Double agent wa CIA Ia ELJ aIiyetikisa vichwa vya majasusi USA

By Wikileaks01 Spy

 

Click image for larger version.  Name: ali2.jpg  Views: 0  Size: 43.3 KB  ID: 129168 Click image for larger version.  Name: 628×471.jpg  Views: 0  Size: 34.6 KB  ID: 129169

 Ni Ali Mohamed alikuwa double agent wa CIA na EIJ( Egyptian islamic jihad) ambayo ndio ilipelekea kuundwa kwa ALQAEDA huku yeye akiwa mwendesha mafunzo wa mbinu za kivita na kijasusi wa kwanza kwenye kambi zao kwa ajili ya kuwaandaa na mapambano dhidi ya utawala wa kisovieti nchini Afghanistan miaka ya 90. yeye ndiye mwalimu wa kwanza wa Osama bin Laden na Ayman Zawahiry( kiongozi wa sasa wa Alqaeda)

 Ali anaelezwa kuwa mtu mwenye uzito wa kilo 90, urefu futi 6 huku akielezwa mtu aliye fiti kimwili, aliyebobea kwenye sanaa za mapigano( martial art),mwenye ufahasa mzuri wa lugha za kiingereza,kifaransa,kiyunani na kiarabu. alikuwa mwenye nidhamu ya juu, mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri, mwenye kujichanganya na watu na uwezo wa kupata marafiki kwa urahisi.

 Uhusiano wake na CIA  kwa mara ya kwanza aliingia marekani kama mkalimani wa Ayman Zawahiry( kiongozi wa sasa wa alqaeda) wakati alipoenda kuchangisha michango kusaidia wana mgambo katika harakati za kuutoa utawala wa wasovieti Aghanistan.kwa maelezo inasemekana Zawahiri akamshauri a-infiltrate marekani, mwaka 1984. Ali anaelezwa aliweza kuingia kwenya kitio cha CIA Egypt kwa urahisi na kuweza kuongea na mkuu wa kituo kuhusu ofa yake ya kufanya nao kazi na akawa recruited kama junior intelligence officer. kazi ya kwanza alipewa ni kupenya ndani ya msikiti mmoja mjini hamburg ujerumani ulisemekana kuwa na mahusiano na wanamgambo wa Hizbollah wa nchini Lebanon lakini cha ajabu akawataarifu viongozi kuwa yeye ni jasusi wa CIA ametumwa kuchukua taarifa, kwa kuwa katika ule mkusanyiko alikuwepo jasusi mwingine wa CIA, taarifa juu ya alichokifanya Ali Mohamed zikawafikia mabosi CIA. Kwa mujibu wa mwandishi maarfu wa jarida la New Yorkers na mshirika wa kituo cha sheria na usalama New York University of Law ni kwamba ulitumwa ujumbe wa limawasiliano kutoka CIA ukitaarifu kuwa sio mwaminifu na ameshadhibitiwa, lakini mda huo taarifa inatumwa tayari Ali mohamed alikuwa mjini Carlifonia kushiriki program maalum ya kuwapatia ruhusa ya kuingia marekani bila kuwa na visa kwa ‘Valuable assets’ waliolifanyia taifa la Marekani utumishi wa hali ya juu, program ambayo yenyewe pia ilikuwa ikifadhiliwa na CIA. Ali akafanikiwa kuoa mmarekani Linda Sanchez na akachukuliwa kwenye special forces na akapangwa katika kambi kubwa ya Fort bragg kama drill commander( sijui kwa kiswahili wanaitwaje, yani wale ambao wanawapokea makuruta na kuwafundisha maisha ya jeshini, taratibu na nidhamu)

 mnamo mwaka 1988 Ali aliwataarifu wakuu wake jeshini kuwa anachukua likizo fupi kwa ijili ya kwenda afghanistan kupambana na wasovieti( huko ndio akawa anatoa mafunzo kwa wanamgambo waanzilishi wa Alqaaeda). Huku nyuma afisa mwandamizi wa Ali, Lt. Col Robert Anderson aliandika ripoti ya kina ikilenga kutaka idara ya ujasusi ya jeshi kumchunguza Ali Mohamed na kumfungulia mashtaka lakini taarifa yake hiyo ilipuuzwa. anaeleza kuwa ” Kuwa na mwanajeshi mmisri, aliyehusika na mauji ya rais wa zamani wa misri Saadat, alafu akapata visa ya kuja kuishi marekani na akachukuliwa kwenye vikosi maalum vya jeshi(special forces) inashangaza, haya mambo hayatokei tu hivi hivi” anaendelea kueleza kuwa ilikuwa ni vigumu kuamini kuwa mwanajeshi wa kawaida wa Marekani kupigana vita katika jeshi la nje bila kuadhibiwa. akaendelea kusema anaamini atakuwa anafadhiliwa na shirika la kijasusi la kimarekani.

 

 Ali mohamed aliendelea kutoa mafunzo kwa wana mgambo wa kiislamu wa Maktab al-Khidamat (iliyoanzishwa na Abdullah Azzam ambayo baadae alijiunga Osama, wakagombana hatimae Osama akaigeuza kuwa ALQAEDA baada ya ku-win popularity over Azzam)nchini marekani kupitia Kambi ya Al Kifah iliyokuwepo mjini brooklyn iliyokuwa akisapotiwa na Marekani kwa ajili ya kuwawaezesha kuutoa utawala wa kisovieti nchini Afghanistan

 miaka ya 90 akarudi tena Afganistani ambako alitoa mafunzo ya kijasusi ikiwemo, kuteka watu, kuteka ndege, jinsi ya kuua n.k na inasemekana katika wanafunzi wake wa kwanza kabisa ni Osama bin laden, Ayman Zawahiry(kiongaozi wa sasa wa Alqaeda) na viongozi wengine wa Alqaeda kwa mijibu wa FBI special agent Jack Cloonan

 mwaka 1993 akiwa ndani ya Alqaeda akawa informant wa FBI, na mmoja wa wapigaji wa ALQAEDA Mohamed Atyf aliyepewa jukumu la kufanya survey katika ubalozi wa marekani nchini kenya(uliolipuliwa mwaka 1998) alikataa kumtajia Ali Mohamed passport namba yake kwa kuwa alikuwa na mashaka kuwa Ali alikuwa ni mshirika wa Marekani

 wiki mbili baada ya balozi za marekani nchini Kenya na Tanzania kulipuliwa, FBI walisachi makao ya Ali na kukuta nyaraka mbalimbali zenye ushahidi juu ya kuhusika kwa na milipuko nchini Kenya na Tanzania na kukamatwa. Ali alikubali makosa ya kigaidi na akaeleza mwanza mwisho kuhusu ushiriki wake katika kundi la Al qaeda, akakiri makosa ili apate kifungo cha maisha jela bila msamaha wowote ule

 mwaka 2001 gazeti la Raleigh News and Observer lilitaarifu kuwa Ali anatoa ushirikiano kwa serikali ya marekani, naeleza kamanda mstaafu wa Delta force katika kitabu chake cha The Mission,The Men and Me:Lessons from former Delta Force Commander Pete Blaber ”Mawakili wa utetezi wanaamini kuwa Ali hajahukumiwa na anasirikiana na serikali japo serikali haijathibitisha hilo,akihukumiwa anaweza akahukumia kidogo, kama miaka 25 kwa mujibu wa makubaliano yao”

 mwaka 2006, mke wa Ali Linda Sanchez alisema kuwa mumwe bado hajahukumiwa na haruhusiwi kuzungumza na yeyote “yani wamemshikilia kiusiri sana ni kama vile amepotelea kwenye hewa”

By Yericko Nyerere

Ukweli wa Mabomu ya Soweto Arusha wajulikana Shahidi asema Mwigulu Nchemba na CCM waliratibu uhalifu huo.

By:

Mkuu ya Kaya

 

Time: 10:28

 

 28/12/2013

Natumai Sikuku ya X-mas ilienda vizuri na leo hii tupo pamoja katika kusukuma gurudumu hilii zito la maendeleo ya Taifa letu wakati tunahesabu siku chache zipite tuuzike mwaka 2013 na Mungu akipenda tuuanze mwaka 2014.

Kwa member wa jamiiForums siku mbili zilizopita Mh. Mwigulu Nchemba alileta post yake ya utetezi humu ndani na mimi niliichachinga kwa kueleza maumivu yaliyo ndani ya moyo wangu. Na baadhi ya wana Jf walinishauri nianzishe Thread japo halikuwa wazo langu mwanzo.

 Mnamo mwezi wa sita mwaka 2013 kulikuwa na uchaguzi mdogo wa madiwani katika baadhi ya mikoa ya Tanzania, Arusha ilikuwa mojawapo ya mikoa hiyo huku ikiwa na kata zipatazo 4 zikirudiwa uchaguzi. Nakumbuka vyama vinne vilijitokeza katika kusimamisha wagombea ila chama cha CCM na CHADEMA ndivyo vilikuwa vikishindana. Kipindi hicho nilikuwa mwanachama wa Cmm na nikimfanyia kampeni kwa karibu mgombea udiwani kwa tiketi ya ccm wa Kata ya Elerai Ndg. Emanuel Laizer.

 Wakati kampeni zinaendelea na tunakaribia kufikia mwisho tulipata ujumbe kuwa kuna Mjumbe toka makao makuu ya chama atakuja akiambatana na mawaziri ili kuongeza nguvu na atakapofika tutatakiwa tufanye kikao cha siri ambapo katika kikao hicho tutapewa mbinu na mipango mbalimbali ya kukabiliana na Chadema. Na wajumbe watakao ruhusiwa kuuudhuria kikao hicho ni wale viongozi wa mitaa na watu wanao aminika na chama tu.

 Tarehe13/06/2013 siku ya alhamisi saa moja jioni tulikutana katika eneo la chuo kimoja cha ufundi (Help to Selph Help Project )kilichopo Sakina kuelekea Olmatejo, kulikuwa na ulinzi mkali ndani na nje ya chuo hicho na magari yapatao sita hivi aina ya Toyota vx na V8 yakiwa yamepaki chuoni hapo, huku taa za chuo hicho zikiwa zimezimwa zoto isipokuwa taa za chumba cha mikutano tu. Tulipewa tangazo kuwa tunatakiwa tuzime simu zetu na tuzikabizi kwa bwana mmoja ambae alikuwa mlangoni (nafikiri waliogopa kurekodiwa au kupigwa picha) kabla ya kuingia ukumbini.

 Tulipo kuwa ukumbini aliingia Mwigulu Nchemba na kuanza kutupa moyo na maelekezo ya mbinu mbalimbali za kikampeni, na muda uliposogea majira ya saa 10:00 usiku ndio akaanza kutoa kauli zilizotuacha na maswali mengi kichwani., namnukuu “Kesho tarehe 14 tutafunga kampeni zetu zote na tuna sababu ya kufanya hivyo, kwa sababu tunazo taarifa kuwa Chadema watafunga kampeni zao tarehe 15 siku moja kabla ya uchaguzi ndio maana tumeamua kufanya hivyo. Pili kila mmoja anatakiwa aimize jamiii yake na rafiki zake kwamba siku ya tarehe 15 wasisubutu kwenda kwenye mkutano wa Chadema na yeyote aliopo hapa asisubutu kwenda na atakae enda kitakacho mkuta tusilaumiane” mwisho wa kunukuu.

 Kiukweli sina ushaidi wa picha wala rekodi yoyote inayoonyesha mwigulu akiyasema hayo ila nina wajumbe wanne waliokubali kutoa ushaidi pindi kesi itakapoenda mahakamani.

 Kwa kuwa Raisi amemfuta kazi aliyekuwa Waziri wa mambo ya Ndani Mh. Nchimbi, ambae alikuwa mtu wa kaaribu sana na Mwigulu Nchemba ndio sababu hasa iliyonifanya kupigana vita hii na wale waliosababisha na namna yoyote kifo cha mwanangu.

 NB:  Mh. Raisi nakuomba uunde tume huru ya kijaji ili mimi muhathirika mkuu na wajumbe waliokuwa katika kikao hicho cha Mwigulu Nchemba tuweze kutoa ushaidi utakaoweza kuisaidia tume hiyo kufanya kazi yake kwa uraisi. Nakuomba sasa Mh. Raisi usikie kilio chetu.

