Wazee Kumi na Saba (17) Waliodai Uhuru waTanganyika

 Kwa kujua au kutokujua, kwa makusudi au kwa bahati mbaya kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana kuhusu hasa ni akina nani waliodai Uhuru wa Taifa letu Tanganyika.

Upotoshaji hauishii hapo tu bali hata dhana halisi ya Maadhimisho yenyewe,Leo wanasema nisherehe za Uhuru wa Tanzania Bara,

Hakuna nchi au taifa duniani linaloitwa  Tanzania Bara, halijapata kutokea na halitotokea katika uso wa dunia hii taifa au nchi iitwayo Tanzania Bara.

Muunganano wa Tanganyika na Zanziber ni mfano wa kuigwa duniani, hakuna muungano wenye hadhi kinadharia dunia kama huu,Kila aliye muamini wa amani duniani na aupiganie kuulinda na kuuhuisha uwe na mafaa kwa wa Tanzania

Lakini muungano unaomeza taifa lingine na kubaka fikra za Watanganyika huku ukipuliza kwa dhihaka Wazanzibar haufai, yatupasa tuuhuishe mapema kabla mbongo za wahafidhina hazijamka na kushuhudia hasira ya Mtanganyika chini ya uvuli wa fikra za ccm mfilisi.

Sihubiri KUUVUNJA muungano huu murua bali, nahubiri uwepo wa Tanganyika na Zanzibar zenye kuwajibika kwa watu wao na uwepo Tanzania yenye kujikita Kimuungano.

Suala hili ni kama halina mantiki ya mageuzi ya mstakabali wa Mtanganyika, lakini aliye Mtanganyika anatambua mafaa ya matokeo ya hili.

Zanzibar ni nchi, yenye mamlaka kamili ya ndani, ina KATIBA, ina rais, ina jeshi, ina mahakama, ina bunge, ina makamu wa rais na zaidi ina makamu wa pili wa rais.

Je Tanganyika ipo wapi????? ilikufa ili iweje???

Vita baridi ilishaisha tunaitaka nchi yetu ikiwa na mipaka ileile.

CCM wamekuwa na kapropaganda kakidikteta kwa mtu yeyote azungumzia Muungano, huitwa mchochezi na zaidi MUHAINI.  Ni faida gani ccm mnzopata kwenye aina ya muungano huu?

Mimi nashauri mfumo wa serikali TATU ndiyo suluhu ya manung’uniko ya wakaazi wa pande zote za muungano huu.


Mh. Rais Kikwete leo kaweka kila kitu hadharani kumbe ni wazee 17 kutoka pande zote za nchi yetu walishiriki kikamilifu kudai uhuru wetu kinyume na historia inavyopindishwa au kuaminishwa kwamba ni watu wa Kariakoo pekee walifanya hivyo.


Julius Kambarage Nyerere, Ali Sykes, Lameck Makaranga, Gosbert Milinga, Gelmandus Pacha, Joseph Kimalando, Japhet Kirilo, Abubakar Ilanga, Saadan Kandoro, Suleiman Kitwara, Kisunguta Kabara, Chewa Said Chewa, Dosa Aziz, Patrick Kunambi, Joseph Kasela Mbantu, John Rupia, Abdulah Sykes.

 

By Yericko Nyerere

Leave a comment