Majina 100 ya wa Israel wahalifu wa vita ya siku 22 dhi ya Palestina yatangazwa

 

 

Orodha ya kwanza ya maafisa wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliotekeleza jinai za kivita katika vita vya siku 22 dhidi ya Wapalestina huko Ghaza imetangazwa.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Qudsna, orodha hiyo inajumuisha majina ya maafisa wa kijeshi na askari wa utawala wa Kizayuni ambao majina yao yalichapishwa katika tovuti ya ‘war criminals’ au watenda jinai za kivita mwaka 2009. Tovuti hiyo lihujumiwa punde baada ya kuchapisha majina hayo.

Kati ya waliotajwa katika orodha hiyo ya watenda jinai ni Gabi Ashkenazi mkuu wa zamani wa vikosi vyote vya kivita vya Israel. Wazayuni hao walihusika katika jinai za kinyama wakati wa vita vya siku 22 dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Vita hivyo vilianza mwishoni mwa mwaka 2008 ambapo Wapalestina wapatao 1500 wakiwemo wanawake na watoto zaidi ya 500 waliuawa shahidi.
Waliowengi duniani wanataka Wazayuni hao watenda jinai wafikishwe katika vyombo vya sheria vya kimataifa lakini Marekani inatumia ushawishi wake vibaya kuzuia hatua zozote kali kuchukuliwa dhidi ya watenda jinai hao wa kivita.

By Yericko Nyerere

Leave a comment