By Yericko Nyerere

Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili iliyowavua nyadhifa Mawazi Kagasheki, Nchimbi, Mathayo, Nahodha

TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA KUHUSU TATHMINI YA MATATIZO YALIYOTOKANA NA OPARESHENI TOKOMEZA ;

 1.0 UTANGULIZI  Mheshimiwa Spika, wakati Bunge likijadili hoja ya kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili jambo muhimu la dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 47 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2013, iliyowasilishwa na Mhe. Said Nkumba, Mbunge wa Sikonge kuhusu Mgogoro kati ya Wafugaji na Wakulima, Hifadhi na Uwekezaji, Mheshimiwa Spika alitoa Uamuzi ‘Speakers Ruling’ kuwa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ishughulikie kazi ya kutathmini na kuangalia jinsi Mpango wa Kupambana na Majangili ulivyopangwa na kutekelezwa na Serikali kupitia ‘Operesheni Tokomeza’.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za Taarifa Rasmi za Bunge za tarehe 1 Novemba 2013, wakati Bunge likihitimisha Hoja ya Kuairisha Shughuli za Bunge, Mhe. Spika alitoa uamuzi ufuatao:-

…Kamati ile ya kawaida ya Maliasili itaendelea na kazi yake ya kufanya tathmini ya kuangalia jinsi mpango ule wa Kupambana na Majangili ulivyopangwa na ndani yake itashughulikia kama kulikuwa na uzembe ama kuna watu wanahusika katika kuondoa maisha ya watu kwa sababu za uzembe …

1.1 Kuundwa kwa Kamati Ndogo ya Uchunguzi  Mheshimiwa Spika, kufuatia uamuzi ulioutoa tarehe 01 Novemba, 2013 Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, ilikutana Dodoma tarehe 9 Novemba, 2013 kwa lengo la kujadili utaratibu wa kutekeleza jukumu hilo.  Katika kikao hicho Kamati iliazimia kuunda Kamati Ndogo kwa mujibu wa Kanuni ya 117(18), ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Tole la 2013 ili iweze kushughulikia suala hilo kikamilifu.

 1.2 Hadidu za Rejea, Wajumbe wa Kamati na muda wa kazi  Mheshimiwa Spika, Kamati Ndogo ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyoundwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kwa agizo lako la tarehe 01 Novemba, 2013, ilipewa Hadidu za Rejea Nne (4) zifuatazo:-

 1) Kutathmini na kuangalia jinsi Mipango ya Kupambana na Majangili ilivyopangwa;

 2) Kuangalia kasoro zilizojitokeza katika kutekeleza mpango huo;

 3) Kutathmini iwapo kulikuwa na uzembe katika kutekeleza Operesheni Tokomeza ambao ulisababisha watu wasio na hatia kupoteza maisha na mali zao; na

 4) Kuchunguza migogoro ya Ardhi inayohusu Wakulima, Wafugaji na Wawekezaji kwenye maeneo yanayozunguka hifadhi.  Mheshimiwa Spika, Kamati hii ya uchunguzi iliundwa na Wajumbe Tisa (9) kama ifuatavyo:-

 i. Mhe. James Daudi Lembeli, Mb.  ii. Mhe. Abdulkarim Esmail Shah, Mb.  iii. Mhe. Susan Limbweni Kiwanga, Mb.  iv. Mhe. Kaika Sanin’go Telele, Mb.  v. Mhe. Dk. Henry Daffa Shekifu, Mb.  vi. Mhe. Amina Andrew Clement, Mb.  vii. Mhe. Haji Khatibu Kai, Mb.  viii. Mhe. Muhammad Amour Chomboh, Mb.  ix. Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa

 Mheshimiwa Spika, Sekretarieti iliyohudumia Kamati Ndogo ya Uchunguzi iliundwa na Wajumbe wafuatao:-  i. Ndg. Theonest K. Ruhilabake  ii. Ndg. Gerald S. Magili  iii. Ndg. Chacha T. Nyakega  iv. Ndg. Stanslaus W.Kagisa

 Mheshimiwa Spika, Kamati Ndogo ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ilitakiwa kutekeleza majukumu yake na kuwasilisha ripoti katika Mkutano wa Kumi na Nne (14) wa Bunge. Hivyo basi, baada ya uteuzi huo, Wajumbe wa Kamati Ndogo walipanga kuanza kazi tarehe 25 Novemba, 2013 na kuikamilisha ifikapo tarehe 15 Desemba, 2013.

 1.3 Njia zilizotumika katika kukamilisha kazi  Mheshimiwa Spika, Kamati Ndogo ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ilitekeleza majukumu yake kwa kuongozwa na Hadidu za Rejea ilizopewa kwa kufanya rejea na kuzingatia yafuatayo:-

 a) Kusoma na kuchambua nyaraka zilizoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuandaa na kutekeleza Operesheni Tokomeza nchini. Nyaraka hizo ni hizi zifuatazo:-  i. Mpango Kazi wa Operesheni Tokomeza (Concept Paper)  ii. Tathmini ya Utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.  iii. Sheria ya Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge (Na.3) 1988  iv. Sheria ya Wanyamapori (Na. 5) 2009  v. Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la mwaka 2013

 b) Kufanya mahojiano na watu mbalimbali:-  i. Waziri wa Maliasili na Utalii  ii. Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii  iii. Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori  iv. Mkurugenzi Msaidizi Kikosi wa Dhidi ya Ujangili  v. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  vi. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)  vii. Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)  viii. Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Hifadhi za Misitu (TFS)  ix. Mahojiano na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge

 c) Kuzuru maeneo yaliyoanishwa katika Taarifa ya Wizara kuhusiana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na yale yenye migogoro kati ya Wakulima au Wafugaji na Wawekezaji katika maeneo ya hifadhi kwa lengo la kuhakiki (verify) masuala yaliyoainishwa kupitia uchambuzi uliofanywa na Kamati.

 2.0 KUPOKEA NA KUCHAMBUA NYARAKA MBALIMBALI ZILIZOHUSU OPERESHENI TOKOMEZA

 Mheshimiwa Spika, Hadidu Rejea ya kwanza iliitaka Kamati Ndogo ya Ardhi, Malisili na Mazingira, kufanya tathmini na kuangalia jinsi mipango ya kupambana na majangili ilivyopangwa. Ili kukamilisha jukumu hilo, Kamati ilifanya yafuatayo:-

 a) Kupitia na kuchambaua Mpango Kazi wa Operesheni Tokomeza (Concept Paper) ulioandaliwa na Wizara  b) Kupitia na kuchambua Tathmini ya Utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.

 2.1 Uchambuzi kuhusu Mpango Kazi wa Operesheni Tokomeza  Mheshimiwa Spika, katika kuchambua Mpango Kazi wa Operesheni Tokomeza kwa lengo la kupata uelewa zaidi wa namna operesheni hiyo ilivyopangwa na kutekelezwa, Kamati ilibaini kuwa, mpango huo uliandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na ulikuwa na mambo yafuatayo:-

 i. Ukubwa wa tatizo la ujangili  ii. Aina za ujangili na sababu za ukuaji wake  iii. Maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ujangili  iv. Malengo ya Operesheni Tokomeza  v. Njia zilizotumika kutekeleza operesheni  vi. Maeneo ya operesheni na gharama za utekelezaji  vii. Tamko la Serikali kusitisha Operesheni Tokomeza

 2.1.1 Ukubwa wa tatizo la ujangili  Mheshimiwa Spika, Kamati ilibaini kuwa, tatizo la ujangili ni kubwa na limekuwa likisababisha idadi ya Tembo iendelee kupungua nchini. Takwimu zinaonesha kuwa, idadi ya Tembo imepungua kutoka 350,000 (miaka ya 1970) hadi kufikia 55,000 (mwaka 1989). Juhudi za kukabiliana na hali hiyo kupitia Operesheni zilizowahi kutekelezwa huko nyuma zilisaidia kuongeza idadi ya  Tembo hadi 141,000 (mwaka 2006) ingawa ilishuka tena hadi kufikia 110,000 (mwaka 2009).

 2.1.2 Aina za ujangili na sababu za ukuaji wake  Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa ya Serikali, vitendo vya ujangili vinavyofanyika nchini vimegawanyika katika makundi mawili yafuatayo:-

 i. Ujangili wa Kujikimu (subsistance poaching)  Aina hii ya ujangili inahusisha watu wenye kipato kidogo na hulenga zaidi katika kujipatia kitoweo na fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji mengine. Ujangili wa aina hii huathiri zaidi wanyama wanaoliwa na si Tembo.

 ii. Ujangili wa Biashara (commercial poaching)  Aina hii ya ujangili inahusisha zaidi watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha na hulenga kupata nyara zenye thamani kubwa. Wanyama wanaoathiriwa zaidi na aina hii ya ujangili ni pamoja na Tembo, Faru, Simba na Chui.

 Mheshimiwa Spika, taarifa ilibainisha kuwa, kuongezeka kwa masoko haramu katika nchi za Asia na Mashariki ya Kati ambayo yanatoa bei kubwa ya nyara hizo, imekuwa ni chachu ya kuimarika kwa mitandao inayojihusisha na ujangili (ndani na nje ya nchi) na hivyo kusababisha ongezeko kubwa la vitendo vya ujangili.

 2.1.3 Maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ujangili  Mheshimiwa Spika,Mpango Kazi waKupambana na Ujangili ulilenga kujikita katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ujangili wa wanyamapori na misitu. Mpango huo ulioelezewa kuwa niwa muda mrefu na kusimamiwa na kikosi kazi cha Taifa (national task force),umeanisha maeneo yafuatayo kuwa ndiyo yaliyoathirika zaidi:-

 i. Pori la Akiba Selous  ii. Hifadhi ya Taifa Serengeti, Pori la Akiba Maswa na Pori Tengefu la Loliondo.  iii. Hifadhi ya Taifa Katavi na Mapori ya Akiba Rukwa na Lukwati.  iv. Hifadhi ya Taifa Mikumi  v. Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi za Taifa Tarangire na Ziwa Manyara.  vi. Mapori ya Akiba Burigi, Biharamuro, Ibanda na Rumanyika.  vii. Mapori ya Akiba Moyowosi, Kimisi, Ugalla na Hifadhi ya Misitu Luganzo.

 2.1.4 Malengo ya Operesheni Tokomeza  Mheshimiwa Spika, Operesheni Tokomeza ambayo ilizinduliwa rasmi tarehe 04 Oktoba, 2013 ilikuwa na malengo yafuatayo:-

 i. Kuzuia vitendo vya ujangili ndani na nje ya Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu, Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro na Misitu ya Hifadhi na kufanya operesheni maeneo yote yaliyoathiriwa na ujangili.

 ii. Kuwatambua mapema majangili na kujua nyendo zao ndani na nje ya maeneo ya hifadhi.

 iii. Kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wafanyabiashara haramu wa nyara za Serikali na mazao ya misitu.

 iv. Kuvunja mitandao ya wafadhili, wanunuzi wadogo na wakubwa pamoja na mawakala wa biashara haramu ya nyara za Serikali na mazao ya misitu.

 v. Kufuatilia na kukamata mali za majangili zilizotokana na biashara haramu ya nyara za Serikali na mazao ya misitu.

 2.1.5 Njia zilizotumika kutekeleza Operesheni Tokomeza  Mheshimiwa Spika, Kamati ilibaini kuwa, Mpango Kazi wa Serikali kuhusiana na Operesheni Tokomeza, uliainisha kuwa operesheni hiyo itaendeshwa kwa kutekeleza mambo yafuatayo:-

 i. Kufanya uchambuzi wa kina wa watuhumiwa wa mtandao wa ujangili wa nyara za Serikali na wavunaji na wasafirishaji haramu wa mazao ya misitu.

 ii. Kuwakamata watuhumiwa wote waliobainishwa kwenye taarifa za kiintelijensia.

 iii. Kupiga picha na kuchora ramani ya eneo la tukio kwa kila mtuhumiwa (sketch map).

 iv. Kuhoji na kuandika maelezo ya watuhumiwa wa ujangili wa nyara za Serikali na wavunaji na wasafirishaji haramu wa mazao ya misitu.

 v. Kukusanya na kuhifadhi vielelezo vyote vitakavyokamatwa kutoka kwa majangili kwa ajili ya kujenga ushahidi mahakamani.

 vi. Kuandika maelezo ya mashahidi na askari wakamataji kwa ajili ya kujenga ushahidi mahakamani.

 vii. Kuandaa mashitaka dhidi ya watuhumiwa na kuwapeleka mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

 2.1.6 Maeneo ya Operesheni na gharama za utekelezaji  Mheshimiwa Spika,Mpango Kazi wa Operesheni Tokomeza ulianisha kuwepo awamu mbili za utekelezaji ambazoni; Mpango Kazi wa Muda Mfupi na Mpango Kazi wa Muda Mrefu.

