By: Yericko Nyerere
Nataka kuzungumza dhana ngumu kidogo machoni pawengi, lakini hima nitaeleweka bila mawaa wala chembe ya makunyanzi. Nazungumza kama mtaalamu wa mifumo ya kiulinzi duniani hasa nikiangaza mifumo ya kiusalama ya Franks Secur, Westm secur, Latino secur, Kremlin secur.
Siasa tuiache kando utaalam uchukue nafasi yake, na hapa nataka tujikite kuuangalia mfumo wa utendaji kazi wa idara ya Usalama wa Taifa na vyombo saidizi vyake katika kulitumikia taifa la Tanzania chini ya Westm secur
Usalama wa Taifa Tanzania ni idara iliyochini ya Ofisi ya Rais, hii inamaana kuwa mkuu wa idara hii anaripoti kwa rais mojakwamoja, pia mkuu wa idara hii huteuliwa na rais kwakuzingatia vetting maalumu iliyochini ya command ya ndani.
Muundo wa utendaji wa idara hii umegawanyika katika sehemu kuu sita, ambazo ni idara ndogondogo ndani ya idara hiyo kubwa nazo ni idara ya mambo ya ndani, idara ya siasa, idara ya mambo ya nje, idara ya ichumi, idara ya ukusanyaji taarifa, idara ya uchakataji taarifa na idara ya vita.
Hapa nataka kuzungumzia idara ya siasa ambayo ndio tunayokumbana nayo mtaani kila kukicha na tunashirikiana katika maandamano nk,
Idara hii nayo ina vitengo mhimu vya kiutendaji ikiwemo ulinzi wa chama na serokali, sera za kisiasa na muundo wa siasa kutegemeana na chama kilichopo madarakani wakati huo.
Pia idara hii inajukumu la kufuatilia na kutambua mienendo ya wanasiasa viongozi na wale wote watu maarufu katika taifa, bila kusahsu kufuatilia mawasiliano yao, baruapepe zao, mizunguko yao ya kila siku, vyakula vyao vya kila siku, vipato vyao nk.
Idara hii pia imepewa jukumu la kuwalinda viongozi wa kisiasa (mawaziri na wabunge) kwa saa 24 bila kukoma. Mfano, Rais hulindwa na watu 40 wanaoonekana na 48 wasioonekana, hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def S2).zingatia kukiwa na hali ya hatari (Def Cond) kiwango cha ulinzi huongezeka.
Makamu wa Rais hulindwa na watu 15 wanaoonekana na 10 wasioonekana, hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def S2).zingatia kukiwa na hali ya hatari (Def Cond) kiwango cha ulinzi huongezeka
Waziri mkuu hulindwa na watu 15 wanaoonekana na 8 wasionekana hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def S2) zingatia kukiwa na hali ya hatari kiwango cha ulinzi huongezeka.
Mawaziri hulindwa na watu 3 wanaoonekana, na 5 wasioonekana, hiki ni kiwango cha juu cha ulinzi (Def s2).
Majukumu ya walinzi wanaooneka na wasioonekana yanatofautiana na kila mtu kati yao huripoti kwa boss wake,
Wale walinzi wanaoonekana huripoti kwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, na wale wasioonekana huripoti kwa rais kila mmoja kwa wakati wake bila wao kujuana.
Hii inamaana kuwa kila anachotaka kufanya ama anachofanya waziri yoyote kabla hajakitenda basi taarifa huwa mikononi mwa rais na mkurugenzi wa Usalama nchini.
Wale wanaoonekana wanaomlinda Rais huripoti kwa mkurugenzi na mnadhimu, wale wasioonekana 10 huripoti kwa rais moja kwa moja, na 30 huripoti pande zote tatu lakini kwa umakini mkubwa bila kujuana.
Mpendwa msomaji, sio nia yangu kusafisha wanasiasa, bali nia yangu nikukuelezeni kitaalamu mfumu wa ulinzi nchini unavyoendeshwa na madhari ya kisiasa kuwa waziri fulani ni mwizi ama fisadi kwa dhana ileile ya kisiasa.
Kwenye medani ya siasa huko kuna filosi tofauti kidogo ambayo hutafsiri uwajibikaji kisiasa katika dhana inayokinzana na uhalisia wa kiutaalam katika mifumo ya kiulinzi.
Hapo sijazungumzia intelligence ya jeshi la polisi ambayo nayo ni mdau, pia sijaigusa Tanzanian Military Intelligence ambayo ndio mwamuzi wa mwisho katika muktadha wa taifa hili..
“Kuna watu wasipokuelewa maneno na matendo yako, mshukuru Jah, wewe bado unafikra chanya, wakianza kukuelewa jichunguze ni wapi umeanguka maana umeanza kuwaza kama wao