Chadema sumbawanga mjini yakanusha upotoshaji uliofanywa na stella manyanya na ccm mkoa wa rukwa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Sumbwanga mjini kimekanusha upotoshaji uliofanywa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa bw Matete kuwa bw Godfrey Shayo iliyekihama Chama hicho na kujiunga na CCM  alikuwa mwenyekiti wa CHADEMA wilaya.

Taarifa za uhakika toka ofisi ya CHADEMA Sumbawanga mjini ni kuwa bw Shayo alishawahi kushika wadhifa wa mwenyekiti wa baraza la Vijana “BAVICHA” Sumbawanga mjini tena siyo wilaya nzima ya Sumbawanga kwani wilaya ya Sumbawanga ina wenyeviti wawili wa BAVICHA akiwepo wa Sumbawanga mjini na Sumbawanga vijijini.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa katika kipindi cha uongozi wa bw Shayo kama mwenyekiti wa BAVICHA Sumbawanga mjini alibainika kuwa mdanganyifu  kwa kutumia mamlaka yake kuchangisha pesa toka kwa wafadhiri na kuzichakachua. Kwa mjibu wa Katibu wa CHADEMA wilaya bw Kasikila upo ushahidi uliyomtia bw Shayo hatiani wa kuchangisha kiasi cha Tsh 48,000/ na kuzitafuna, ni kwa ubadhirifu huo ndo kikao rasmi cha BAVICHA Sumbawanga mjini cha  tarehe 16/07/2011 kiliamua kwa manufaa ya chama na kwa kauli moja kumvua uongozi bw Shayo baada ya kupoteza sifa za kuwa kiongozi. Mhutasari wa kikao cha kutokuwa na Imani na Bw Shayo.

Tazama kiambatanisho nimeambatanisha na makala hii. Katika  hafla kubwa yenye sura ya kimkoa iliyoandaliwa na CCM Mkoa wa Rukwa  kwa ajili ya kumkaribisha bw Shayo CCM na kurushwa na Sumbwanga Tv, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa bw Matete alikaririwa akitamka kwa ujasiri mkubwa kuwa bw Shayo ametokea CHADEMA kama mwenyekiti wa wilaya na kuongezea kuwa zaidi ya kuwa mwenyekiti wa wilaya Sumbawanga pia alikuwa akiongoza wilaya ya Nkasi kwa wadhifa huo huo,

Taarifa sahihi ni kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Sumbwanga ni bw Godfrey Katata, na mwenyekiti wa sasa wa BAVICHA tangu tar 18/07/2011 ni bw Conwell Kakwaya, kwa mjibu wa mjumbe wa Baraza la vijana CHADEMA taifa mkoa wa Rukwa bw Frank Joseph Fumpa huu ni upotoshaji wa hali ya juu kwani bw Shayo baada ya kuvuliwa uongozi alibaki akitapatapa mara baada ya kukosa platform CHADEMA na kwa maana hiyo ndiyo maana akaona ni bora ahamie CCM, rekodi sahihi ni kuwa bw Shayo amehamia CCM kama mwanachama wa kawaida wa CHADEMA tena mwanachama mwenye doa au kovu la utaperi.

CCM wanapongezwa kwa kuandaa hafla kubwa iliyohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyaya, wakuu wa wilaya, wabunge, watendaji wakuu wa mkoa, na halmashauri zote za mkoa, (Mpanda, Nkasi, Sumbawanga vijiji na Manispaa) kwa ajili ya kumkaribisha bw Shayo, lakini wajue si sahihi sana kufanya hivyo kwa sasa kwani kutokana na hali mbaya ya maisha wanayokabiliwa wanarukwa ni fedheha kwa CCM na Serikali kwa ujumla. Ikumbukwe kuwa mkoa wa Rukwa una wenyeji wanaotegemea kilimo lakini kwa sasa pamoja na kuwepo na sera ya kilimo kwanza wakulima wanashindwa kununua pembejeo, kwa sasa mfuko wa mbolea Sumbwanga ni  50 elfu @ kilo 50 (mbolea ya Ruzuku) na mbolea y a kuuzwa tu kwa kawada ni shilingi 82 elfu hadi 90 elfu, barabara ni mbovu hazitumiki kwasasa, mafuta ni shida siku ya x mas lita moja ya mafuta ya petroli ilifikia shilingi elfu 7.

Namuomba Stella Manyanya ayafanyie kazi haya na si propaganda za kisiasa, ni vema kama ana nia ya kuendeleza mkoa hizo awaachie wakina Tambwe Hiza      CHADEMA Sumbawanga mjini imekanusha pia upotoshaji mwingine kuwa bw Shayo ameihama CHADEMA eti kwa sababu ya ukabila na udini, upotoshaji huo unajibainisha kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, viongozi wa madhehebu ya kikristo walijiingiza katika kampeni makanisani kwa kumpinga mgombea wa CCM bw AESHI kwa kuwa ni muumini wa kiislam, hoja hii inahitimishwa kwa kusema kuwa CHADEMA Sumbwanga ni chama cha wakristo, Hoja hii si sahihi na kwamba udini Sumbwanga mjini haupo kwa vyama vyote viwili yaani CCM na CHADEMA.