 Katika Mpango Kazi wa Muda mfupi itafanyika operesheni maalum katika maeneo yote ya ndani na nje ya hifadhi za wanyamapori na misitu nchi nzima. Maeneo hayo yaligawanywa katika kanda 12 za utekelezaji kama ifuatavyo:-

 i. Selous, Mikumi, Udzungwa, Lukwika/ Lumesule na Liparamba,  ii. Burigi/Biharamuro, Ibanda/Rumanyika na Rubondo,  iii. Moyowosi, Ugalla na Lugazo,  iv. Serengeti, Loliondo, Maswa, Ikorongo na Kijeshi,  v. Kilimanjaro, Arusha, Mkomazi/Umba, Simanjiro na Longido,  vi. Tarangile, Manyara, Karatu/Ngorongoro, Swagaswaga na Mkungunero,  vii. Rungwa, Ruaha, Mpanda – Kipengele,  viii. Rukwa, Lukwati, Katavi, Lwafi, Piti na Wembere,  ix. Mahale na Gombe,  x. Saadani na kwenye maeneo yenye misitu ya mikoko,  xi. Pori Tengefu la Handeni, Kilindi na Mkinga na  xii. Msitu wa Kazimzumbwi, Kisarawe, Rufiji na Mkuranga,

 Mheshimiwa Spika, ilianishwa kuwa, awamu ya kwanza ya Mpango Kazi wa muda mfupi ingegharimu jumla ya Tshs. 3,968,168,667/= ambazo zingechangwa na Taasisi za wanyamapori (WD, TANAPA, NCAA na TFS) kwa kila moja jumla ya Tshs. 992,042,167/=

 2.1.7 Tamko la Serikali kusitisha Operesheni  Mheshimiwa Spika, kufuatia michango na malalamiko ya Waheshimiwa Wabunge wakati wakichangia hoja iliyotolewa na Mhe. Said Nkumba Mbunge wa Sikonge, pamoja na maagizo ya Bunge kutaka Serikaliitoe maelezo kuhusu hoja zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge, Serikali ilitoa Tamko la kusitisha Operesheni Tokomeza tarehe 01 Novemba, 2013.

 2.2 Uchambuzi wa Taarifa ya awali ya Utekelezaji wa Operesheni Tokomeza  Mheshimiwa Spika, taarifa hii ya awali kuhusiana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza ilikuwa na mambo yafuatayo:-  i. Washiriki wa operesheni  ii. Awamu za operesheni  iii. Mafanikio ya operesheni  iv. Idadi ya watuhumiwa na kesi zilizofunguliwa  v. Changamoto za operesheni

 2.2.1 Washiriki wa Operesheni  Mheshimiwa Spika, Operesheni Tokomeza ilihusisha jumla ya washiriki 2,371 kutoka vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa mgawanyo ufuatao:-

 i. Wanajeshi (885) kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania,  ii. Askari (480) kutoka Jeshi la Polisi,  iii. Askari (440) kutoka Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU)  iv. Askari Wanyamapori (383) kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)  v. Askari (99) kutoka Wakala wa Huduma za Misitu (TFS)  vi. Askari Wanyamapori (51) kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)  vii. Waendesha Mashitaka (23) na  viii. Mahakimu (100)

 2.2.2 Awamu za Operesheni  Mheshimiwa Spika, Operesheni Tokomeza ilipangwa kutekelezwa katika awamu Nne (4) kama ifuatavyo:-  i. Awamu ya kwanza ambayo ililenga kusaka Silaha za Kivita na Meno ya Tembo kutoka miongoni mwa wanaojihusisha na vitendo vya ujangili.  ii. Awamu ya pili ambayo ililenga kusaka silaha zisizomilikiwa kihalali na zile zinazomilikiwa kihalali lakini zinasadikiwa kutumika kwenye vitendo vya ujangili.  iii. Awamu ya tatu, ambayo ililenga kutafuta yalipo Maghala ya Nyara, kusaka Wafadhili na Wanunuzi wa nyara hizo na kuwabaini watu wanaowakingia kifua wahusika wa vitendo vya ujangili.  iv. Awamu ya nne, ambayo ililenga kukamata Nyara nyingine mbali na Meno ya Tembo na kuhakikisha watu walio katika makundi yafuatayo wanakamatwa:-  – Wawindaji haramu,  – Wavunaji haramu wa mazao ya misitu,  – Watu wanaolisha Mifugo ndani ya hifadhi, na  – Watu waliojenga ndani ya maeneo ya hifadhi

 2.2.3 Mafanikio ya Operesheni Tokomeza

 a) Idadi ya watuhumiwa na kesi zilizofunguliwa  Mheshimiwa Spika, tangu kuanza kutekelezwa kwaOperesheni Tokomeza (tarehe 04 Oktoba, 2013 hadi ilipositishwa (tarehe 01 Novemba, 2013) jumla ya kesi 687 zilifunguliwa zikiwahusisha watuhumiwa 1,030 katika maeneo yote kama ifuatavyo:-  i. Kanda ya Kwanza kesi 105 zikiwahusisha watuhumiwa 105  ii. Kanda ya Pili kesi 370 ambazo zilihusisha watuhumiwa 375  iii. Kanda ya Tatu kesi 165 zilizohusisha watuhumiwa 498  iv. Kanda ya Nne kesi 47 zilizohusisha watuhumiwa 52

 Mheshimiwa Spika, hadi wakati Operesheni Tokomeza inasitishwa tarehe 01 Novemba, 2013 kati ya Kesi 687 zilizokuwa zimefunguliwa ni 132 tu ndiyo zilikuwa zimetolewa maamuzi na 555 bado zilikuwa katika hatua ya kusikilizwa. (Tazama Kiambatisho Na. 1)

 i. Kukamatwa kwa meno ya Tembo 211 yenye uzito wa kilo 522, meno ya Ngiri 11, Mikia ya wanyama mbalimbali 36, Ngozi za wanyama mbalimbali 21, Pembe za Swala 46, Mitego ya wanyama 134, ng’ombe 7,621 Baiskeli 58, Pikipiki 8 na Magari 9.

 ii. Kupungua kwa kasi ya mauaji ya Tembo kutoka wastani wa Tembo wawili (2) kwa siku hadi tembo wawili tu katika kipindi chote cha operesheni (siku 29).

 iii. Hadi kufikia tarehe 11 Novemba, 2013 jumla ya Bunduki za Kijeshi 18 zilikamatwa, Bunduki za kiraia 1579, Risasi 1964, Mbao vipande 27,913, Mkaa Magunia 1242, Magogo 858 na Misumeno 60. Vyote hivyo vilikamatwa katika Kanda ya Nne.

 2.2.4 Changamoto za Operesheni Tokomeza

 a) Vifo vilivyotokea wakati wa Operesheni  Mheshimiwa Spika,Taarifa ya Serikaliiliainisha vifo kamachangamoto kubwa iliyojitokeza wakati wautekelezaji wa Operesheni Tokomeza kutokana na watumishi 6 na watuhumiwa 13 kupoteza maisha. (Tazama Kiambatisho Na. 2)

 b) Hujuma dhidi ya Operesheni  Mheshimiwa Spika, taarifa ya Serikali ilifafanua kuwa,utekelezaji wa Operesheni Tokomeza ulikumbwa na vitendo vya hujuma kutoka kwa baadhi ya makundi ya jamii kama ifuatavyo:-  i. Mamluki miongoni wa washiriki wa Operesheni. Mfano; kukamatwa kwa Askari Polisi na Askari Wanyamapori wakisindikiza gari lenye Meno ya Tembo, na gari la Serikalikutumika kusafirisha Meno ya Tembo.  ii. Vyombo vya Habari kutumika kuvuruga operesheni kwakueneza propaganda zilizolenga kushawishi wananchi kupinga operesheni hiyo.  iii. Baadhi ya wamiliki wa silaha kutuhumiwa kutoa silaha zao ili zitumike kwa ajili ya vitendo vya ujangili.

 C) Tuhuma dhidi ya Operesheni  Mheshimiwa Spika, taarifa ya Serikai ilifafanua kuwa,ingawa lengo la operesheni lilikuwa ni kupambana na vitendo vya ujangili dhidi ya raslimali za Taifa, utekelezaji wake ulikumbwa na tuhuma kadhaa zikiwemo zifuatazo:-  i. Mateso dhidi ya watuhumiwa yaliyosababisha maumivu, kupata ulemavu wa kudumu na hata wengine kupoteza maisha (Mfano; Marehemu Emiliana Gasper Maro wa Gallapo – Babati).  ii. Matumizi mabaya ya Silaha (Mfano; Mzee wa miaka 70 kuuawa kwa kupigwa risasi 3).  iii. Nyumba za wananchi kuchomwa moto (Mfano; Kijiji cha Kabage Wilaya ya Mpanda – Katavi).  iv. Mifugo kuuawa kikatili kwa kuchomwa moto na kupigwa risasi (Mfano; Ng’ombe 60 kuuawa kwakupigwa risasi).  v. Kukosekana kwa mwongozo wa utoaji wa taarifa jambo lililosababisha viongozi husika wa Serikali kutopewa taarifa muhimu za utekelezaji wa Operesheni. (Mfano; Waziri wa Maliasili naUtalii, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Ulinzi na Wakuu wa Mikoa na Wilaya).  vi. Askari waliotuhumiwa kukiuka taratibu kukataa kutoa ushirikiano wa kutosha pale walipohitajika kufanya hivyo.  vii. Kutoshirikishwa kwa viongozi wa Mamlaka za Utawala katika ngazi za Mikoa na Wilaya.

 3.0 MAHOJIANO BAINA YA KAMATI NA WIZARA PAMOJA NA WABUNGE  Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya mahojiano na makundi yafuatayo:-  i. Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Taasisi zake  ii. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  iii. Waheshimiwa Wabunge

 3.1 Mahojiano baina ya Kamati na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Taasisi zake

 Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha wajumbe wa Kamati wanapata uelewa wa kutosha kuhusiana na Operesheni Tokomeza, Kamati liagiza uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ukiongozwa na Waziri, kufika mbele ya Kamati ili kueleza namna Operesheni Tokomeza ilivyoandaliwa na kutekelezwa hadi ilipositishwa kupitia tamko la Serikali lililotolewa Bungeni tarehe 01 Novemba, 2013.

 Mheshimiwa Spika, Kamati ilikutana na Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na timu yake kwa siku tatu, tarehe 28- 29 Novemba, na tarehe 01 Desemba, 2013. Katika vikao hivyo, Waziri aliieleza Kamati juu ya Mpango Kazi wa Operesheni Tokomeza, raslimali (watu na fedha) pamoja na tathmini iliyofanyika kwa kipindi ambacho Operesheni Tokomeza ilitekelezwa.

 Mheshimiwa Spika, katika mahojiano na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Kagasheki, Mb na watendaji wake Kamati ilifahamishwa yafuatayo:-

 i. Kwamba Operesheni Tokomeza ilikuwa ya kijeshikama alivyonukuliwa katika Taarifa Rasmi za Bunge (Hansard) akisema: “…Operesheni ilikuwa ya kijeshi. Ilikuwa ya kijeshi kwa sababu ilitekelezwa kwa amri ya jeshi Namba 0001/13 iliyotolewa tarehe 28 Septemba, 2013 na kusainiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi…”

ii. Kwamba, kinadharia inaonekana kwamba, Waziri wa Maliasili na Utalii ndiye alikuwa Msemaji Mkuu, lakini kiuhalisia hakuwa msemaji mkuu wa Operesheni Tokomeza kama alivyonukuliwa katika Taarifa Rasmi za Bunge akisema; “…kinadharia inaweza ikasemekana kwamba mimi ndiye msemaji mkuu, lakini mimi sikuwa msemaji mkuu wa Operesheni Tokomeza …”

iii. Utekelezaji wa Operesheni Tokomeza ulisimamiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

 iv. Taarifa za mwenendo wa operesheni zilikuwa zinapelekwa moja kwa moja kwa Mkuu wa Majeshi na kwamba, hazikumfikia Waziri wa Maliasili na Utalii.

 v. Operesheni Tokomeza iliingiliwa na Wanasiasa.

 vi. Pamoja na Mpango kazi huo kuandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa namna ambayo haieleweki Waziri hakuuona wala kuidhinisha rasimu ya mwisho ya Mpango huo. Hiyo ilidhihirika mbele ya Kamati kutokana na Waziri kukiri kwamba hakuuona wala kuudhinisha

 3.1.1 Tathmini ya Kamati kuhusu majibu ya Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na watendaji wa Wizara

 Mheshimiwa Spika,kwa kutumia tathmini ya awali ya nyaraka zilizowasilishwa pamoja na mahojiano na Waziri ilionekana kwamba, Operesheni Tokomeza iliandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake na kushirikisha vyombo vya Ulinzi na Usalama.

 Mheshimiwa Spika, licha Mpango wa Operesheni Tokomeza kuandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, hata hivyo utekelezaji wake ulisimamiwa na kuongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

 Hatua ya jeshi kuchukua jukumu la kuongoza Operesheni Tokomeza, lilifanya viongozi wa Wizara kujiengua katika jukumu la kuongoza (ead agency) na badala yake kuacha jukumu hilo kwa Jeshi pekee jambo lililotafsiriwa kwamba, Operesheni Tokomeza ilikuwa ya kijeshi.

