Walikubali Mchakato wa Katiba Mpya wakubali na Matokeo yake.

By Mwanakijiji

 

Hawazi watu kuamka sasa na kulalamika kuwa ati Bunge la Katiba litakuwa limejaza CCM na kuwa Katiba Mpya itakuwa ni ya CCM! Haiwezekeni watu wapate ufunuo leo hii baada ya kutangazwa kwa majina ya wabunge wa  Bunge la Katiba ati sasa wametambua kuwa Kikwete anawachezea akili ati kwa vile wameona majina ya makada na wana CCM maarufu kama kina Kingunge Ngombare Mwiru, Shamim Khan, Paul Kimiti, Sixtus Mapunda, na Dr. Zainab Gama nikiwataja wachache tu.

Kuna watu wanataka tuamini kuwa makundi yaliyogawanywa katika matangazo ya majina hayo watajadiliana kimakundi kwenye Bunge la Katiba; kwamba wakulima watakaa kama wakulima na kujadiliana, wavuvi kama wavuvi, wanasiasa kama wanasiasa n.k. Ukweli ni kuwa sheria ya Katiba Mpya haijaweka utaratibu wa mijadala ya Makundi au kulazimisha kupiga kura kwa makundi. Hivyo watu wasifikirie kuwa ati kwenye Bunge la Katiba makundi yataulizwa na kupiga kura ili kutoa msimamo wao kama kundi. Sheria inatoa uhuru wa maoni na mijadala kwenye Bunge la Katiba na hivyo wabunge hawa hawafungwi na utii au umoja wa makundi yao!

Lakini jambo ambalo liko wazi – na nililionesha miaka miwili iliyopita – ni kuwa Bunge litajaa watu wenye maslahi na CCM hasa kwa vile ‘magenius’ wetu walikubali kuwa wabunge wote na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa kutangazwa kwa majina haya watu wenye maslahi na CCM au ambao wamewahi kushika nafasi za uongozi ndani ya CCM wanaunda kundi kubwa zaidi (super majority) kwenye Bunge hili. Hili si jambo la bahati mbaya; siyo jambo ambalo linakuja tu hivi hivi na ukiangalia kwa karibu utaona kuwa ni jambo ambalo litahakikisha kuwa kile ambacho CCM wanataka wanakipata.

Sasa wapo waliokubali mchakato huu mbovu wa kuandika Katiba Mpya; walikubali kwa sababu waliamini – kwa makosa – kuwa utakuwa ni wa haki, wa wazi na ambao utawapa nguvu wananchi. Badala yake walikubali kumpa Rais wa JMT na Rais wa Zanzibar nguvu kubwa sana. Hivi kulikuwa na ubaya gani kwa taasisi kutaja wajumbe wake wa Katiba (wachaguliwe kwenye taasisi hizo kwa uhuru) badala ya kuachiwa Rais kuamua? Matokeo yake wapo baadhi ya wabunge hawa ambao wanamshukuru Rais leo hii kwa “kuwakumbuka” kwani wengine nyota zao za kisiasa zilishafifia!

Tulisema huu ni mchakato mbaya; na kama watu wanafikiri wameshaona ubaya wake wangoje mijadala ya Bunge hili itakavyoanza. Binafsi nitawakatalia wapinzani wakianza kulalamika kuwa wanaburuzwa au kuwa hawana imani na mchakato au na Rais! Hilo litakuwa ni kigeugeu kilichopitiliza! Yote ambayo yatatokea wapinzani wanajua na walishajulishwa na wakakaza shingo zao kuukumbatia mchakato huu haramu (ni haramu kwa sababu umevunja Katiba ya sasa).

Nitaendelea kuukataa na japo ninatamani sana kuona Tanzania inakuwa na Katiba Mpya nzuri na inayotokana na wananchi naamini kuwa mchakato huu hadi hivi sasa umewanyima Watanzania haki hiyo. Walioukumbatia toka mwanzo, wakatoa maoni na kutoa wajumbe na kukubali kuwa ni halali wasigeuke sasa; wametikisa dawa, sasa wainywe; wasiseme “chungu

By Yericko Nyerere

Leave a comment