Chachu ya udini Sumbawanga iliingizwa kwa wapiga kura katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana na viongozi wa kampeni wa CCM bw Matete( mwenyekiti CCM mkoa),bw  Tung’ombe (katibu mwenezi wilaya), bw Aeshi (mgombea wa ubunge), na wengineo. Hali ilikuwa mbaya sana pale bw Aeshi mgombea wa ubunge CCM alipoishiwa sera kwa wapiga kura na kujinadi katika mikutano kadhaa ya hadhara yeye kama YESU, na kumwita Kikwete MUNGU na Madiwani ROHO MTAKATIFU, jambo hili lilionekana kama fedheha na dharau kubwa kwa wakristo, kanisa katoriki lilitoa onyo kali kwa bw Aeshi na kutoa ujumbe wa kuombwa msamaha kwa dharau hiyo, jambo ambalo halikuwezekana, hali iliendelea kuharibiwa zaidi pale bw Matete kutumia advantage ya yeye kusoma seminari na mapadre wa kikatoriki na kuwa karibu nao kwa muda na kutumia mikutano ya kampeni kuwaita mapadre wahuni na wazinzi na kuwa yeye anawafahamu vizuri.

Kauli hizi alizipata mh Pinda na kuwaamuru wahusika waombe msamaha kwa makanisa, kwa bahati mbaya hawa kufanya hivyo.     Mh Pinda aliamua mwenyewe kuja Sumbawanga kuongea na viongozi wa dini wa kikristo kadhaa na kuamua mwenyewe kuapanda jukwaani katika uwanja wa Rukwa high school na kueleza yote kwa kujaribu kumtetea bw Aeshi kwa kusema alikuwa alijaribu kuomba kura kwa kutumia mafiga matatu akajisahau akatamka YESU,MUNGU na ROHO MTAKATIFU, lakini Pinda alikiri kuwa ni kosa kubwa na hasa kwa Aeshi ambaye si dhehebu hilo, mwishowe mh Pinda aliomba msamaha kwa niaba ya CCM na wote waliohusika.Mh Pinda aliondoka, lakini bado wahusika hawakukoma na hadi sasa kama ilivyoelezwa na bw Shayo bado hoja hii iko katika kauli za viongozi wa CCM mkoa.

CHADEMA Sumbawanga mjini inatamka kuwa  haihusiki kwa hili  la udini, CHADEMA iko imara na itaendelea kuwa imara zaidi Sumbawanga mjini.

By Yericko Nyerere

Ehud Barak katufananisha na Tripolitania (nchi isiyoexist)

Honorary consul: Barak belittled Tanzania

Kasbian Nuriel Chirich says that in trying to stress importance of key euroepean countries to Israel, defense minister made disparaging remark on African count

Addressing the Foreign Ministry’s response to harsh criticism leveled by European Union members of the UN Security Council over Israel’s settlement construction in the West Bank, the Israeli defense minister said “Germany, France and Britain are not Tanzania, Mauritania or Tripolitania. These are very important countries in the world and we have no interest in increasing the tensions with them.”

 

 

 

'Vast country's wonders.' (Photo: Omri Wendel)
‘Vast country’s wonders.’ (Photo: Omri Wendel)

 

 

In an official letter to Foreign Minister Avigdor Lieberman, the consul, Kasbian Nuriel Chirich, said “on behalf of the Republic of Tanzania I wish to express regret over the comments made by Defense Minister Ehud Barak, who, in an attempt to (emphasize) the importance of key European countries, chose to belittle Tanzania and even compare it to a country that does not exist.”

 

 

Chirich stressed that Tanzania was the largest country in east Africa with a population of 46 million. He said Israel and Tanzania maintain extensive financial, diplomatic and security relations which go back to the early 1960s, when the African nation gained its independence.

 

 

“I would be glad if an official Israeli representative accompany on my next visit to Tanzania in January so that he will be able to experience the wonders of this vast country and its peace-seeking people,” the honorary consul said.

 

Kwa msaada wa mtandao wa  http://www.ynetnews.com/articles/0,7340,L-4166711,00.html

By Yericko Nyerere

Mbinu muhimu kwa Chadema strategist kuelekea Magogoni kwa ridhaa ya Watanzania.

Baada ya kumalizia sherehe za xmass za maubwabwa na mapilau, sasa narudi katika harakati za ukombozi wa Tanzania toka kwa mkoloni mweusi anaefanana kwa kila kitu na mzungu yule wa miaka ya 1945, kasoro huyu ni mweusi tu mwenye kutumia magwanda ya kijana akibaka uchumi na rasilimali za urithi wa Tanzania.