 Mheshimiwa Spika, kupitia mahojiano ilibainika kwamba, hakukuwa na utaratibu mzuri wa kupashana habari kuhusiana na mwenendo mzima wa Operesheni Tokomeza jambo lililofanya baadhi ya wahusika kutotambua kikamilifu wajibu waokatika Operesheni hiyo.Mfano mzuri ni kwamba, licha ya kuelezwa kwenye Kanuni za Utendaji (Operational Guidelines)za Operesheni Tokomeza kwamba, Waziri wa Maliasili na Utalii ndiye atakuwa Msemaji Mkuu wa Operesheni Tokomeza, bado Mhe. Waziri hakutekeleza jukumu hilokwani alikwishatoa mapendekezo katika rasimu kwamba Msemaji Mkuu awe ni Mkurugenzi wa Wanyamapori.

 Aidha, Kamati ilibaini kuwa baadhi ya Watendaji wa juu wa Wizara walidaiwakukwamishautekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Maliasili na Utalii kutokana na kuingilia mawasiliano aliyokuwa anayafanya na baadhi ya Watumishi. Mfano ni majibizano kwa njia ya barua pepe kati ya Waziri na Katibu Mkuu, Waziri na Mkurugenzi wa Wanyamapori na pia Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Wanyamapori. Kwa mujibu wa majibizano hayo Waziri anaonekana kushangazwa na hatua ya Katibu Mkuu kuhoji hatua ya yeye kumuita mmoja wa mtumishi wa Wizara ofisini kwake. (Kiambatisho Na. 3)

 Mheshimiwa Spika, kukosekana kwa mfumo mzuri wa kupashana habari kwa pande husika kuhusu mwenendo mzima wa Operesheni Tokomeza, kulionekana kuathiri utaratibu mzima wa viongozi husika akiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, kupata taarifa zinazotakiwa kwa wakati. Hali hiyo ilichangia utekelezaji wa Operesheni Tokomeza kukumbwa na athari ambazo zingeweza kuepukika iwapo kungekuwa na mfumo mzuri wa mawasiliano.

 Mheshimiwa Spika, kupitia mahojiano pia Kamati ilibaini uwepo wa hujuma kutoka kwa viongozi wa kisiasa na Serikali ambao kwa namna moja au nyingine walionekana kuhusishwa na Operesheni Tokomeza ama wao binafsi au ndugu zao.

 Mheshimiwa Spika, miongoni mwa hujuma ambazo Kamati ilizibaini kupitia mahojiano naWaziri wa Maliasili na Utalii na Watendaji wake ni pamoja na:-  i. Baadhi ya watuhumiwa wenye mahusiano na viongozi wa kisiasa kutumia majina ya viongozi hao kuingilia utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.

 ii. Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge kutuhumiwa kujihusisha navitendo vya ujangili na biashara haramu ya nyara za Serikali.

 iii. Baadhi ya Mawaziri kutoa kauli zenye kuingilia utekelezaji wa Operesheni Tokomeza. (Mfano: kutoa maelekezo kwa wahusika wa Operesheni Tokomeza kwamba wasiguse viongozi wa kisiasa wa ngazi zote).

 iv. Baadhi ya viongozi wavyombo vya Ulinzi na Usalama kushiriki kudhoofisha utekelezaji wa Operesheni Tokomeza kwa kusindikiza au kusaidia watuhumiwa wa ujangili kutoroka. (Mfano; viongozi wa Polisi wa Wilaya na Mikoa)

 Mheshimiwa Spika, kubainika kwa hujuma hizo ni ishara tosha kwamba hata ndani ya Serikali yenyewe hakukuwa na dhamira ya dhati kwa baadhi ya kwa viongozi na watendaji katika kuhakikisha vita dhidi ya vitendo vya kijangili inapiganwa kikamilifu.

 Hali hiyo ilisababisha utekelezaji wa operesheni kukumbwa na athari nyingi kama vile; wananchi kupoteza maisha, mifugo kuuawa kwa kuchomwa moto, njaa, kiu au kupigwa risasi), upotevu wa mali, nyumba kuchomwa moto na vitendo vya ukatili dhidi ya wananchi ambavyo vilikiuka haki za kibinadamu. Hali hiyo imesababisha utekelezaji wazoezi la Operesheni Tokomeza kutafsiriwa kwamba ulilenga wananchi wasio na hatia na kuacha wahusika wa ujangili.

 3.2 Mahojiano baina ya Kamati na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 30 Novemba, 2013 Kamati ilikutana na kufanya mahojiano na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kubaini namna ilivyoshiriki katika Operesheni Tokomeza.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dk. Emmanuel Nchimbi, Mb alieleza kuwa, operesheni hii ilikuwa na lengo la kutimiza azma (Commitment) ya Serikali iliyoitoa Bungeni kwamba, inakusudia kufanya Operesheni ya kupambana na majangili. Wizara yake ilishiriki kwa kutoa Askari Polisi 504 pamoja na baadhi ya vyombo vya usafiri na kwamba vyombo vya Ulinzi na Usalama vya nchi vilikuwa vikikutana mara kwa mara kwa lengo la kuandaa mkakati wa namna ya kushirikiana katika kutekeleza mpango huo wa vita dhidi ya ujangili.

 Mheshimiwa Spika,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alikiri kuwa, licha ya lengo la operesheni kuwa zuri, kulijitokeza changamoto kadhaa zilizotokana na baadhi ya washiriki wa operesheni kwenda kinyume na malengo yaliyokusudiwa kama vile; ukatili dhidi ya mifugo na vitendo vya unyanyasaji wa wananchi kwa kuwatesa kiasi cha kuwasababishia ulemavu wa kudumu au vifo.

 Pia Mheshimiwa Waziri alikiri kwamba, kutokuwepo mfumo mzuri wa mawasiliano na Operesheni kuongozwa na jeshi, iliashiria kwamba taarifa za operesheni zilikuwa zinakwenda kwa Mkuu wa Majeshi – CDF moja kwa moja na hivyo kufanya pande zingine zinazohusika zisijue kinachoendelea.

 3.2.1 Tathmini ya Kamati kuhusu majibu ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na watendaji wake

 Mheshimiwa Spika, Kamati ilibaini kuwepo kwamawasiliano hafifu kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara nyingine zilizoshiriki katika operesheni hii.Pia,kukosekana kwa mfumo mzuri wa mawasiliano, kuliikosesha Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo iliandaa na kugharamia Operesheni Tokomeza,fursa ambazo zingeiwezesha kufanya tathmini kuhusu utekelezaji wa Operesheni hii.

 Aidha, Kamati ilibaini kwamba, hatua ya kutoshirikisha Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya ililenga kutovujisha siri dhidi ya watuhumiwa wa ujangili. Hatua hiyo ilisababisha usumbufu mkubwa kwa viongozi wa mamlaka za utawala za Wilaya na Mikoa kutokana na kulaumiwa na wananchi kwa kushindwa kuwasaidia pale walipokumbwa na matatizo.

 3.3 Mahojiano baina ya Kamati na Waheshimiwa Wabunge  Mheshimiwa Spika, kwa kuwa suala hili liliibukia Bungeni baadaya wawakilishi wa wananchi kupaza sauti kuhusu athari zilizowakumba wapiga kura wao, Kamati iliona ni busara kuhoji baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliochangia hoja hii. Wabunge hao walitoa taarifa muhimu kuhusu vitendo vilivyofanyika katika maeneo yao wakati wa operesheni.

 Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge walieleza kusikitishwa na namna ambavyo Operesheni Tokomeza ilikiuka malengo yaliyokusudiwa na badala yake ikanyanyasa wafugaji kwa kuangamiza mifugo yao na kuwaharibia mali zao kama vile; kuchoma moto nyumba, kupora fedha na vitu vingine. Mbunge mmoja alinukuliwa katika Taarifa Rasmi za Bunge akisema:- “…badala ya Operesheni Tokomeza kusaka majangili, ikageuka kuwa Operesheni Tokomeza Ufugaji…”

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge waliieleza Kamati kuwa, siyo jambo la kawaida kwa watu wanaoagizwa kufanya jambo fulani kwenda kinyume na maagizo. Wakashauri kuwa, wahusika wote waliotenda kinyume namaagizo wachukuliwe hatua stahiki ili kuepusha vitendo vya aina hiyo visijirudie katika operesheni zitakazofuata. Pia Waheshimiwa Wabunge walishauri kasoro zilizojitokeza zirekebishwe na operesheni iweze kuendelea ili kutowapa mwanya majangili kujipanga upya.

 3.3.1 Tathmini ya Kamati kuhusu majibu ya Waheshimiwa Wabunge Mheshimiwa Spika, kimsingi Waheshimiwa Wabunge wanaunga mkono Operesheni Tokomeza ambayo ililenga kukomesha vitendo vya kijangili na kunusuru raslimali za nchi hasa wanyamapori na misitu. Hata hivyo, walieleza kusikitishwa na vitendo vilivyojitokeza wakati wa utekelezaji wa operesheni na walisema haviwezi kuvumilika.

 Mheshimiwa Spika, baada ya kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge, mahojiano na viongozi na watendaji wa Wizara na kuzingatia taarifa zilizowasilishwa na Serikali, Kamati iliazimia kuzuru baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na Operesheni Tokomeza ili kufanya uhakiki.

 4.0 KAMATI KUZURU MAENEO YALIYOATHIRIKA KWA AJILI YA KUHAKIKI (VERIFICATION/OUTREACH)

 Mheshimwa Spika, kutokana na wingi wa maeneo pamoja na ufinyu wa muda, Kamati ilijigawa katika makundi matatu ili yaweze kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoainishwa katika Taarifa ya Serikali ili kufanya tathmini (verification) kwa utaratibu ufuatao:-

 4.1 Kundi la kwanza lilielekea Kanda ‘C’iliyohusisha maeneo yaliyoathiriwa na Operesheni Tokomeza katika Mikoa ya Shinyanga, Kagera, Tabora, Kigoma, Rukwa, Katavi na Singida.

 Mheshimiwa Spika, kundi hili liliundwa na Wajumbe wafuatao:-  Mheshimiwa James Daudi Lembeli, Mb, Mheshimiwa Haji Khatibu Kai, Mb na Mheshimiwa Susan Limbweni Kiwanga, Mb.

 4.2 Kundi la pili lilielekea Kanda ‘B’iliyohusisha maeneo yaliyoathiriwa na Operesheni Tokomeza katika Mikoa ya Simiyu, Mara, Arusha na Manyara.  Mheshimiwa Spika,kundi hili liliundwa na wajumbe wafuatao, Mheshimiwa Abdulkarim E. Shah, Mb, Mheshimiwa Henry Daffa Shekifu, Mb na Mheshimiwa Amina Andrew Clement, Mb.

 4.3 Kundi la tatu lilielekea Kanda ‘D’iliyohusisha maeneo yaliyoathiriwa na Operesheni Tokomeza katika Mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa, Ruvuma na Mtwara.

 Mheshimiwa Spika, kundi hili liliundwa na wajumbe wafuatao; Mheshimiwa Kaika Saning’o Telele, Mb, Mheshimiwa Muhammad Amour Chomboh, Mb na Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa, ambaye hata hivyo hakushiriki kutokana na dharura.

 Mheshimiwa Spika,kama ilivyoainishwa hapo juu lengo la Kamati kutawanyika Mikoani lilikuwa kutathmini athari zilizotokana na Operesheni Tokomeza ambayo iliendeshwa nchini kuanzia tarehe 04 Oktoba, 2013 hadi tarehe 01 Novemba, 2013.

 Mheshimiwa Spika, ili kutimiza jukumu hilo kikamilifu, Kamati iliongozwa na taarifa zifuatazo;  i. Mpango Kazi wa Operesheni Maalum ya kupambana na Ujangili nchini,  ii. Taarifa ya Utekelezaji wa Operesheni Tokomeza iliyotolewa na Serikali.  iii. Michango ya Waheshimiwa Wabunge kama ilivyonukuliwa katika Taarifa Rasmi za Bunge (Hansard).  iv. Madai yaliyotolewa na Wabunge kuhusiana na athari zilizotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.  v. Maelezo yaliyotolewa na Mashahidi ambao walihojiwa na Kamati.  vi. Vielelezo vilivyowasilishwa na Mashahidi waliofika mbele ya Kamati.

 5.0 MAKUNDI YA KAMATI YALIVYOTEKELEZA MAJUKUMU YAKE  Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumu hili, Kamati ilikutanana makundi yafuatayo:-  i. Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya  ii. Waheshimiwa Madiwani  iii. Waathirika wa Operesheni Tokomeza

 5.1 Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya  Mheshimiwa Spika, Kamati ilikukutana na Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya na kupokea taarifa iliyohusu hali ya Ulinzi na Usalama hususan wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.  Mheshimiwa Spika, kwa sehemu kubwa taarifa za Ulinzi na Usalama za Wilaya zilisaidia kuanisha maeneo na matukio yaliyojiri wakati wa Operesheni Tokomeza na athari zilizojitokeza. Wajumbe wa Kamati walitumia uchambuzi wa taarifa hizo kupata uelewa zaidi kuhusiana na utekelezaji wa Operesheni hiyo kabla ya kukutana na wananchi walioathirika ili kupata maelezo zaidi.

