KAMATI YA KUHAKIKI MALI ZA CHAMA
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana Aprili, 2007 mjini Dar es Salaam iliunda Kamati ya Wataalam kwa ajili ya uhakiki mali za Chama. Majina ya Wataalam hao ni:-
(1) Ndg. Peter Machunde – Fedha na Vitega Uchumi (2) Ndg. George Fumbuka – Fedha na Vitega Uchumi (3) Ndg. Sam Mapande – Mwanasheria (4) Ndg. Kanyoni Salum Kanyoni – Mhandisi (5) Ndg. Jacquiline Noni – Mfanyabiashara (6) Ndg. Simon Mapolu – Mchumi (7) Ndg. Janeth Mbene – Mchumi (8) Ndg. Ussi Faki – Mkaguzi Katibu wa Kamati hiyo alikuwa Ndugu L.L. Burugi – Meneja Miliki wa Chama.
Kamati ilianza kazi tarehe 19/6/2007 na kukamilisha tarehe 28/10/2007. Kazi ya Kamati hii ililenga mali za Kudumu za Chama zilizopo Makao Makuu, Mikoani na katika Wilaya zilizopo kwenye Makao Makuu ya Mikoa. Aidha, zoezi hili lilihusisha pia mali za Jumuiya za Chama katika maeneo hayo pamoja na kufanya tathmini ya mwenendo wa Makampuni ya Chama.
12. BAADHI YA MADENI AMBAYO CHAMA KINADAIWA (1) MADENI YA BENKI NA TAASISI ZA FEDHA NBC Ltd. – 143,763,404.00 NSSF – 831,822,961.50 Ukaguzi wa Hesabu – 72,240,000.00 1,107,826,365.50
Deni la NBC ni la tangu mwaka 1994 kupitia Kampuni ya Chama TANTI kwa kuweka rehani nyumba 10 za CCM zilizoko Area ‘C’ – Dodoma.
Mkopo wa NSSF unahusu Jengo la CCM Shinyanga. NSSF walimalizia kujenga Jengo. Mazungumzo yalifanyika kati ya CCM/NSSF na kufikia makubaliano ya Chama kununua Jengo hilo kwa shs. 1,109,097,282/= kiasi cha 25% kimelipwa.
Deni la ukaguzi linatokana na ukaguzi wa hesabu za mwaka 2009/2010 na 2010/2011.
(2) MADENI YA VYOMBO VYA HABARI
1. Clouds Entertainment Media Group 13,080,000.00 2. Radio Tumaini 424,800.00 3. ITV 3,778,360.00 4. Sahara Media Group Ltd 44,244,000.00 5. Sports Dream Co. Ltd 810,000.00 6. KIUTA 9,430,350.00 7. Colour Print 22,619,792.00 8. Business Times Ltd (Majira) 4,988,945.00 9. Habari Corporation 6,850,000.00 10. Mwananchi Communication Ltd 9,620,000.00 11. TSN 8,271,160.00 12. Guardian Ltd 11,702,160.00 13. TBC 7,687,360.00 14. Uhuru Publication Ltd 55,049,040.00 15. WAPO Radio 1,000,000.00 16. Zanzibar Leo 4,500,000.00
17. Raia Mwema 1,129,000.00 18. FTV Production 1,980,000.00
Jumla Tshs. 201,866,807.00