Naomba niwakumbushe wanamikakati ya kisiasa (political strategists) wa chadema juu ya hili.

Chama chochote cha kisiasa kinacholenga kuchuku uongozi wa dola lazima kipitie hatua kuu mbili za kimkakati katika ukuaji

 (1)unity of opposition

Hii ni hatua ya kwanza ya kimkakati katika ukuaji wa chama,ambayo chama kinajipambanua kama chama halali cha upinzani (legitimate political oppostion) pia kinatumia muda mwingi katika hatua hii kupinga sera,maamzi na mambo mbalimbali yanayofanywa na chama tawala,hii ikiwa na lengo la kupata public attention na kutengeneza political base na zaidi kupata wawakili shi (wabunge) zaidi bungeni na kua kambia rasimi ya upinzani (chadema imepitia hatua hii).

Na mnaweza kulifanya hili kwa kuchagua agenda mmoja kuu ya kukitambulisha chama chenu na kuvutia wanachama na kujipambanua kama chama cha upinzani (chadema ilifanya hili kwa kuchagua vita zidi ya ufisadi/mafisadi na ruswa kama ajenda yake kubwa)katika hatua hii kinachowaunganisha ni upinzani wenu kwa chama tawala (unity of opposition),lakini hatua hii tu haiwezi kukifanya chama kupata uungwaji mkono wa kutosha  ili kupata uongozi wa dola.

(2)unity of construction

Hii ni hatua ya pili ya kimkakati ambayo ndio inakiiandaa chama kuchukua uongozi wa dola.katika hatua hii nguvu kubwa inawekwa katika kuuza sera mbadala kwa wananchi,na zaidi kueleza mtawafanyia nini wananchi katika nyanda zote afya,elimu,ajira nk,na pia mnaaenda mbali zaidi kutekeleza kwa vitendo kwa wananchi baadhi ya mambo ambayo yako ndani ya uwezo wenu.Katika hatua hii,mnaonesha majibu saidi kwa matatizo ya wananchi na sio kutumia muda mwingi kukosoa chama tawala kimekosea nini bila kuonesha majibu mbadala:

Angalizo kwa chadema:

Mimi naamini chama cha chadema kimeshapita katika hatua ya kwanza ya ukuaji (unity of opposition) na kinatakiwa kwenda hatua ya pili sasa (unity of construction),hii itafanya chama kijiweke wazi zaidi kwa wananchi walio wengi na kuonesha nini tofauti yake ya kisera katika nyanda zote ukilinganisha na chama tawala (ccm).

Hii itajenga kuaminika kwa chama,pia kuonesha wapiga kura kwamaba chama sasa kimeiva na kikotayari kuchukua dola. Vyama vingi vya upinzani vinafanya kosa la kubaki katika hatua ya kwanza tu ya ukuaji,hii haiwezi kukifanya chama kishinde na kupata dola,kitaishia kupata wabunge tu!,inakifanya chama kieendelee kuonekana mbele ya umma kama chama cha upinzani tu,na sio chama kinachoweza kuchukua dola! Strategist wa chadema liangalie hili,msisubili kuuza ilani ya uchaguzi 2015 mkategemea ndani ya kampeni mtajijengea uhalali wa kutosha kuonekana mbele ya wapiga kura kama  chama dola.

Onesheni chama tawala kimeshindwa tayari na ni adui dhaifu,nendeni katika hatu ya pili ya ukuwaji (unity of construction) itawapa nafsai ya kuuza zaidi sera zenu kwa wananchi na sio kutumia muda wote kuuza agenda mmoja(ufisadi) na kuipinga serikali tu,wakati ni huu wa kutoka kuwa chama cha upinzani kwenda kuwa chama chenye kujiaanda kushika dola.

Na hata ikitokea chama kikapata uongozi wa dola moja kwa mmoja bila kupitia hatua ya pili ya ukuwaji,hakitakua na manufaa na kitapoteza umaarufu wake mapema,kwani wananchi wanakua hawajui hasa kwa undani sera za chama hichi,na nini hasa kinalenga kuwafanyia wananchi kama kipaumbele katika kutatua matatizo yao!

Kwani mara nyingi chama kinapewa madaraka kwa imani kitatatua matatizo yote kwa wakati mmoja.

Hili ndilo lililokikuta chama kipya cha democratic cha japan,ilibidi waachie madaraka baada ya miezi mitatu tu ya kushika dola. Politica strategist

CDM inavijana wasomi na werevu ktk nyanja ya siasa mtambuka za kisasa, ninaamini toka moyoni mwangu mtalifanyia kazi ili kulikomboa taifa lililotopea kuzimu!

Sioni haya mbele ya CDM kutoa usaidizi wenye mafaa  kwa kizazi cha sasa na kijacho cha watanzania wote!

Mungu ni bariki mimi Yericko Yohanesy Nyerere,  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CDM

By Yericko Nyerere

Mzungu afukuzwa kwa ufedhuli na kuwadharau Waafrika, apewa saa 48!