 5.2 Waheshimiwa Madiwani  Mheshimiwa Spika,katika baadhi ya Wilaya, Kamati ilikutana nabaadhi ya Madiwani wakiwa ni wawakilishi wa wananchi katika ngazi ya halmashauri ili kupata maelezo zaidi kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza kabla ya kukutanana waathirika wa Operesheni.

 5.3 Waathirika wa Operesheni Tokomeza  Mheshimiwa Spika, Kamati ilikutana nabaadhi ya wananchi walioathirika na Operesheni Tokomeza na kupokea maelezo na malalamiko yao kuhusu namna walivyoathiriwa na uekelezaji wa Operesheni.  Mheshimiwa Spika, wapo baadhi ya waathirika walitoa ushahidi/vielelezo vya maandishi na picha ili kuthibitisha yale waliyokuwa wakiyaeleza mbele ya Kamati. Wengine walikwenda mbali kiasi cha kuonesha majerahana makovu waliyoyapata katika miili yao kutokana na mateso waliyopata kwenye kambi maalum za mahojiano zilizoandaliwa na waendeshaji wa Operesheni Tokomeza.

 5.4 Kuzuru maeneo yaliyoathirika zaidi na Operesheni  Mheshimiwa Spika, Kamati ilipata fursa ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na athari za operesheni Tokomeza kwa lengo la kushuhudia mabaki ya vielelezo ili kujiridhisha iwapo tuhuma za athari zilizotolewa kuhusu maeneo hayo zilikuwa zakweli.

 6.0 YALIYOBAINIKA KATIKA ZIARA ZA KAMATI

 6.1 Vikao na Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa/Wilaya  Mheshimiwa Spika, katika vikaona Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa/ WilayaKamati ilibaini kuwa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza haukushirikisha viongozi wa maeneo hayo ya utawala.

 Kulikuwa na manung’uniko kwamba licha ya Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuwa wawakilishi wa Rais, waliachwa kando na Operesheni kuendeshwa katika maeneo wanayosimamia hadi malalamiko ya wananchi waliokamatwa yalipowafumbua macho kwamba walikuwa wanateswa na kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na watekelezaji wa Operesheni. Aidha,  Kamati ilielezwa kwamba utekelezaji wa Operesheni Tokomeza ulisababisha hofu miongoni mwa wananchi na viongozi na kusababisha baadhi yao kukimbia makazi. Mfano; Mkuu wa Wilaya ya Ulanga alikiri kujihifadhi kwenye Hoteli moja nje ya Wilaya yake ambako alikutana na baadhi wananchi wake waliokimbia adha za Operesheni Tokomeza.

 Viongozi hao walieleza kwamba, kimsingi hawapingi Operesheni Tokomeza Majangili kwaniililenga kunusuru raslimali za nchi hasa wanyamaporina misitu visitoweke kutokana nakushamiri kwa vitendo vya ujangili. Hata hivyo, walieleza kuwa hatua ya kutowashirikisha imelifanya zoezi hilo kuwa na kasoro nyingi pamoja na udhalilishaji hata kwa viongozi waliochaguliwa na wananchi.

 6.2 Vikao vya Kamati na Waathirika wa Operesheni Tokomeza  Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya mikutano mbalimbali katika baadhi ya maeneo ilikofanyika Operesheni Tokomezakwa lengo la kuwasilikiliza waathirika na kubaini mambo yafuatayo:-

 Watuhumiwa kupekuliwa, kudhalilishwa na baadhi kutojulikana walipo  i. Mheshimiwa Spika, badhi ya wananchi wakiwemo viongozi, Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji na Watumishi wa Serikali walikamatwa na kudhalilishwa mbele ya wananchi wanaowaongoza. Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa walikuwa hawajulikani walipo hadi Kamati ilipozuru maeneo hayo. Mfano; Vijana watatu wa Kijiji cha Osteti, Kata ya Chapakazi, Wilayani Kiteto, walituhumiwa kujihusisha na biashara ya Meno ya Tembo. Vijana hao ni Nyafuka Ng’onja, Ng’onja Kipana na Mswaya Karani.

 ii. Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa walidai kudhalilishwa mbele ya wanafamilia kwa kupewa adhabu wakiwa uchi na wanawake kushikwa sehemu za siri bila ridhaa yao. Mfano; ndugu Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga alidai kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa viboko huku mwanae wa kiume (11) akishuhudia.

 Pia alidai kulazimishwa kuchora picha ya Chatu kwa kutumia wembe kwenye paja lake. Vilevile, Bi. Neema Moses wa Babati alidai kuvuliwa nguo na kulazimishwa afanye mapenzi na wakwe zake na pia kuingizwa chupa sehemu zake za siri.

 Aidha, baadhi ya akina mama walidai kubakwa na kulawitiwa. Mfano; katika Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga, mwanamke mmoja alidai kubakwa na Askari wawili (2) wa Operesheni Tokomeza Ujangili mida ya usiku. Vilevile, mama mmoja mkazi wa Kata ya Matongo Wilayani Bariadi, alibakwa na askari watatu (3) wa Operesheni Tokomeza Ujangili huku akiwa ameshikiwa mtutu wa bunduki

 iii. Watuhumiwa waliokamatwa walifanyiwa upekuzi bila kuhusisha viongozi wa Serikali za maeneo husika na kutokuwepo kwa mashahidi na hati za upekuzi.

 Mfano; Ndg. Abdallah Pata naBi. Flora Mwarabu wa Kata ya Iputi Wilayani Ulanga na Ndg. Elias Cosmas Kibuga wa Gallapo Babati, walipekuliwa bila kufuata utaratibu.

 Ukatili na Udhalilishaji katika Kambi za Mahojiano  iv. Mheshimiwa Spika, baadhi ya watuhumiwa waliopelekwa katika kambi za mahojiano walidai kutwezwakwa adhabu zinazokiuka haki za binadamu. Mfano; Diwani wa Kata ya Sakasaka wilaya ya Meatu Ndg. Peter Samwel, alidai kuadhibiwa akiwa mtupu kwa kupewa adhabu za kijeshi kama kuning’inizwa kichwa chini miguu juu, kupigwa kwa vyuma na kulazimishwa kufanya mapenzi na mti.

 Mheshimiwa Spika, kutokana naukatili uliopitiliza, baadhi ya kambi za mahojiano zilipewa majina kama vile Guantanamo (Ruaha), Goligota (Ngorongoro), Duma na Andajega (Serengeti).

 Upotevu wa mali za watuhumiwa na faini zisizoeleweka  v. Mheshimiwa Spika, ilidaiwa kuwa wakati wa utekelezaji wa Operesheni TokomezaUjangili, baadhi ya watuhumiwa walipoteza mifugo, mali na fedha zao. Mfano; katika Wilaya ya Ulanga Kata ya Iputimwananchimmoja alidai kuporwa sanduku la VICOBA lenye shilingi laki saba na nusu (750,000/=) pamoja na simu ya mkononi na Askari wa Operesheni Tokomeza waliovamia nyumbani kwake. Vilevile Ndugu Musa Masanja wa Sakasaka Wilaya ya Meatu, alidai kuporwa shilingi laki tatu 300,000/= pamoja na simu 2 za mkononi na Askari Askari wa Operesheni.

 Mheshimiwa Spika,Pia ilidaiwa kuwa mifugo ya watuhumiwa ilikamatwa na kuingizwa ndani ya maeneo ya hifadhina kufa kwa kupigwa risasi au kukosa maji na malisho kutokana na kuzuiliwa kwa muda mrefu.

 Baadhi ya mifugo ilitozwa faini bila stakabadhi au stakabadhi kuonesha viwango vidogo ikilinganishwa na fedha halisi iliyolipwa. Mfano:Ndugu Sosoma Shimula mwenye Ng’ombe 1700 Wilayani Kasulu alidai kwamba alitakiwa kulipa faini ya shilingi Milioni thelathini (30,000,000/=, alipowasihi alipunguziwa hadi Milioni kumi na mbili (12,000,000/=) hata hivyo aliweza kulipa Milioni kumi (10,000,000/=).

 Alionesha Kamati stakabadhi inayoonesha kuwa amelipa faini ya shilingi milioni moja tu (1,000,000/=). Stakabadhi hiyo ilijazwa sehemu ya tarakimu, lakini hakuna kilichoandikwa katika sehemu ya kiasi cha fedha kwa maneno. (Tazama Kiambatisho Na. 4)

 Watuhumiwa kuteswa na kuumizwa  vi. Mheshimiwa Spika, baadhi ya watuhumiwa walidai kupigwa na kuumizwa na askari wa Operesheni na wengine kupata ulemavu wa kudumu. Mfano; katika Wilaya ya Itilima,Kijiji cha Mbogo NdgSita Rumala alidai kupigwa na kuvunjwa mkono alionesha wajumbe mkono uliokuwa umefungwa bandeji ngumu (P.O.P).

 Aidha, Diwani Peter Samwel Ndekija wa Kata ya Sakasaka, Wilaya ya Meatu, alidai kupigwa na kuumizwa vibaya mgongoni na alionesha kwa wajumbe wa Kamati makovu aliyoyapata. Vilevile,ilielezwa kuwa Ndugu Munanka Machumbe (24) ambaye ni bubu alipigwa risasi 3zilizomjeruhi mapajani na kuharibu sehemu za siri wakati akijaribu kuwahoji Askari wa Operesheni kwa ishara sababu za kumtesa baba yake.

 Aidha, katika tuko lingine Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ali Mohamed (70) aishiye kijiji cha Iputi, alidai kurushwa kichura na kutandikwabakora na Askari wa Operesheni Tokomeza.Pia,Ndg. Nyasongo Magoro Serengeti waKata ya Majimoto wilaya ya Mulele alidhalilishwa mbele ya wananchi wake. (Tazama Kiambatisho Na. 5)

 Mifugo kuingizwa hifadhini nawatuhumiwa kubambikwa kesi  vii. Mheshimiwa Spika,wakati wa Operesheni, mifugo mingi ilikuwa hifadhinilakini hata ile iliyokuwa nje ya hifadhi iliingizwa na askari wa hifadhi na wafugaji kutakiwa walipe faini ya shilingi Milioni tatu (3,000,000/=) hadi Sita (6,000,000/=) kwa idadi ya ng’ombe 30 hadi ng’ombe 100 na aliyeshindwa kulipa faini mifugo yake iliuawa au kupigwa mnada na mfugaji kufilisiwa.

 Walioshindwa kulipa faini mifugo ilipigwa mnada na wafugaji hawakuruhusiwa kununua wala kukaribia eneo la mnada, na katika mnada mifugo iliuzwa kwa bei ya chini kuliko faini iliyotozwa Mfano; shilingi elfu sitini (60,000/ kwa kila ng’ombe.

 Watuhumiwa kubambikwa kesi  viii.Ilidaiwa kwamba, baadhi ya watuhumiwa walidai kubambikwa makosa ambayo hawahusiki nayo kama vile kumiliki silaha kinyume na sheria, kukutwa na bangi au nyara za Serikalimfano; Bw. Elias Cosmas Kibuga wa Gallapo Babati alidai kubambikiwa kesi ya kumiliki bunduki kukutwa na mkia wa twiga kinyume cha sheria.

 Mheshimiwa Spika, pia Bibi Zuhura Ali wa Kilombero alidai kuteswa huku akilazimishwa kutoa silaha ambayo hakuwa nayo. Aidha, Bw. Melkzedeck Abraham Sarakikya wa Itigi alidai kuteswa akilazimishwa atoe silaha.

 Mateso na vifo kwa Watuhumiwa  ix. Mheshimiwa Spika, baadhi ya wananchiwalidai kuwa ndugu zao waliteswa kikatili kwa muda mrefuna bila kupatiwa huduma za lazima kama chakula, maji na matibabu (siku 1 -2) hadi mauti yalipowafika. Kwa mfanoNdg. Kipara Issa wa Wilaya ya Kaliua na ndugu Emiliana Gasper Maro wa Gallapo, Wilaya ya Babati.

 Aidha, wananchi hao walidaikuwa mahojiano kwa watuhumiwa yaliambatana na mateso makali kwa muda mrefu kiasi cha kusababisha vifo. (Tazama Kiambatisho Na. 6).

 Vilevile, watuhumiwa wengine waliodaiwa kupoteza maisha wakati wa Operesheni Tokomeza ni Ndg. Wegesa Kirigiti wa Kijiji cha Remagwe na Ndg. Peter Masea wa Kijiji cha Mrito (Tarime), Ndg. Mohamed Buto (Masasi) na Gervas Nzoya (Kasulu).

