Tatizo si posho, Tatizo ni wakwepa kodi wakubwa na taifa kutonufaika na rasilimali zetu

Nimeona maneno ya wamaharakati wengi ya kupingana na posho za wabunge mufilisi, mimi natambua wanamtazamo na mawazo yanayoweza kutofautiana na mimi au na watu wengine kwani huo ndio uhuru wa kufikiri.

Tanzania si taifa la kupambana vita kwenye posho za wafanyakazi wake, bali ni taifa linalotakiwa kufanya mapambano katika kudhibiti wakwepa kodi kwenye sekta ya madini, mawasiliano na wengine kama wahindi wanaotumia maduka ya jeshi kukwepa kodi kubwa sana.

kuwa mfanyakazi wa tanzania si kwamba ulipwe mafao dhaifu, na wafanyakazi wengine kama walimu wakipunjwa mishahara basi ni lazima watu wote wapunjwe mishahara na posho.

nadhani ningewaelewa wanaharakati kama wangepigania kwanza wafanyakazi wengine kama walimu wapate posho na mishahara mikubwa na kuimiza ukusanyaji wa kodi na taifa kunufaika na rasilimali zetu.

By Yericko Nyerere

Leave a comment