mwanzo, wakatoa maoni na kutoa wajumbe na kukubali kuwa ni halali wasigeuke sasa; wametikisa dawa, sasa wainywe; wasiseme “chungu

By Yericko Nyerere

Kwanini Hayati Baba wa Taifa alitumia kura yake ya veto kumkataa Lowasa?

By Yericko Nyerere

 

“Kwanini Hayati Baba wa Taifa alitumia kura yake ya veto kumkataa Lowasa kwa sababu iliyoitwa na inayoaminika mpaka sasa kuwa “Lowassa ni MWIZI anautajiri mkubwa usio na ufafanuzi alioupata kwa mda mfupi tu akiwa mkurugenzi wa AICC?”

 Ikumbukwe nikuwa hoja hiyo ya Mwalimu Nyerere ilikuja baada ya Lowassa na wapambe wake kukodi ndege binafsi kutoka Arusha kwenda Dodoma kuhudhuria vikao vya uteuzi wa urais mwaka 1995, kitendo hiki kilimfedhehesha sana Mwalimu na wazalendo wengine na hata kufikia kuliondoa jina la fisadi huyu nguli wa Tanzania,

 Je leo utajiri wa Lowassa umekuwa halali?

 Mamlaka ya mapato Tanzania inaweza kututhibitishia uhalali wa kodi alipayo mtu huyu?

 Tangu afukuzwe uwaziri mkuu mwaka 2007 taarifa za kuaminika kutoka vyanzo muhimu nikuwa Lowasa alitenga 12bilioni kwaajili ya kujitakasa, ambapo mpaka leo hii ameshatumia 8bilioni, je pesa hii ameipata wapi? Imelipiwa kodi kiasi gani? Atairudishaje akiwa rais?

 Ili kuhuisha mjadala huu hebu niwaeleze jambo mhimu dhidi ya mtu huyu aitwae Edward Ngoyai Lowasa,

 Labda niwaelekeze watafiti watafute faili la EL la enzi za TANU pale Lumumba. Mzee Paul Sozigwa suala hili analifahamu fika.

 Ndiyo, Mwl. Nyerere alichukizwa na tabia ya Lowasa ya kujitajirisha kwa kuiba mali ya umma. Lowasa, licha ya tuhuma za wizi enzi akiwa AICC, kujimilikiaha majumba ya Masajili wa Majumba wakati akiwa waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, Mwl. Nyerere alikuwa akifahamu wizi wa Lowasa tangu enzi za TANU. Kati ya mwaka 1974 na 1977 Lowasa aliiba pesa za TANU alizopewa kusamia ujenzi wa ofisi ya TANU Arusha. Badala ya kujenga ofisi ya TANU Lowasa alinunua kiwanja na kujenga nyumba yake binafsi. Jambo hilo lilipogundulika mwaka 1982, lilimkasirisha sana Mwl hivyo kuamuru afukuzwe kwenye chama. Ni marehemu Edward Moringe Sokoine ndiye alimwombea msamaha kwa Mwl. Nyerere abadilishiwe adhabu. Edward Lowasa alipewa adhabu mbadala; kuhudhuria kazini Ofisi Ndogo ya Chama Mtaa wa Lumumba kila siku bila kukosa, kuwa kazini masaa 8 bila kutoka lakini bila kupangiwa kazi yoyote hadi Chama kingeona ametubu na hatimaye apangiwe kazi nuingine. Lowasa alitumikia adhabu yake hadi Sokoine alipofariki.

 Hiyo ndio sababu kuu ya Mwl. Nyerere kumkatalia Lowasa kugombea urais.

 Kikwete, Mkuchika, Twaa Khalifan, Kinana, Bagenda na Msekwa wanajua ukweli wotekuhusiana na jambo hili. Ila maadamu kwa sasa hakuna tena maadili ya uongozi wa kisiasa nchini Tanzania, Lowasa anaweza kuachiwa awatawale wezi, wala rushwa na mediocre wa nchi hii.

 

“Kuna watu wasipokuelewa maneno na matendo yako, mshukuru Jah, wewe bado unafikra chanya, wakianza kukuelewa jichunguze ni wapi umeanguka maana umeanza kuwaza kama wao”

By Yericko Nyerere