 Mheshimiwa Spika, pamoja na uthibitisho wa picha zilizotolewa na wananchi kuhusu kuteswa hadi kufa kwa Bi Emiliana Gasper Maro, Serikali kupitia Mkurugenzi wa Wanyamapori ilitoa Taarifa kwa Umma ikipinga Taarifa iliyorushwa na kituo cha luninga cha ITV tarehe 19 Oktoba 2013 kuhusu mauaji ya kutisha yaliyofanywa na Askari wa kupambana na ujangili.

 Taarifa hiyo ya Serikali inapinga kuwa Askari wa Operesheni Tokomeza hawauski na kifo cha mtajwa. Taarifa hiyo imeonekana kukosa umakini kutokana na kujichanganya juu ya watu inaowazungumzia. Taarifa hiyo inazungumzia majina mawili tofauti (Evelyn Gasper na Mariana Gaspar Mallo wa eneo la Olongadiola) wakati muathirika halisi ni Bi. Emilliana Gasper Maro wa Kijiji cha Orngadida, Gallapo. (Tazama kiambatisho Na.7)

 Ukatili dhidi ya Wanyama  x. Mheshimiwa Spika, kuhusu vitendo vya ukatili kwa wanyama ilidaiwa kwamba ng’ombe walipigwa risasi, na ndama walikufa kwa kukosa maziwa kutokana na mama zao kukamatwa na kuzuiwa kwenye mazizi yaliyopo maeneo ya hifadhi kwa muda mrefu. (Tazama Kiambatisho Na.  Rushwa kwenye Mapori ya Akiba

 xi. Mheshimiwa Spika,Wananchi walidai kukithiri kwa vitendo vya rushwa kwa watumishi wanaosimamia mapori ya akiba ya Maswa, Kigosi Moyowosi, Burigi, Kimisi na Mkungunero kwa kutaja majina ya baadhi ya watumishi wanaowatuhumu. Mfano; Ndg. Kileo mtumishiwa pori la Maswa, alidaiwa kuwa na tabia ya kutoza wananchi faini bila stakabadhi au kutoa stakabadhi kinyume na faini iliyotolewa au kutoa stakabadhi bandia.

 Aidha, katika pori la Kigosi-moyowosi, watumishi wafuatao walidaiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa; Ndg. Msocha, Alfred, Kobelo na Odhiambo.

 Aidha, ilidaiwa kuwa katika mapori ya Kigosi Moyowosi na Kimisi zaidi ya wafugaji 100 wenye ng’ombe wanaokadiriwa kuwa 50,000 wanalipia kuchungia ng’ombe wao kwenye mapori hayo ya hifadhi tangu mwaka 2000 kwa malipo maalum na hata Operesheni Tokomeza haikuwagusa.  Aidha, ilidaiwa kuwaNdg. Msocha (Meneja wa Pori la Akiba la Kigosi Muyowosi), alituhumiwa na baadhi ya wananchi kuwa amekuwa akiwakodisha wafugaji hao kwa vipindi vya miezi mitatu, na wafugaji huruhusiwa kulipa tena muda unapoisha. Aidha, Mfugaji ambaye hulipa kiasi kidogo hulazimishwa kulipa huku akipigwa namifugo yake kuuawa kwa kupigwa risasi.

 Ilielezwa kuwa, Wafugaji na Askari Wanyamapori huwasiliana kwa simu ilil kutekeleza makubaliano ya malipo kwa malisho yao. Nambaza simu zinazodaiwa kuwa za Askari Wanyamapori zimeorodheshwa. (Tazama Kiambatisho Na. 9)

 Mahusiano kati ya wananchi na Askari wa mapori ya Akiba  xii. Mheshimiwa Spika, wananchi wanaoishi kwenye Mapori ya Akiba yanayo wazunguka walidai kuwa katika mahusiano mabaya naAskari wa mapori hayo. Mfano;wananchi wa kijiji cha Kimotorok, Wilaya ya Simanjiro na Askari wa pori la akiba la Mkungunero kiasi cha kufikia hatua ya kutishiana maisha. Vitendo hivyo pia vipo kwa jamii zinazopakana na mapori ya Gurumeti.

 Mahakama na Magereza kuzidiwa uwezo  xiii.Mheshimiwa Spika, kutokana na Operesheni Tokomeza ilidaiwa kuwa vyombo Mahakama na Magereza katika maeneo husika vilizidiwa uwezo kutokana na wingi wa kesi na idadi ya Mahabusu. Mfano;Gereza la Wilaya ya Bunda lenye uwezo wa kuchukua jumla ya wafungwa na mahabusu 217 lililazimika kuchukua hadi watu 411.

 Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa wanalazimika kusafiri umbali mrefu kuhudhuria kesi zao. Mfano; katika wilaya ya Serengeti baadhi ya watuhumiwa walifunguliwa kesi Wilaya za Tarime, Bunda na Bariadi.  Watumishi wa Umma kuhusishwa na Ujangili

 xiv.Mheshimiwa Spika, ilidaiwa kuwa baadhi ya Watumishi waSerikali na vyombo vya dola (Polisi) wanajihusisha na ujangili. Mfano niDereva wa OCD, Wilaya ya Ngorongoro aliyetuhumiwa kujihusisha na ujangili wa Meno ya Tembo.

 Askari huyo alihojiwa na viongozi wa Operesheni Tokomeza katika kituo chake cha kazi. Vilevile, Ndg. Mohamed Ismail, Afisa Wanyamapori (W) Meatu anatuhumiwa kukutwa na nyara zaSerikali.

 Aidha,Askari Polisi wawili (2)Cpl. Isaack na PC Sixbert wa Mugumu Wilayani Serengeti walikamatwa wakiwa na meno ya Tembo.  Mheshimiwa Spika, pia ilidaiwa kuwa baadhi ya Maofisa wa Serikali wamekuwa wakitumia magari ya Umma ama kusafirisha au kusindikiza watoroshaji wa nyara za Serikali. Mfano nigari la Serikali lililokamatwa likifaulisha meno ya Tembo kutoka kwenye gari jingine huko Mkuranga kwa lengo la kuyasafirisha kwenda Dar es Salaam.

 Sambamba na hilo baadhi viongozi wa jeshi la Polisi wametuhumiwa kusaidia watuhumiwa wa vitendo vya kijangili kutoroka na kuepuka mkono wa sheria.

 Migogoro kuhusu mipaka ya Maeneo ya Hifadhi  xv. Mheshimiwa Spika,wananchi walidai kuwa baadhi ya Mapori ya Akiba naHifadhi yamekuwa yakipanua mipaka yake bila kushirikisha wananchi wa maeneo yanayowazunguka. Mfano; wananchi wa Wilaya ya Bunda wanaopakana na Pori la Akiba la Gurumeti.

 Pia, wananchi wa vijiji vya Kegonga na Masanga, katika Kata ya Nyanungu, Wilayani Tarime wako katika mgogoro wa mpaka na TANAPA wakidai kuwa bonde la Nyanungu limemezwa na eneo la Hifadhi kutokana na TANAPA kuongeza mipaka yake bila kushirikisha wananchi wa maeneo hayo.  Aidha, katika Wilaya ya Ulanga kuna mgogoro katika kata za Iputi na Lupiro dhidiHifadhi ya Selous.

 Idara za Wanyamapori katika Halmashauri kukosa vitendea kazi  xvi.Mheshimiwa Spika, kutokana na silaha za Idara ya Wanyamapori katika baadhi ya Halmashauri kuchukuliwa wakati wa Operesheni Tokomeza kwa ajili ya uchunguzi, wananchi wamedai kupata shida kutokana na wanyama hasa Tembokuvamia mashamba na kuharibu mazao pamoja na kujeruhi au kuua watu na mifugo.

 Wanasiasa kushawishi wananchi kuishi kwenye maeneo ya Hifadhi  xvii. Mheshimiwa Spika, wakati wa kutekeleza Operesheni Tokomeza ilidaiwa kuwa nyumba na maboma ndani ya mapori ya akiba zilichomwa moto. Mfano; Wilaya ya Sumbawanga kijiji cha Msila Kata ya Mfinga na kijiji cha Kabage Wilaya ya Mpanda. Hata hivyo baadhi ya wananchi wameanza kurejeakatika baadhi ya maeneo ya hifadhi kutokana na ushawishi wa wanasiasa.

 Mfano; katika Pori la Hifadhi ya Jamii Ubende Wilaya ya Mpanda walichangishwa shilingi laki moja (100,000/ kwakila kaya kwa ajili ya kupatiwa huduma za kisheria iwapo mamlaka husika zitajaribu kuwaondoa ndani ya hifadhi. Aidha, Kamati ilipata taarifa kuwa, baadhi ya viongozi wa Vyama vya Siasa wamekuwa wakigawa kadi za vyama vyao kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya hifadhi na kwa ahadi kwamba, vyama walivyojiunga nga navyo vitawatetea wasiondoke katika maeneo hayo.

 Tatizo la Vibali vya Wakulima wa Muda  xviii. Mheshimiwa Spika, Kamati ilielezwa lipo tatizo la raia wa nchi jirani kuingia nchini na kupewa vibali vyakuendesha shughuli za kilimo(Peasant Permit)kwa muda, ambavyo hutolewa bilakubandika picha ya mhusika/mwombaji hasa maeneo ya Karagwe.

 Raia hao wanadaiwa kutumia nakala za vibali hivyo kuingiza nchini wahamiaji haramu ambao baadhi yao huingiza makundi makubwa ya mifugo hasa ng’ombe na wengine kutumia mwanya huo kuingiza silaha na kujihusisha na vitendo vya ujangili katika baadhi ya mapori ya akiba. Mfano; Pori la Akiba la Ibanda Rumanyika.

 Vilevile kuna tatizo la majangili kutumia vivuli va wafugaji kuingia kwenye hifadhi huku wakiwa wameficha silaha, na hivyo kuwepo mazingira ya kushindwa kutofautisha kati ya majangili na wafugaji hususan katika maeneo ya hifadhi ya Ruaha.

 xix.Mheshimiwa Spika, kuna mgogoro katika eneo la Ushoroba (Buffer Zone) katika Kata za Lupiro, Mbugana Iputi Wilaya ya Ulanga, maeneo ambayo jamii imejenga miundombinu kwa miaka mingi ikiwa ni pamoja na shule, nyumba, mashamba, misikiti na makanisa huku Serikali ikiwa kimya kwa muda mrefu.Hata hivyo, wakati wa Operesheni Tokomeza wananchi hao walilazimishwa kuhama bila kuelekezwa waende wapi.

 Michango ya Waheshimiwa Wabunge kuhusu Operesheni  xx. Mheshimiwa Spika, Kamati ilibaini kuwa baadhi ya michango iliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge wakati wakichangia Hoja ya Mhe. Saidi Nkumba haikuwa imefanyiwa utafiti wa kutosha kwani baadhi ya madai waliyoyatoa hayakuwa na uhusiano na Oparesheni Tokomeza.

 Kwa mfano;ni kweli kwamba ng’ombe 51 walitumbukia katika mto Rubana Wilayani Bunda na kufa, hata hivyo tukio hilo lilitokea mwezi April, 2013 ikiwa ni miezi 6 kabla ya Operesheni. Aidha, ni kweli kuwa Wakazi wa Vijiji vya Kabage Wilayani Mpanda na Luchima Wilayani Mulele walihamishwa kutoka katika maeneo ya hifadhi na nyumba zao kuchomwa moto katika utaratibu uliofanywa na Halmashauri hizo mwezi Septemba, 2013 kwa lengo la kuwapeleka kwenye maeneo rasmi ya makazi.