Angalizo: Tokeo hili lilichapishwa kwenye gazeti la Mwafrika 1962. Mwafrika, Jumatatu Oktoba 29, 1962

MZUNGU mwingine ambae ni Meneja wa kampuni ya kuuza dawa, Arusha Bw. R. Bawley ameamriwa aihame Tanganyika, Mzungu huyo amepewa saa 48 tu kufanya hivyo.

Ripoti iliyopokelewa jana na gazeti hili ni kwamba Bwana Bawley alionekana akiondoka na matokaa kuelekea Kenya.

Sababu za kufukuzwa Mzungu huyo ni ufedhuli na kuwadharau Waafrika.

Mwandishi wetu akizungumza na na Regional Commissiner wa Jimbo la Kaskazini, Bwana P. Walwa jana alijulishwa kwamba jambo hilo alilihakikisha yeye mwenyewe alipofukuzwa na Meneja huyo.

Bwana Walwa alipata malalamiko kutoka kwa watu wengi kuhusu ufedhuli wa meneja huyo. Watu wengine walisema kwamba huwafukuza watu dukani kwake au kuwatupia fedha wakinunua vitu.

Bwana Walwa alikwenda katika duka hilo ili ahakikishe mwenyewe kabla ya kuchukua hatua na kwenda kufika Bawley akamwambia ‘nenda zako’. Hapo Bwana Walwa alitoka na kutoa habari hizi kwa polisi.

Radhi yakataliwa:

Asubuhi yake Meneja huyo alikwenda kuomba radhi akisema hakujua kuwa yule aliyemfukuza alikuwa Regional Commssioner.

Bwana Walwa alikataa kumsamehe kwa sababu, alisema ‘dharau ile ilifanyiwa Waafrika wote’. Bwana Walwa alimwambia mwandishi wetu hiyo jana kwamba yeye alitembelea jimbo lote akiwaonya watu waheshimiane. Aliona si haki wengine waachiwe kufanya dharau.

Bawley sasa ni Mzungu wa sita kuondolewa kwa visa kama hivyo tangu nchi hii ipate uhuru wake.

NIONAVYO:

Ukikisimuliwa nchi hii ilivyokua zamani na ilivyo sasa, ni masikitiko makubwa, nisawa na jua na mwezi.

Leo mzungungu anaua mwafrika kwa bastola huku serikali dharimu impa nyongeza ya muda wa uwekezaji chini ya upinde wa miaka mitano ya msamaha wa kodi!

Swali je hivi leo, ambapo viongozi wetu wanawakumbatia wawekezaji, kuna yeyote kati yao anayeweza kufikia maamuzi kama haya?

 

 

By Yericko Nyerere

Kafulila Hawezi kukata rufaa dunia, mpaka mbinguni kwa katiba ya NCCR na Katiba ya Tz

“”Mwanasheria wa NCCR Mageuzi, Dk Sengondo Mvungi alisema Kafulila hawezi kukata rufaa sehemu yoyote dhidi ya uamuzi wa kumfukuza uanachama kwa mujibu wa kanuni ya 7 (2) ya chama hicho.

Kanuni hiyo ya 7(2) ya nidhamu na usuluhishi sehemu ya (d) inaeleza kuwa, baada ya uamuzi wa mwisho kufanywa, kikao husika kitatoa maelekezo kwa kikao au vikao vya chini vyenye mamlaka ya kuchukua hatua au kutoa adhabu kwa kiongozi au mwanachama husika. Kipengele (f) kinasema uamuzi utakaofanywa kwa mujibu wa kupengele (d) utakuwa wa mwisho ila tu pale unapomhusu Mwenyekiti Taifa na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar) ambao uamuzi wa mwisho kuwahusu wao ni Mkutano Mkuu.

Kanuni hiyo hiyo sehemu ya 7(1) inaeleza, ‘’Mlalamikiwa au mhusika atakuwa na haki ya kukata rufaa kwenda kamati ya nidhamu na usuluhishi iliyo katika kikao cha ngazi ya juu zaidi ya kikao husika, na kamati hiyo itakuwa na uwezo sawa na ule wa kamati ya kwanza, ila tu haitapokea ushahidi mara ya pili’’.

MY NOTES:

Kwa katiba za ajabu kama hizi za NCCR; Je wana mageuzi tuna haki ya kuipa pressure serikali kushirikiana na wadau kuandika katiba mpya?Je Nape akianza kusema kabla ya kuiambia serikali ilete katiba mpya ingelikuwa vyema mngezisafisha zenu zilizooza!tutamjibu nn?

Kafulila alichaguliwa kwa kura maelfu kule Kigoma-Kusini lkn likely atapoteza Ubunge wake kwa kunyang’wanywa kadi na watu wasio zidi hata 100 waliokutana wakiwa na agenda ya kumtimua wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mbatia ambaye katiba imemfanya awe na nguvu kama ya Mungu-mtu!

