Angalizo: Tokeo hili lilichapishwa kwenye gazeti la Mwafrika 1962. Mwafrika, Jumatatu Oktoba 29, 1962
MZUNGU mwingine ambae ni Meneja wa kampuni ya kuuza dawa, Arusha Bw. R. Bawley ameamriwa aihame Tanganyika, Mzungu huyo amepewa saa 48 tu kufanya hivyo.
Ripoti iliyopokelewa jana na gazeti hili ni kwamba Bwana Bawley alionekana akiondoka na matokaa kuelekea Kenya.
Sababu za kufukuzwa Mzungu huyo ni ufedhuli na kuwadharau Waafrika.
Mwandishi wetu akizungumza na na Regional Commissiner wa Jimbo la Kaskazini, Bwana P. Walwa jana alijulishwa kwamba jambo hilo alilihakikisha yeye mwenyewe alipofukuzwa na Meneja huyo.
Bwana Walwa alipata malalamiko kutoka kwa watu wengi kuhusu ufedhuli wa meneja huyo. Watu wengine walisema kwamba huwafukuza watu dukani kwake au kuwatupia fedha wakinunua vitu.
Bwana Walwa alikwenda katika duka hilo ili ahakikishe mwenyewe kabla ya kuchukua hatua na kwenda kufika Bawley akamwambia ‘nenda zako’. Hapo Bwana Walwa alitoka na kutoa habari hizi kwa polisi.
Radhi yakataliwa:
Asubuhi yake Meneja huyo alikwenda kuomba radhi akisema hakujua kuwa yule aliyemfukuza alikuwa Regional Commssioner.
Bwana Walwa alikataa kumsamehe kwa sababu, alisema ‘dharau ile ilifanyiwa Waafrika wote’. Bwana Walwa alimwambia mwandishi wetu hiyo jana kwamba yeye alitembelea jimbo lote akiwaonya watu waheshimiane. Aliona si haki wengine waachiwe kufanya dharau.
Bawley sasa ni Mzungu wa sita kuondolewa kwa visa kama hivyo tangu nchi hii ipate uhuru wake.
NIONAVYO:
Ukikisimuliwa nchi hii ilivyokua zamani na ilivyo sasa, ni masikitiko makubwa, nisawa na jua na mwezi.
Leo mzungungu anaua mwafrika kwa bastola huku serikali dharimu impa nyongeza ya muda wa uwekezaji chini ya upinde wa miaka mitano ya msamaha wa kodi!
Swali je hivi leo, ambapo viongozi wetu wanawakumbatia wawekezaji, kuna yeyote kati yao anayeweza kufikia maamuzi kama haya?