Kuelekea uchaguzi mkuu 25/10/2015, makada hawa wapo hatarini

By. Martin Madafa

HALI ya kisiasa ni mbaya kwa sasa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika wiki mbili zijazo yaani 25/10/2015, viashiria vya uvunjifu wa amani vimejikita ndani ya chama cha mapinduzi kwa ubia wa vyombo vya dola nchini., Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinasema makada wa UKAWA John Mrema, Yericko Nyerere na Reginalnd Munisi kwa zaidi ya mwezi sasa wanawindwa na vyombo vya dola kwa siri kubwa kwa shinikizo la kisiasa (ccm). Makada hao ndio wanaoongoza idara ya mikakati ya ushindi ya ukawa.

Taarifa hizi zinakaziwa na kutoweka kwa kada wa Chadema Yericko Nyerere, Tangu siku ya jumatatu ya tarehe 15/9/2015, Yericko hajaoneka hadharani wala kwenye mitandao yakijamii jambo linalozusha wasiwasi mkubwa hasa kwa vijana ambao niwafuasi wake mitandaoni na katika siasa nchini, simu zake zote 0755865544 na 0715865544 zote hazipatikani, pia taarifa za kuaminika toka kwa majirani zake huko kigamboni zinasema nyumba yake imetelekezwa.

Katika ukurasa wake wa facebook tarehe 16/9/2015 Yericko aliandika kuwa “Jeshi la polisi jana usiku limefanya uvamizi nyumbani kwangu, kwa bahati mbaya mimi sikuwepo, lakini kiongozi wa uvamizi huo aliponipigia simu alisema wanahitaji kuchukua maelezo yangu, Wiki mbili zilizopita alinipigia simu ZCO Mr Mbuta, akaoomba kuonana na mimi, nilimuuliza ni mazungumzo ya kawaida au ya kiofisi? Akajibu ni yetu ya kawaida tu, ieleweke kuwa ninafahamiana na huyu Mh na nimarafiki, hivyo kwakuwa nipo kwenye kampeni nilimweleza kywa nikimaliza kampeni nitakuja mh, Lakini kumbe nyuma ya pazia kulikuwa na hili, Ushauri wangu, jeshi la polisi liache kutumika kisiasa”, Hii inaonyesha Yericko anamahusiano ya karibu na vigogo wa hao wa dola nchini, kama anafahamiana nao, ilikuwaje avamiwe usiku na wavamizi wakajitambulisha wametumwa toka ikulu? Kuna utata mkubwa juu ya hili.

Taarifa toka ndani ya ccm zinasema kuwa vigogo wa chama hicho kuna nyaraka muhimu za MKAKATI ya USHINDI wa UKAWA wanazozitafuta kwa mda mrefu sana, sasa kupitia kwa aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema Dr Slaa ambae kwa sasa ni mpiga kampeni wa Magufuli, aliwadokeza kuwa wakitaka kuipata nyaraka hiyo wamuone Yericko ndie aliyeandaa, inatajwa kuwa tayari walishatumia mbinu nyingi ikiwemo kujaribu kumshawishi kupitia kwa marafiki zake lakini kijana huyo alionyesha kukataa. Inaelezwa kuwa mswada wa mkakati huo awali alikabidhiwa Dr Slaa kabla hajajiuziru na kuasi chama hicho,

Kada wa ccm ambaye hakutaka kutajwa anasema, “Dr ametueleza kuwa mkakati huo aliupokea kutoka kwa mwandaaji (Yericko) akaenda nao nyumbani , baada ya siku chache akajiuzuru ukatibu. Anazidi kusema kuwa baada tu ya kujiuzuru Dr alizima simu zake zote na akawa na namba mpya ambayo alikuwa akiwasiliana na mshauri wake Yericko Nyerere tu kwa zaidi ya siku tatu. Nikipindi hicho ndicho Yericko alikutana na Dr nyumbani kwake aliuchomoa mkakati huo hali iliyopelekea Dr kukosa nyaraka yoyote mhimu yakuwavuruga ukawa”, Inasadikiwa kuwa hata Mwenyekiti Mh Mbowe alilazimika kuwasiliana na Dr Slaa kupitia kwa Yericko katika kipindi kile cha mgogoro.

Viongozi wa Chadema hakuna aliyepatikana na kulizungumzia kwa undani hili, lakini Mh Mbowe alipoulizwa alisema, “tunatambua hila zote dhidi ya watu wetu, tunalionya jeshi lapolisi na ccm kuheshimu uhuru, haki ya mtu kuishi na kufikiri” simu yake ikakatwa na alipopigiwa tena hakupokea. Mtandao huu umeweza kuona mkakati huo wenyekichwa kisemacho “THE PEOPLES’ AMANDLA ELECTORAL VICTORY THE ROAD TOWARDS IKULU” unaonyesha umeandikwa na Yericko Nyerere ukiwa na kurasa 150 kwa lugha ya Kiswahili na kiingereza.

By Yericko Nyerere