Si hiyo tu, Je katiba ya Tanzania si  inatambua haki ya wananchi kumchagua kiongozi wanaemtaka? sasa katiba hiyohiyo inazidiwa na katiba za vyama vya siasa kimaamuzi juu ya kiongozi wa kuchaguliwa kwa kura.

 

Katiba ya NCCR kuhusu kufukuzana ni madudu matupu; Je kuna yeyote  anayo katiba ya vyama vikuu vya upinzani vya CHADEMA na CUF nione tofauti zao kwenye vipengele vya kufukuzana?

By Yericko Nyerere

Angalizo kwa CHADEMA juu ya Jimbo la Kigoma Kusini!

Kafulila amefukuzwa Uanachama NCCR wakati akipinga NCCR kutumiwa na CCM hoja ambayo iliungwa na Mbowe katk harakati za kukataa kuungana na Mbatia katika Umoja wa Vyama vya upinzani

Kule Kigoma Kusini Kafulila ana nguvu na katika mtandao wa Chama , Chadema na NCCR ndivyo vyenye Nguvu!!
Mgombea wa CHadema ni Mhindi anaitwa Hassanary na hakubaliki huku!!!

Mbinu Pekee ya CDM kushinda Uchaguzi huo ni kumushawishi Kafulila kama CCM walivyo mshawishi Rostam !!!

Endapo kafulila atarudi CDM , Kauli ya Mbowe kuwa Mbatia ni CCM -B itakuwa agenda ya uchaguzi na jimbo hilo litahamia CDM !!!
Pia Mkosamali anaweza kurejesha kadi ya Uanachama NCCR kwani alisema hataki kuona Mbatia anaendelea Kuwa Mwenyekiti !!!

Sasa hapa majimbo yote hayo mawili yanaweza kurudi CDM!!!
Ukweli uliopo ni kwamba Siasa za Nchi hii ni kwamba mtu yupo tayari kuitumikia CCM na kuuza wanyonge!!

Endapo CDM watashindwa kumuchukua Kafulila kule jimboni kura zinaweza kugawanyika kwa kuwa Mbatia amiengia Mkataba na CCM ili jimbo hilo linge CCM na yeye apate ubunge kupitia Afrika Mashariki!!

Vita hii ni ya kimutizamo!!!

 

By Yericko Nyerere

Rais Kikwete ateua mabalozi wapya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Mabalozi:-
*<
(i) Mhe. Phillip MARMO, ameteuliwa kuwa Balozi nchini CHINA. Kabla ya hapo Mhe. Marmo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.
(ii)************ Dkt. Deodorus B. KAMALA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini BELGIUM. Kabla ya hapo Mhe. Kamala alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
*
(iii)********** Dkt. Batilda S. BURIAN, ameteuliwa kuwa Balozi nchini KENYA. Kabla ya hapo Mhe. Dkt. Burian alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).
*
(iv)********** Dkt. Ladislaus C. KOMBA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini UGANDA. Kabla ya hapo Dkt. Komba alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.
*
(v)************ Bibi Shamim NYANDUGA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MSUMBIJI. Kabla ya hapo Bibi Nyanduga alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
*<
(vi)********** Bibi Grace J.E. MUJUMA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini ZAMBIA. Kabla ya hapo Bibi Mujuma alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda (Regional Co-operation), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
*
(vii)******* Bwana Mohamed H. HAMZA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MISRI. Kabla ya hapo Bwana Hamza alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, ZANZIBAR, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
*
(viii)***** Ndugu Ali A. SALEH, ameteuliwa kuwa Balozi nchini OMAN. Kabla ya hapo Bwana Saleh alikuwa Balozi Mdogo (Consul General) nchini Dubai.
*
2.******** Uteuzi huu unaanzia tarehe 12 Oktoba, 2011.* Wataapishwa tarehe***** 19 Desemba, 2011 saa 03.00 Asubuhi.
*

By Yericko Nyerere

Jinsi Bunge linavyotumia madaraka yake kuliibia Taifa via Tume ya Utumishi ya Bunge

 

 

Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Wabunge ya 1997 (siina uhakika kama imewahi kufanyiwa marekebisho)

Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge: (WAJUMBE WOTE NI WABUNGE)

(a) the Speaker, who shall be the Chairman,
(b) the Deputy Speaker, who shall be the Vice- Chairman;
(c) The Minister responsible for Parliamentary Affairs;
(d) five other members appointed by the National Assembly from amongst its Members.
(3) The Clerk shall be the Secretary of the Commission and shall be responsible for securing or facilitating the implementation of
all the decisions of the Commission

Wafanyakazi wengine wa Tume mishahara yao na marupurupu yao yanatakiwa yaendane na yale ya Tume ya Utumishi wa Umma – ukiondoa Katibu wa Tume

Ibara ya 7:

(2) In the performance of its
functions under this section, the Commission shall
ensure that the complementing, grading and pay of
staff in the Service are kept broadly in line with
those in the Civil Service, and that so far as
consistent with the requirements set by the
National Assembly, the other conditions of staff in
the Service are also kept broadly in line with those
in the Civil Service.
(3) The Commission shall ensure that,
the pensions and other similar terminal benefits of
staff in the service are kept in line with the
provisions of the main pension scheme of the Civil
Service, but shall not do so in the case of staff for
whom provision for such benefits was made under
another statutory scheme before they entered
service in the National Assembly.