 7.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI KUHUSU TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA OPERESHENI TOKOMEZA

 Mheshimiwa Spika, baada ya Kamati kuchambua nyaraka husika kuhusiana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza, kuwahoji viongozi mbalimbali wa Wizara na Waheshimiwa Wabunge, pamoja na kufanya ziara mikoani kwa lengo la kuhakiki yaliyojiri kutokana na Operesheni Tokomeza, Kamati inapenda kutoa maoni na ushauri ufuatao:-

 i. Kwa kuwa, lengo la Operesheni Tokomeza lilikuwa kunusuru raslimali za nchi hususani Wanyamapori na hasa Tembo na Misitu, na kwa kuwa Waheshimiwa Wabunge na Wananchi wameiunga mkono mbali na matatizo ya kiutendaji yaliyojitokeza, hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba, Serikali irekebishe haraka kasoro zilizojitokeza katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza ili kuendeleza na kukamilisha awamu zote za operesheni kama zilivyo kwenye mpango na kunusuru raslimali za Taifa hasa wanyamapori na misitu ambayo inatishiwa kutoweka kutokana na vitendo vya ujangili.

 ii. Kwa kuwa,Kamati imejiridhishakwamba matatizo na upungufu uliojitokeza katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza yamechangiwa na maandalizi mabaya ya Mpango kazi ambao Waziri Mwenye dhamana hakuidhinisha, na kwa kuwa, imedhihirika kuwepo hali ya sintofahamu (kwa mujibu wa hansard) iliyosababishwa na watendaji wakuu wa Wizara kwa makusudi kuamua kutomshirikisha kikamilifu Waziri katika hatua za mwisho za maandalizi ya Mpango kazi, hivyo basi Bunge linaazimia kwamba, Serikali iwachukulie hatua stahiki za kinidhamu Wasaidizi Wakuu wote wa Waziri walioshiriki katika Mpango kazi huo.

 iii. Kwa kuwa, Kamati imebaini kwamba pale Jeshi la Wananchi (JWTZ) linaposhirikishwa katika Operesheni ufanisi mkubwa hupatikana, na kwa kuwa, bado iko haja ya kuendeleza Operesheni Tokomeza kwa maslahi ya Taifa, na kwa kuwa ushahidi wa mazingira ‘circumstantial evidence’ unaonesha kuwa Jeshi lilichukua uongozi wa operesheni baada ya kugundua kuwa washiriki kutoka Vikosi vingine (Polisi, TANAPA, TSF na NCAA) kwa kushirikiana na wafugaji wenye ushawishi wa kifedha pamoja na wanasiasa, walihujumu operesheni hiyo kwa kutoa taarifa kwenye mtandao mkubwa wa kijangili ambao umejengeka kuanzia Wizarani hadi kwenye maeneo ya Hifadhi na kusaidia ‘majangili papa’ wasikamatwe, hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba:-

 – Serikali kuchukua hatua za makusudi kuuvunja mtandao huo na pia;  – Kuandaa operesheni nyingine ambayo itapangwa na kutekelezwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Idara ya Usalama wa Taifa.

 iv. Kwa kuwa, kumekuwepo na operesheni kadhaa kabla ya Operesheni Tokomeza ambazo zililenga kupambana na ujangili, na kwa kuwa, Operesheni Tokomeza imeshindwa kupata mafanikio yaliyotarajiwa, na kwa kuwa, ushahidi wa mazingira unaonesha wazi kwamba, Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) kimeshindwa kutimiza wajibu wake, hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba, Serikali iimarishe kikosi hicho kwa kukifanyia tathmini na kukiunda upya ikiwa ni pamoja na kukiwezesha kwa rasilimali (Watu, fedha, magari, silaha za kisasa na vifaa vya mawasiliano kama redio na simu).

 Serikali iunde chombo ambacho kitakuwa na jukumu la kusimamia na kutathmini utendaji kazi wa KDU. Iwapo utaratibu huo utazingatiwa ni wazi vitendo vya ujangili vitadhibitiwa bila kutumia operesheni kubwa kama Uhai na Tokomeza.

 v. Kwa kuwa, Kamati imebaini kuwepo kwa vitendo vya utesaji na ukatili wa hali ya juu, ukiukwaji wa haki za binadamu na uzembe miongoni mwa Askari wa Operesheni Tokomeza (ushahidi wa wahusika upo), hali ambayo imesababisha baadhi ya Wananchi kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu pamoja na kupoteza mali zao. Hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba:-

 – Serikali Iwabaini wote waliohusika na vitendo vya kinyama, mateso na udhalilishaji dhidi ya watuhumiwa, iwachukulie hatua stahiki na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa agizo hili katika Mkutano ujao wa Bunge.

 – Ifanye tathmini ya kina kwa kupitia Wakuu wa Mikoa na Wilaya ili kujua athari za Operesheni hii na kutafuta njia ya kutoa kifuta machozi kwa waathirika, ili kurejesha imani ya Wananchi kwa Serikali yao.

 vi. Kwa kuwa, Kamati imebaini kuwa Operesheni Tokomeza ilikuwa haikutengewa fedha katika Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 na kwa kuwa kiasi cha fedha Tshs. 3,968,168,667/= kilichopatikana kutoka Idara na Mashirika Tanzu ya Wizara haikutosheleza mahitaji ya fedha ya Operesheni Tokomeza kutokana na ukubwa wa eneo la Operesheni, hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba, Serikali itenge Bajeti Maalum ya kutosheleza mahitaji ya Operesheni Tokomeza.

 Serikali kutenga Bajeti kwa ajili ya kuendeleza shughuli za uhifadhi katika maeneo ya Hifadhi ikiwa ni pamoja na kuweka raslimali watu ya kutosha na miundombinu mingine muhimu.

 vii. Kwa kuwa, Kamati imebaini kuwa Taarifa kwa Umma iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori tarehe 23 Oktoba 2013, haikuwa sahihi na pia ililenga kuudanganya Umma kwa kuficha mazingira na sababu za kifo cha Bi Emilliana Gasper Maro, hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba, Serikali ichukue hatua za kumwajibisha Mkurugenzi wa Idara ya Wanyapori kwa kuudanganya umma kwa kujaribu kuficha ukweli.

 viii.Kwa kuwa, Kamati imebaini kuwa kumekuwapo mchezo mchafu unaofanywa na baadhi ya Maafisa Wanyamapori, Maafisa Misitu katika mapori ya akiba, Misitu ya Serikali na katika baadhi ya Hifadhi za Taifa wa kupokea rushwa, kutesa wananchi, kuwabambika kesi na kujihusisha na ujangili,na kwa kuwa Kamati inayo majina na vielelezo vya wahusika, hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba, Serikali ifanye tathmini nchi nzima kwa lengo la kutambua kiwango cha vitendo vya rushwa miongoni mwa watumishi hao, na kuwachukulia hatua stahiki za kinidhamu wale watakaobainika kuhusika ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

 ix. Kwa kuwa, Kamati imebaini kuwa baadhi ya viongozi wa kisiasa na Serikali waliingilia utekelezaji wa Operesheni Tokomeza kwa manufaa yao binafsi, kwa mfano, agizo la kuwataka wahusika wa Operesheni Tokomeza kutowagusa Viongozi wa Kisiasa wa ngazi zote, kauli ambayo ilitafsiriwa kuathiri utekelezaji wa Operesheni Tokomeza kwa kubagua Watanzania katika makundi ya Viongozi na Wananchi wa kawaida, hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba, Serikali ihakikishe kuna uwajibikaji wa pamoja pale inapoamua kutekeleza jambo la Kitaifa kama Operesheni Tokomeza.

 x. Kwa kuwa, Kamati imethibitisha kuwa, baadhi ya wanasiasa wamekuwa wanawadanganya wananchi waliothibitika kufanya shughuli za uchumi kwenye maeneo ya hifadhi, na kuwaahidi kuwatetea pindi Serikali inapochukua hatua za kuwaondoa katika sehemu hizo, ikiwa ni pamoja na kuwapa kadi za vyama vyao vya siasa, hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba, serikali ihakikishe kwamba, wananchi hawaendeshi shughuli za kiuchumi kwenye maeneo ya hifadhi na kuwaonya wanasiasa waache kuwalaghai wananchi kwa maslahi yao binafsi.

 xi. Kwa kuwa,Kamati imebaini kwamba katika baadhi ya maeneo ya mipakani mfano Karagwe, Idara ya Uhamiaji hutoa vibali kwa raia wa nchi jirani vya kuishi na kulima hapa nchini, vibali ambavyo havina udhibiti wala tija kwa nchi, na kusababisha migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji lakini pia uharibifu wa mazingira kwa kuingiza mifugo hifadhini, hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba, Serikali isitishe mara moja zoezi la kutoa vibali hivyo, kufuta vilivyopo na kuwataka raia hao wa kigeni wenye vibali kuondoka Nchini mara moja.

 xii.Kwa kuwa, Kamati imebaini kwamba zaidi ya asilimia 25 ya eneo la Nchi ni hifadhi, namipaka ya maeneo mengi yaliyohifadhiwa haijaainishwa, na kwa kuwa Serikali haina uwezo wa (raslimali watu na fedha) wa kusimamia na kulinda mipaka ya maeneo haya kikamilifu, hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba, Serikali kufanya yafuatayo:-

• Kuridhia Idara ya Wanyamapori na Wakala wa Huduma ya Misitu kuajiri idadi ya watumishi wanaotakiwa kama Serikali bado inaendelea kuyahifadhi maeno hayo. • Kuainisha mipaka ya mapori yote ya akiba, hifadhi za taifa na Misitu ya Serikali kwa alama maalumu na za kudumu ili kuepusha Wananchi kuingia katika maeneo hayo kwa kutojua mipaka. • Kuyaachia mapori ya Serikali ambayo yamekosa sifa, ili yatumike kwa kilimo na ufugaji kwa kuzingatia mpango wa matumizi bora ya ardhi.

 xiii.Kwa kuwa,yapo maeneo ya mapori na Hifadhi ambayo yana migogoro ya muda mrefu ambapo wananchi wameishi katika maeneo hayo kwa muda mrefu, hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba, Serikali irekebishe mipaka husika au iwahamishie Wananchi hao kwenye maeneo mengine yenye miundombinu. Serikali iwaagize Mawaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Maliasili na Utalii na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutembelea maeneo yote yenye migogoro nchini na kuitafutia ufumbuzi ili wananchi waweze kuelewa hatma yao katika maeneo hayo kwani wamekuwa katika hali ya sintofahamu kwa muda mrefu.

 xiv.Kwa kuwa, Kamati imebaini kuwepo kwa migogoro baina ya Wananchi, Wawekezaji na hifadhi katika maeneo ya Meatu, Tarime, Bunda na ile ya Loliondo na Kimotorok ambayo inashughulikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba, Serikali ihakikishe inamaliza (kama ilivyoahidi) migogoro iliyopo Loliondo na Kimotorok na maeneo mengine mapema iwezekanavyo.

 Kurekebisha haraka kasoro zote za kisheria zilizokiukwa kwa makusudi na Idara ya Wanyamapori kiasi cha kusababisha mgogoro baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu na mwekezaji katika Pori la Hifadhi ya Jamii la Makao pamoja na kuwawajibisha Watendaji wa Idara ya Wanyamapori waliosababisha mgogoro huo.

 xv.Kwa kuwa, Kamati imebaini kwamba, migogoro wanayokumbana nayo wafugaji kutokana na kuingiza mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na kero nyingine ni kutokana na kukosekana kwa miundombinu sahihi na endelevu kwa ajili ya ustawi wa mifugo, na kwa kuwa, Mheshimiwa Rais aliunda Wizara mahsusi kwa ajili ya kuendeleza Sekta ya Mifugo nchini akitambua umuhimu wa Sekta hii kwa uchumi wa Taifa, na kwa kuwa, Tanzania ni ya pili kwa wingi wa mifugo Barani Afrika, ni wazi kwamba adha wanazokumbana nazo wafugaji ni matokeo ya kutokuwepo sera na mipango madhubuti ya muda mfupi na mrefu.

 Hivyo basi, Bunge linaishauri Serikali kumtaka Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, kujipima na kuona iwapo bado anastahili kuendelea kuhodhi wadhifa alionao.

 xvi.Kwa kuwa, Kamati imebaini kuwa baadhi ya madai yaliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge Bungeni wakati wakichangia Hoja ya Mhe. Saidi Nkumba ilikuwa ni ya kweli; na kwa kuwa yaliyoelezwa katika madai hayo hayana uhusiano na Operesheni Tokomeza kwani yalitokea kabla ya Operesheni hiyo; hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba, Waheshimiwa Wabunge kuwa makini zaidi na kufanya utafiti kwa lengo la kuhakikisha michango yao inakuwa sahihi na inalenga hoja mahsusi iliyo mbele ya Bunge.

 8.0 HITIMISHO

 Mheshimiwa Spika, jukumu uliloikabidhi Kamati hii lilikuwa zito na lilihitaji umakini mkubwa na muda wa kutosha katika kulitekeleza. Kutokana na ufinyu wa muda na mazingira magumu wakati wa kutekeleza jukumu hilo, Kamati inakiri kwamba haikuweza kutembelea maeneo yote yaliyoathirika na zipo lawama kutoka kwa baadhi ya wananchi kwamba, Kamati haikuweza kupita katika maeneo yao.

 Mheshimiwa Spika, Kamati inapenda kuwahakikishia wananchi wote kuwa, kupitia taarifa mbalimbali za viongozi na wawakilisihi wa waathirika mbele ya Kamati, malalamiko yao yamezingatiwa na kufanyiwa kazi.

 Mheshimiwa Spika,kama tulivyoeleza katika maelezo yetu ya utangulizi, Kamati inaamini na kote tulikopita wananchi wanakiri kuwa, lengo na azma ya Serikali kuanzisha Operesheni Tokomeza Ujangili lilikuwa jema kwani lililenga kunusuru maliasili zetu kwa ajili ya maendeleo endelevu na heshima ya Taifa letu.

