By WikiLeaks01 Spy.
Wanadiplomasia wa nchi za Kiarabu wenye uhusiano na utawala wa Aal Saud nchini Saudi Arabia wamesema kuwa, nchini humo kuna jela za siri ambazo zinafanya shughuli zake chini ya uongozi na usimamizi wa moja kwa moja wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA.
Kanali ya Televisheni ya al Manar ya Lebanon imetangaza kuwa jela hizo zinawashikilia mahabusu waliotekwa nyara katika nchi mbalimbali za Asia, za Kiarabu na Kiafrika. Imeelezwa kuwa moja ya jela hizo iko katika mji wa Tabuk kaskazini magharibi mwa Saudi Arabia na hakuna mawasiliano yoyote kati ya mahabusu hao na familia zao.
Vilevile taarifa zinasema kuwa, baadhi ya mahabusu wameuawa kutokana na mateso wanayoyapata ndani ya jela hizo za siri na za kuogofya zinazosimamiwa na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA nchini Saudi Arabia.