Maamuzi yao yanaamuliwa na Bunge (mapendezo toka kwa wabunge yanaulizwa wabunge wote!) na wakipitisha fedha ni lazima zilipwe mara moja kwenye mfuko wa Bunge

Ibara ya 11: The moneys required from time to time for the purposes of this Act shall, when the estimates have
been approved by Parliament, be paid by the Treasury from the Consolidated Fund into the National Assembly Fund.

Ibara ya 12: Tume inaweza kubadilisha mapendekezo ya makadiridio yatakayoletwa na Katibu wa Bunge


Mgogoro na Ibara ya 13?

The Commission shall from time to time, Prepare and recommend to the President the rates of salaries, allowances and other remuneration to be paid to Members of Parliament.

Swali kuhusu Ibara ya 11, 12 na ile ya 13? Je Rais anahitaji kuridhia ongezo la mishahara ya wabunge kwa mujibu wa sheria? Napendekeza kwamba (kwa maoni yangu) RAis anapewa taarifa tu; sheria haimtaki kuridhia kwani uamuzi wa mwisho wa makadirio na maamuzi ya kulipa wabunge yanafanywa na Tume hiyo. Sheria haimtaki rais kuridhia mapendekezo hayo au chombo kingine chochote. Tunaweza kujadiliana juu ya use ya neno “recommend” but in light of Article 11 Spika Makinda yuko sahihi.

Kulinganisha na Tume nyingine za Utumishi?

NImejaribu kulinganisha japo kwa haraka haraka na tume nyingine za utumishi ili kuona kama kinachofanywa na Wabunge kinafanywa na tume hizo nyingine (walitungiwa sheria na Bunge!). Je, tume ya utumishi ya Walimu au ya Mahakama na hata tume ya Utumishi wa Umma ziko huru kama tume ya Utumishi wa Bunge kufanya wapendavyo kuhusu fedha za Watanzania? Where did we go wrong?

 

By Yericko Nyerere

Vita ya mamba wa Wili iliyoingiliwa na kenge wasiokuwa na uelekeo.

. Ilikuwa ni kunako asubuhi tulivu kijua cha mawio kinachomoza na mto ukiwa tulivu na upepo tulivu ukipepea ghafla bin vuu mto ukaanza kuchafuka kilichofanya mto kuchafuka ni ugomvi wa mamba wawili uliokuwa mkubwa kupita kiasi huku baadhi ya watu waliokuwa nchi kavu wakishuhudia ugomvi huo pasipo kujua sababu za mamba hao kugombana ghafla mamba mmoja aliyeonekana kushindwa akaamua kutoka ndani ya mto na kuja nchi kavu.

Akakaa kidogo nchi kavu na kushindwa kukaa nchi kavu na kuamua kurudi tena mtoni na mwishowe wakapatana na yule mamba mwenzie huku akiwa na hasira za kimoyomoyo za kutaka kulipiza kisasi na hatimaye akaamua kuwashika kenge masikio na kuwaambia kenge kuwa yule mamba mwingine ndiye anayewafanya kuwa masikini na wale kenge kutokana na njaa zao wakaamua kuingilia ugomvi wasioujua na mamba yule aliyepgwa mwanzo akaona bado haitoshi akaanza kumzushia na kuipakazia taasisi yake mambo meng ya uongo mara ooh ananibania hapigi ngoma zangu hv kutopigwa ngoma na clouds pekee ndo itakufanya upotee kwenye game?kwan kuna radio ngap?

E.a,radio1,kiss fm,magic,radio uhuru,passion,rfa,times,capital,classic!!!radio zote hzo zisifanye ngoma yako kuwa hit? Kama ngoma yako kali lazima itakuwa hit tu kwan hit nyingi huamuriwa na mashabiki ndio wanaopga simu redion,kutuma msg,e mail n.k. Sugu na vinega wake wanashndwa kutambua kuwa style zao ni old fashion,tangu sugu anaanza ku rap mwanzoni mwa miaka ya 90 hadi leo anatumia style yake ile ile hv haoni kuwa style ile imechuja?

