Rais Kikwete ateua mabalozi wapya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Mabalozi:-
*<
(i) Mhe. Phillip MARMO, ameteuliwa kuwa Balozi nchini CHINA. Kabla ya hapo Mhe. Marmo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.
(ii)************ Dkt. Deodorus B. KAMALA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini BELGIUM. Kabla ya hapo Mhe. Kamala alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
*
(iii)********** Dkt. Batilda S. BURIAN, ameteuliwa kuwa Balozi nchini KENYA. Kabla ya hapo Mhe. Dkt. Burian alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).
*
(iv)********** Dkt. Ladislaus C. KOMBA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini UGANDA. Kabla ya hapo Dkt. Komba alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.
*
(v)************ Bibi Shamim NYANDUGA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MSUMBIJI. Kabla ya hapo Bibi Nyanduga alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
*<
(vi)********** Bibi Grace J.E. MUJUMA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini ZAMBIA. Kabla ya hapo Bibi Mujuma alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda (Regional Co-operation), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
*
(vii)******* Bwana Mohamed H. HAMZA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MISRI. Kabla ya hapo Bwana Hamza alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, ZANZIBAR, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
*
(viii)***** Ndugu Ali A. SALEH, ameteuliwa kuwa Balozi nchini OMAN. Kabla ya hapo Bwana Saleh alikuwa Balozi Mdogo (Consul General) nchini Dubai.
*
2.******** Uteuzi huu unaanzia tarehe 12 Oktoba, 2011.* Wataapishwa tarehe***** 19 Desemba, 2011 saa 03.00 Asubuhi.
*

By Yericko Nyerere

Leave a comment