Rais wa Iran aanza ziara yake Amerika ya kaskazini

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad ameanza ziara yake ya siku 5 hii leo ya Amerika ya kusini katika mataifa ambayo yanamuunga mkono katika msimamo wake dhidi ya Marekani ambayo inaoongoza juhudi za kuiwekea Vikwazo. Ziara hiyo itamfikisha Venezuela, Nicaragua, Cuba na Ecuador.Nchi hizo zote zinapinga ukandamizaji wa Marekani pamoja na mitazamo ya kikoloni. Rais Ahmadinejad amesema Amerika ya kusini ni  eneo ambalo halikubali tena kuchezewa na Marekani.

Katika nchi zote atakazotembelea ikiwemo Cuba Rais huyo wa Iran anapanga kutia saini mikataba. Maswala ya eneo hilo na yale ya kimataifa yatazungumziwa ikiwemo swala la Marekani kuingilia mipango ya nchi nyingine na kuwepo kwa majeshi yake duniani.

Marekani inaongoza kampeni ya kuibana Iran kiuchumi ili kuiadhibu kutokana na mpango wake wa Kinuklia. Marekani inashuku kwamba Iran inatengeneza Bomu la Nuklia madai ambayo yanapingwa nchini Iran.

By Yericko Nyerere

Leave a comment