Ebu mwangalie mwana fa wa ‘ingekuwa vp’ na mwangalie fa wa ‘yalaiti’ ni mwana fa wawili tofauti kabsa mwangalie fid q wa ‘dot com’ na mwangalie fid q wa ‘ngosha ze swaga don’ ni tofauti kabsa hapa namaansha kubadilika kwa style.Kuna siku nilimuuliza prof Jay kuwa anajua kwa nini ngoma zake mbili za mwisho yan ‘msilie’ na ‘kama ipo’ hazkufanya vzur?akanijibu kwa kunisikilizsha ngoma yake mpya ambayo inatarajia kutoka hv karibuni inayoitwa ‘kamili gado’ ngoma ile nilivoisikiliza nikamwambia vzuri kwa kubadilika.Na sio bongo tu hata marekani wasanii wote wasiobadilika wamepotea yuko wapi method man?twalib?red man?ja rule?black milk? na wengi tu wasiobadilika wameshapotea kwenye industry .

Vinega hawa wanashndwa kuelewa hiki kitu kinachoitwa Edu-tainment yan education+entertinment yani unaburudika zen unaelimika mimi nikimsikiliza sugu siburudiki hata kidogo bali naelimika tu,yan me nimetoka kazini nimechoka nipo kwenye foleni kubwa tu ya kurudi nyumbani alafu nimskilize sugu au sogy dog khaa!si ndo ntazidi kuongeza stress kwa nini nismsikilize Izo business naburudika huku naelimika pia.

Kama mziki wako ukiwa na radha+video kali lazima itakuwa hit tu,eti wanasema ruge anampendelea fa,hv yeye ruge ndiye aliyempa fa tunzo ya EA?au ruge ndo alimpeleka fa channel 0 awards?ukifanya video kali km za ay,fa au cpwaa hata clouds wasipozpga ztagongwa tu kwngne tu.Au ruge ndye anayepga video ya Ay MTV? Ebu nitajie ni kinega gani mwenye video kali itakayoweza kupgwa channel 0?sugu ana video gani yenye quality ya kuweza kujivunia?Je ana video hata ya Dola 5000?Jibu ni hapana.

Sugu huyu anachukua chuki zake binafsi na kuzpeleka bungeni ili kumchafua tu ruge,sugu huyu anachukua maneno ya mitaani na kuyapeleka bungeni!hv huyu ni mbunge makini kweli?alisema kuwa THT wamepewa nyumba na serikali!una ushahid gan wa hili kwel we ni mbunge makini?THT Ile nyumba ni wamepanga na wanalipa kodi kama kawaida usipeleke mambo na chuki zko binafsi bungeni bhana me nilidhani ataongelea kuhusu mauzo ya albamu ndpo wasanii wanaponyonywa sana,badala ya kuiomba serikali kushughurikia tatizo hlo kwa kuwa watapata kodi kwny mauzo hayo,au kufanya harakat kwa wanao ban cd,juke box,na cd fake!!.Me nina uhakika clouds haifanyi wasanii kuwa masikini bali wao ndio wanaowasaidia na kuwainua.

Vinega hawa ndio wanaopga show mbovu wasiokuwa na mawasiliano mazuri na Dj(speaking of experience kwa kuwa nshahudhuria show nying tu). Kama sogy bdo anapanga lakin diamond ana mjengo wake unaona tofauti hyo?sogy z old diamond z new product. Vinega hacheni kufuata mkumbo kwa njaa zenu na kuinglia ugomvi msioujua(Ambao mimi naujua cwezi kuuanka hapa jamvini,kwa kuwa upo kisheria zaid) ki undani na kutumiwa km chambo AMKENII yooI!!.Cha msingi cha gongeni ngoma kali,video kali na mjue kupga show lazma mtatajirika tu hata kama ngoma zenu hazipgwi clouds na mumuangalie sana sugu atawavuruga sana,na najua sugu utakuwa umeshanijua mimi ni nani kwa 7bu nilishawahi kukuambia na hatimaye pia ukaniita ni snitch yoo!..yoo!

Chanzo GT JF

By Yericko Nyerere

Wazee Kumi na Saba (17) Waliodai Uhuru waTanganyika

 Kwa kujua au kutokujua, kwa makusudi au kwa bahati mbaya kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana kuhusu hasa ni akina nani waliodai Uhuru wa Taifa letu Tanganyika.

Upotoshaji hauishii hapo tu bali hata dhana halisi ya Maadhimisho yenyewe,Leo wanasema nisherehe za Uhuru wa Tanzania Bara,

Hakuna nchi au taifa duniani linaloitwa  Tanzania Bara, halijapata kutokea na halitotokea katika uso wa dunia hii taifa au nchi iitwayo Tanzania Bara.

Muunganano wa Tanganyika na Zanziber ni mfano wa kuigwa duniani, hakuna muungano wenye hadhi kinadharia dunia kama huu,Kila aliye muamini wa amani duniani na aupiganie kuulinda na kuuhuisha uwe na mafaa kwa wa Tanzania

Lakini muungano unaomeza taifa lingine na kubaka fikra za Watanganyika huku ukipuliza kwa dhihaka Wazanzibar haufai, yatupasa tuuhuishe mapema kabla mbongo za wahafidhina hazijamka na kushuhudia hasira ya Mtanganyika chini ya uvuli wa fikra za ccm mfilisi.

