TAARIFA KWA UMMA WA WATANZANIA .
YAH; MADAKTARI WALIOKUWA MAFUNZONI/WASAIDIZI WA MADAKTARI BINGWA KUONDOLEWA KAZINI HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI WAREJESHWE KAZINI.
Juzi tarehe 07/01/2012 tumeshuhudia tukio la ajabu ambalo limefanywa na mtu anayeitwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuwasimamisha kazi madaktari wasaidizi 229 ambao wamekuwa wakifanya kazi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na serikali ikashindwa kuwalipa na hata yeye na hospitali anayoiongoza walishindwa kuweka utaratibu wa kuwalipa kama ilivyofanyika katika hospitali za Mbeya, Dodoma na kwingineko nchini.
Uamuzi huu wa kiuonevu umefanywa na viongozi ambao wameshindwa kutii masharti na makubaliano ya mkataba baina ya madaktari hao na wizara ya afya ambao ulikuwa umesainiwa baina ya pande mbili hizo kuwa wanastahili kulipwa kila tarehe 22 ya mwezi , kitu ambacho serikali imeshindwa kutekeleza hadi madaktari walipogoma kuanzia tarehe 03/01/2012.
Kutokana na tukio hili ambalo linasababisha maisha ya watanzania kupotea , kutokana na uzembe wa serikali kushindwa kuwalipa madaktari ambao wamefanya nao makubaliano ya kimkataba ni muendelezo wa uzembe ule ule ambao tumekuwa tukiulalamikia kila mara.
Wizara hii imekuwa na utamaduni wa kutokutatua misingi na vyanzo au mizizi ya matatizo na badala yake imekuwa na utamaduni wa kushughulikia matokeo ya matatizo husika kama ilivyofanya kwenye chuo cha ustawi wa jamii Dar Es Salaam kwa kuwafukuza wahadhiri badala ya kuangalia kiini cha tatizo ambacho nilikianisha bungeni wakati wa hotuba mbadala ya kambi ya upinzani, kufukuza wanafunzi waliolalamikia masuala mbalimbali kuhusiana na bodi ya mikopokatika Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili n.k.
Kutokana na hali hii ambayo inawafanya watanzania kuendelea kuumia na wengine kupoteza maisha yao ni kitendo ambacho kamwe hakikubaliki na hakivumiliki tena kuona kuwa serikali inawatesa watanzania kutokana na kushindwa kuwalipa madaktari ambao wangefanya kazi ya kuwahudumia wananchi hawa ambao wamekuwa wakilipa kodi na fedha hizo kutumiwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijinufaisha wao binafsi na ambao ni viongozi serikalini.
Hivyo basi , ninaitaka serikali ifanye mambo yafuatayo;

- Kuwarejesha kazini mara moja na bila masharti madaktari ambao wamesimamishwa kiuonevu kwa kuwa kosa sio la kwao bali ni la serikali.
- Serikali iwalipe madaktari wote wanaodai posho zao ili waweze kuendelea na kazi ya kuwahudumia wananchi maeneo yote nchini ambako hawajalipwa.
- Serikali iwe inatibu viini vya matatizo na sio kukimbilia kushughulikia matokeo ya matatizo hayo kama ambavyo salamu za mwaka mpya za Katibu Mkuu wa CHADEMA ziliainisha waziwazi.
- Serikali iseme wazi kama imeshindwa kukusanya mapato na hivyo kufilisika ili wananchi wajue na waweze kuchukua tahadhari ama hatua madhubuti kwa kadri watakavyoona inafaa.
Mwisho ninawapa pole sana watanzania wote ambao wamekumbwa na adha hii iliyosababishwa na uzembe wa Serikali na kwa wale waliopoteza ndugu zao kutokana na mgomo huu uliosababishwa na serikali nawapa pole sana na Mungui awatie nguvu kipindi hiki kigumu.
Tamko hili limetolewa na .
…………………………
Gervas Mbassa (Mb).
Waziri kivuli wa wizara ya Afya na ustawi wa Jamii.
08/01/2012.