 Mheshimiwa Spika, Kamati inaamini maelezo yote yaliyotolewa na wananchi pamoja na viongozi wao yalikuwa na dhamira njema. Aidha, mapendekezo yaliyotolewa na Kamati yanalenga kuisaidia Serikali kuchukua hatua za makusudi na haraka kurekebisha kasoro zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, ili kuepuka kutokea kwa vitendo vinavyoashiria ukiukwaji wa misingi ya haki za binadamu na Utawala Bora nchini.

 Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru wewe binafsi kwa dhati kutokana na kuiamini Kamati yangu na kuikabidhi jukumu hili zito. Hii ni ishara tosha kwamba una imani na Wabunge wako na kwamba wanaweza kufanya kazi kwa niaba yako.

 Mheshimiwa Spika, pia nitoe shukrani za dhati kwa Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Didimu Kashilillah, kwa kuiwezesha Kamati hii kufanya kazi yake vizuri na kuikamilisha kwa wakati. Aidha, kwa namna ya pekee napenda kuwashukuru makatibu walioihudumia Kamati hii wakiongozwa na Ndugu Theonest K. Ruhilabake ambao ni Ndugu Gerald Magili, Ndugu Chacha Nyakega na Ndugu Stanslaus Kagisa.

 Aidha, ninapenda kuwashukuru viongozi wa Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji ambao walionyesha ushirikiano mkubwa Kamati ilipotembelea maeneo yao.

 Mheshimiwa Spika, mwisho lakini si kwa umuhimu Kamati inawashukuru watumishi wafuatao; Ndugu Silva Chindandi, Ndugu Ndigwako Mwaigaga, Ndugu Victoria Mizengo, Ndugu Germina Magohe na watumishi wengine ambao kwa namna moja au nyingine walishiriki katika kuihudumia Kamati hii hadi inakamilisha taarifa hii.

 Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

 James Daud Lembeli, Mb  MWENYEKITI KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA

By Yericko Nyerere

CIA ina jela za siri na za kuogofya Saudi Arabia

By WikiLeaks01 Spy.

Wanadiplomasia wa nchi za Kiarabu wenye uhusiano na utawala wa Aal Saud nchini Saudi Arabia wamesema kuwa, nchini humo kuna jela za siri ambazo zinafanya shughuli zake chini ya uongozi na usimamizi wa moja kwa moja wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA.

Kanali ya Televisheni ya al Manar ya Lebanon imetangaza kuwa jela hizo zinawashikilia mahabusu waliotekwa nyara katika nchi mbalimbali za Asia, za Kiarabu na Kiafrika. Imeelezwa kuwa moja ya jela hizo iko katika mji wa Tabuk kaskazini magharibi mwa Saudi Arabia na hakuna mawasiliano yoyote kati ya mahabusu hao na familia zao.

Vilevile taarifa zinasema kuwa, baadhi ya mahabusu wameuawa kutokana na mateso wanayoyapata ndani ya jela hizo za siri na za kuogofya zinazosimamiwa na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA nchini Saudi Arabia.

By Yericko Nyerere

John F. Kennedy’s assassination is shown

 

By Alec Travelyan wikileaks01 team

 

The evidence of the government’s cover-up of John F. Kennedy’s assassination is shown in a single file, with autopsy photos and an x-ray. There is no possible other explanation for what they have done. No government apologist can possibly come up with a logical argument against the cover-up. Autopsy photos were taken after the back of JFK’s head was reconstructed in order to tell us that a blowout happened to the front of his head. The cover-up was as extensive as it possibly could have been. Because the government covered up his assassination to the full extent of their abilities, they have to be the ones responsible for his assassination since they would not have done this for a communist plot, or for just the mafia.

 

The evidence of the government’s cover-up of John F. Kennedy’s assassination is shown in a single file, with autopsy photos and an x-ray. There is no possible other explanation for what they have done. No government apologist can possibly come up with a logical argument against the cover-up. Autopsy photos were taken after the back of JFK’s head was reconstructed in order to tell us that a blowout happened to the front of his head. The cover-up was as extensive as it possibly could have been. Because the government covered up his assassination to the full extent of their abilities, they have to be the ones responsible for his assassination since they would not have done this for a communist plot, or for just the mafia.

 

 

 

 

 

 

By Yericko Nyerere

UCHUNGUZI KUHUSU JARIBIO OVU LA KUCHOMA MOTO OFISI ZA CHADEMA ARUSHA

UCHUNGUZI KUHUSU JARIBIO OVU LA KUCHOMA MOTO OFISI ZA CHADEMA ARUSHA  

 

 

na 3/12/2013 jaribio baya lilifanyika dhidi ya kuchoma ofisi ya CHADEMA ya Kanda ya Kaskazini na Mkoa wa Arusha .  Hata hivyo Jeshi la Polisi lilifika kwa ajili ya uchunguzi wa awali na Chama kilielekeza Kitengo chake cha Usalama na Ulinzi kuanza kufuatilia jambo hilo kwa kina ili kubaini wahalifu wa jaribio hilo baya . Taarifa ambazo tumepokea mpaka sasa ni taarifa muhimu ambazo tunahamini zitaisadia Jeshi la Polisi katika uchunguzi wake.  Tumepeleka majina ya Watu ambao taarifa zetu za kina zinaonyesha wanahusika na tukio hili takribani wasiozidi watano na ni imani yetu kuwa Jeshi la Polisi litachukuwa hatua muhimu katika uchunguzi wao huku Chama tukiwa tiyari kabisa kutoa ushirikiano wa dhati katika uchunguzi wa kina na wakitaalaamu ambao utaweza kuthibitisha udadisi wetu na uchunguzi wetu ili kuponya Taifa letu .  Hata hivyo Chadema kinalitaka Jeshi la Polisi kutokufanya Siasa katika jambo hili kwani ni muhimu wakaelewa kwamba kupuuza uchunguzi wa jambo hili ni hatari kwa Mkoa wa Arusha na mustakabali wa Amani ya Taifa letu . Chama katika utafiti wake kimebaini kuwa miongoni mwa washukiwa katika tukio hili wamekuwa ni Vijana ambao wamekuwa wakifanya kazi na Polisi katika jitihada za kuhujumu Chadema na hivyo kunaleta mashaka makubwa juu ya uchunguzi wa jambo hili kama utafanyika kwa ufasaha na weledi wa hali ya juu kwa majina ambayo Chama imemkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa .  Hata hivyo katika uchunguzi wake Chadema inasikitishwa sana na kitendo cha Serikali kumpatia mmoja wa washukiwa umiliki wa silaha aina ya bastola wakati Mtu huyo akiwa na rekodi ya kuwa na kichaa cha mara kwa mara .  Chadema Kanda ya Kaskazini inawataka Wanachama wake na wafuasi watulie kimya bila kutafakari aina yeyote ya kisasi kwa jaribu hili baya ili kutoa fursa njema kwa Viongozi wao na Jeshi la Polisi ili kuwabaini Watu hawa waliotaka kuteketeza Ofisi ya Chama kwa moto . Lakini pia Chadema inamshukuru sana na kumpongeza mmiliki wa nyumba hiyo kwa kutambua majaribu ambayo tumepitia wakati huu kwa kukubali kurekebisha nyumba ambayo ni ofisi yetu kwa gharama zake mwenyewe kama sehemu ya kuheshimu jitihada za kushinda hofu na woga unaotaka kupandikizwa miongoni mwa jamii yetu .

 

 

 NANYARO E.J.  

 

Mwenyekiti Wilaya Arusha

 

  4/12/2013

By Yericko Nyerere

Edward Snowden ‘attended hacking course in India’

 

Edward Snowden ‘attended hacking course in India’

Delhi-based training institute says Snowden took ‘security analyst and ethical hacker’ course in 2010 and was an ‘intelligent, quiet’ student

 

 

According to the Delhi-based Koenig training institute, Mr Snowden attended a six-day

 

Dean Nelson

By  Dean Nelson, New Delhi

4:42PM GMT 04 Dec 2013

  

 

 

Edward Snowden, the CIA contractor who revealed the scale of America’s internet surveillance around the world, may have learned the hacking skills to leak thousands of files on a £1,000 course he attended in India.

According to the Delhi-based Koenig training institute, Mr Snowden attended a six-day “security analyst and ethical hacker” course in 2010, two years before he disclosed the files which outraged foreign leaders and embarrassed his government.

Last night the company told the Daily Telegraph that the rogue analyst had contacted them in 2009 to join the course and later paid the fee for his tuition and extra for his boarding in Karol Bagh, a grimy market district of the Indian capital.

The company’s Delhi training centre manager, Hema Sharma, said he had first contacted the company in 2009 and paid for his course in advance by Paypal before joining later in September 2010. He had been a quiet student who had stayed in his hostel room and focused entirely on his course.

“He was an intelligent, quiet and cooperative student,” Mr Sharma said. “A thorough hacking professional, who preferred to maintain a low profile and not share details about [his] personal life. He got in touch with us in 2009 and in September 2010 joined the course. We provided him accommodation and other facilities.

 

Related Articles

Guardian journalists could face criminal charges over Edward Snowden leaks  03 Dec 2013

Edward Snowden spy leaks: Liam Fox in push for Guardian newspaper to be prosecuted  09 Nov 2013

Terrorists are ‘rubbing their hands with glee’ after Snowden leaks  07 Nov 2013

Edward Snowden leaks ‘could help paedophiles escape from the police’  06 Nov 2013

Snowden leaks caused ‘serious damage’ to national security  06 Nov 2013

“He made the initial payment through PayPal and the rest through his credit card. It was a self-sponsored course. He mostly spent time at the institute and used to go out rarely.

He addded: “Certainly his course here included some elements which may have helped him in what he did. But overall he was a very intelligent student and good learner.”

The course required a year’s experience in managing Windows and Linux systems, a detailed knowledge of internet protocol (IP) addresses, and allowed Mr Snowdon to become a “Certified Ethical Hacker”, and an EC-Council Certified Security Analyst (ECSA). “Through groundbreaking penetration testing methods and techniques, ECSA class helps students perform the intensive assessments required to effectively identify and mitigate risks to the security of the infrastructure”, the company’s course prospectus explains.

 

 

 

 

 

 

 

 

   

 

 

 

   

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

    

 

 

  

 

   

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

    

 

 

 

 

 

 

By Yericko Nyerere

CHADEMA Yazindua Sera Mpya

Na http://www.Chadema.or.tz

Leo tarehe 01/12/2013 Chama kimezindua rasimu ya sera mpya ya mabadiliko ya Tabia ya nchi. Akizindua Sera hiyo Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya Ndani wa Chama Mh. John John Mnyika (Mb) ambaye aliambata na Katibu wa Baraza la Wanawake la Chama Mh. Naomi Kaihula, Afisa wa Sera na Utafiti wa Chama Mh. Mwita Waitara pamoja na Maafisa wengine wa Chama; Mh. Mnyika amesema CHADEMA ndio taasis ya kwanza kuzindua sera hiyo hapa nchini.

“CHADEMA ndio Chama cha kwanza hapa nchini na Afrika kuwa na Sera ya Mabadiliko ya Nchi. Hata serikali yetu pamoja na kuwa Rais na Viongozi wengi wa Serikali wameshashiriki mikutano mingi kuhusu athari za Mabadiliko ya Tabia ya nchi lakini mpaka leo Tanzania haina Sera ya kukabiliana na janga hili” Alisema Mnyika.

Mh. John John Mnyika Mh. John John Mnyika

Mnyika aliongeza kuwa Rais ameshashiriki mikutano mingi akitolea mfano mkutano wa hivi karibuni uliofanyikanchini Scotland ambapo Rais alihudhuria ukiwa ni mkutanowa 19. Mikutano hiyo inayojulikana kwa jina la CORP imekuwa ikifanyika kila mwaka katika nchi mbalimbali ambapo mwaka juzi ulifanyikia Daban Afrika Kusini, mwaka jana ulifanyikia Doha Qatar na mwaka huu umefanyikia Scotland.

Mnyika ameongeza kuwa kilichozinduliwa leo ni rasimu iliyoandaliwa baada ya kukusanya maoni kwa wadau mbalimbali wakiwemo wataalam wa mazingira na sasa kitakachofanyika ni kukusanya maoni kutoka kwa Watanzania kwa muda wa mwezi mmoja na baadae Sera kamili itazinduliwa.

Sera hiyo inapatikana katika tovuti yetu katika kipengele cha Sera za Chama. Unaweza kuisoma na kutoa maoni yako kwa anuani zinazoonekana katika tovuti yetu au hapa hapa kwenye tovuti http://www.chadema.or.tz

 

By Yericko Nyerere