Iran na Tanzania zasaini mkataba wa ushirikiano wa kiutamaduni

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Tanzania zimetia saini mkataba wa ushirikiano katika sekta za utamaduni na sanaa baina ya nchi mbili.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, mkataba huo umetiwa saini Tehran kati ya Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran Dk. Seyyed Mohammad Husseini na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Emmanuel John Nchimbi. Akizungumza katika kikao hicho Dk. Husseini amesema Iran iko tayari kushirikiana na Tanzania katika sekta ya utengenezaji filamu. Ameongeza kuwa Waislamu wa Tanzania wameiomba Iran iwatengenezee vipindi vya radio na televisheni kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Ameongeza kuwa Waislamu wa Tanzania wameiomba Iran iwasaidie kuimarisha televisheni za Kiislamu nchini humo. Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran pia ameitaka Tanzania kuandaa ‘Wiki ya Utamaduni ya Tanzania nchini Iran’ ambapo athari za sanaa za Tanzania zitaonyeshwa. Kwa upande wake Dk. Nchimbi ameafiki kuandaliwa ‘Wiki ya Utamaduni ya Tanzania nchini Iran’. Aidha amesema Tanzania inahitajia msaada wa Iran katika sekta ya sinema.

By Yericko Nyerere

Leave a comment