Lowassa hawezi kuwa rais wa nchi hii labda katika njozi,

Edward Lowassa amegeuzwa mradi wa watu kujichumia pesa kwa tafsiri ya lugha ya kimjini ni kwamba amefanywa buzi la baadhi ya watu wenye njaa AMA kuendekeza njaa na kumdanganya mzee huyu kwamba anafaa kuwa rais yalaiti wakiujua ukweli kabisa kwamba Lowassa haweZi kuwa rais wa nchi hii labda katika njozi,baadhi ya wanasiasa,

Kikundi kimoja ndani ya umoja wa Vijana wa ccm wakiongozwa na bashe, kundi la wafanyabiashara ambalo walinufaika Wakati Lowassa akiwa Waziri mkuu, kundi linalojiita friends of Lowassa,baadhi ya blogs na magazeti kadhaa na vyombo kadhaa vya habari na baadhi ya watu humu ndani ya jamii forum wakuwa wakitumika vibaya kwa kupewa pesa na mzee Lowassa kazi Yao kubwa ni kuimba Wimbo wa lowassa anafaa kuwa rais 2015.

 

 La hasha wanamlia pesa mzee huyu ambae ata familia yake na haswaa mkewe wamekuwa wakimtaadharisha na wachumia tumbo hawa ambao wanajua hali ya afya ya Lowassa ni tete kwa sasa
 Huu hapa sasa ndio ukweli mtupu wa kwanini Lowassa hawezi kuwa rais wa nchi hii na Jambo ambalo limepelekea kwa kiasi kikubwa mkewe kumkataza na kumwambia mzee apumzike

 

 1. Habari za ndani na za uhakika ni kwamba mzee huyu baada ya kufanyiwa operation ya mgongo madaktari wake ujerumani walimshauri asijishugulishe na siasa ata za jimboni kwake na badala yake atumie muda mwingi sana kupumzika, kinachotokea sasa- Lowassa hawezi kukaa kwenye kiti vizuri na anakalia upande mmoja AMA kushoto au kulia na hawezi kusimama kwa muda mrefu pia,huyo ndio wachumia tumbo wanamwita rais.

 

 2.kutokana na matumizi ya pombe kali na haswa alipojiuzuru kwa kashfa ya ufisadi ambayo mpaka Leo hakuna chombo chochote cha kiserikali ambacho kimesema hakuusika na kumsafisha hadi Leo hii Lowassa sasa amepatwa na ugonjwa wa kutetemeka mikono na hawezi kuandika si kwa kutumia Kalamu au ata kujibu MSG kazi inayofanywa na wapambe kwa sasa huyo ndio wanaemwita rais 2015

 

 3. Lowassa pia amepoteza uwezo wa kuona, haoni zaidi ya mita 5 na ata Kama anakusalimu ni mpaka uwe karibu nae Kama anakuja ndipo atajua nimekutana na Fulani,ukiwa nae karibu angalia jicho lake la kushoto utagundua kwamba limeshuka chini na kufumba na kufunguka kila baada ya sekunde kadhaa baada ya operation pia ya jicho, wote tunajua siri ya mgonjwa ni ya daktari lakini hizi ni za kifamilia zaidi maana Kama ndugu lazima mjue anaumwa nini na kwakua tunataka rais ni vyema tukajua tunapata rais wa aina gani maana kiongozi ni kioo..huyo ndio Lowassa mnaeimbiwa Wimbo na wachumia tumbo Huku haya yote wanayajua.

 

 Walipokuwa monduli hivi majuzi Wakati wachumia tumbo hawa walipokwenda kumuunga mkono kwa safari yake ya kusadikika alisikikika kanisani akitoa kauli hii namnukuu, mke wangu najua umekua ukinitaka nipumzike lakini watu hawa wananiitaji sana kujenga taifa hili nami sitowaangusha, nisamehe mke wangu Kama nitakukwaza. Mwisho wa kumnukuu.

 

 Ndugu Zangu watanzania nchi hii tuko mil 45 hivi kwanini awa watu wanalazimisha kubeba gari bovu na Magari mazima yamejaa katika nchi hii? Kwa pesa na si utu? Najua Kama ingekuwa kununua ujana inawezekana Leo hii Lowassa angeununua ata kwa mabillion ya pesa tena za wale wanaojiita marafiki zake ambao aliwapa Dili akiwa Waziri mkuu sasa wanataka kuuza nchi kabisa apate urais japo ata kwa mwaka mmoja maana wanaijua vyema afya ya Lowassa kwa sasa, 

 

Ni ukweli usiopingika Lowassa alikuwa mchapakazi, mtu wa maamuzi magumu enzi hizo ana nguvu, uwezo mkubwa na afya imara: urais si kazi ndogo, kusafiri vijijini, wilayani, mikoani ndani na nje ya nchi sasa kwa hali ya mzee huyu je wanamnadi kwa historia ya utendaji wake au uhalisia wa sasa? Hoja kwangu hapa ni afya ya Lowassa inamnyima nafasi ya kutumikia nchi hii kwa sasa.., mzee pumzika na shtuka na hawa wanaokufanya wewe mradi.

 

 Sidhani pia CCM nao wanaweza beba mzigo Kama huu kiafya katika kampeni za kuzunguka nchi nzima lakini wakijua fika tutawauliza alisafishwa na nani na lini katika kuhusika na ufisadi.. Pumzika kwa amani mzee kabla hawajakuua na presha hawa wachumia tumbo wanaokufanya mradi.
 Mungu ibaraki Tanzania.

By Yericko Nyerere

Leave a comment