Sihubiri KUUVUNJA muungano huu murua bali, nahubiri uwepo wa Tanganyika na Zanzibar zenye kuwajibika kwa watu wao na uwepo Tanzania yenye kujikita Kimuungano.

Suala hili ni kama halina mantiki ya mageuzi ya mstakabali wa Mtanganyika, lakini aliye Mtanganyika anatambua mafaa ya matokeo ya hili.

Zanzibar ni nchi, yenye mamlaka kamili ya ndani, ina KATIBA, ina rais, ina jeshi, ina mahakama, ina bunge, ina makamu wa rais na zaidi ina makamu wa pili wa rais.

Je Tanganyika ipo wapi????? ilikufa ili iweje???

Vita baridi ilishaisha tunaitaka nchi yetu ikiwa na mipaka ileile.

CCM wamekuwa na kapropaganda kakidikteta kwa mtu yeyote azungumzia Muungano, huitwa mchochezi na zaidi MUHAINI.  Ni faida gani ccm mnzopata kwenye aina ya muungano huu?

Mimi nashauri mfumo wa serikali TATU ndiyo suluhu ya manung’uniko ya wakaazi wa pande zote za muungano huu.


Mh. Rais Kikwete leo kaweka kila kitu hadharani kumbe ni wazee 17 kutoka pande zote za nchi yetu walishiriki kikamilifu kudai uhuru wetu kinyume na historia inavyopindishwa au kuaminishwa kwamba ni watu wa Kariakoo pekee walifanya hivyo.


Julius Kambarage Nyerere, Ali Sykes, Lameck Makaranga, Gosbert Milinga, Gelmandus Pacha, Joseph Kimalando, Japhet Kirilo, Abubakar Ilanga, Saadan Kandoro, Suleiman Kitwara, Kisunguta Kabara, Chewa Said Chewa, Dosa Aziz, Patrick Kunambi, Joseph Kasela Mbantu, John Rupia, Abdulah Sykes.

 

By Yericko Nyerere

Tatizo si posho, Tatizo ni wakwepa kodi wakubwa na taifa kutonufaika na rasilimali zetu

Nimeona maneno ya wamaharakati wengi ya kupingana na posho za wabunge mufilisi, mimi natambua wanamtazamo na mawazo yanayoweza kutofautiana na mimi au na watu wengine kwani huo ndio uhuru wa kufikiri.

Tanzania si taifa la kupambana vita kwenye posho za wafanyakazi wake, bali ni taifa linalotakiwa kufanya mapambano katika kudhibiti wakwepa kodi kwenye sekta ya madini, mawasiliano na wengine kama wahindi wanaotumia maduka ya jeshi kukwepa kodi kubwa sana.

kuwa mfanyakazi wa tanzania si kwamba ulipwe mafao dhaifu, na wafanyakazi wengine kama walimu wakipunjwa mishahara basi ni lazima watu wote wapunjwe mishahara na posho.

nadhani ningewaelewa wanaharakati kama wangepigania kwanza wafanyakazi wengine kama walimu wapate posho na mishahara mikubwa na kuimiza ukusanyaji wa kodi na taifa kunufaika na rasilimali zetu.

By Yericko Nyerere

Madhara Ya Chuki, Uhasidi Na Uadui (Falsafa Binasfi chini ya Mang’amuzi tata)


Mang’amuzi ni jambo lenye mafaa kwa dunia hii ya kizazi    hiki cha  nyoka.    

 

Leo nitajaribu kuelezea maradhi makubwa yanayo tusumbua wanadamu wengi kwenye nafsi zetu. Binadamu tunaye adui mkubwa kabisa ambaye tunaishi naye, tunatembea naye na tunalala naye na kushauriana naye kila kukicha. Adui huyu si mwingine ila nafsi zetu wenyewe, hii ni nafsi iliyojaa uadui uwovu na majivuno yakiambatana na kiburi na kutafuta kukomoana, pasipo sababu za maana. Hakuna tabia mbaya katika tabia za binadamu na yenye kuchukiwa kama tabia hii**.

Tabia hizi kama zikimea kwenye nafsi zetu basi uondoa mfungamano wa kirafiki na kindugu na hata majadiliano yetu hukosa busara na hikma kiasi cha kupelekea kwenye utengano na uhasama.

Mwenye hizi tabia usababisha kufungulia madirisha na milango ya kuchukiwa na watu. Japokuwa kila mtu anatarajia apendwe na aheshimiwe na wengine, ndivyo hivyo hivyo, mtu huyo anategemewa awapende na ahifadhi heshima za wengine pia. Na ajiepushe kabisa na kila jambo linalokwenda kinyume na maingiliano mazuri au yanaosababisha kuharibika kwa maelewano na wengine.

Naweza kuuhita ugonjwa huu kwa jina la maradhi ya kimaadili yanayompata mtu, maradhi haya ya chuki na uadui ni miongoni mwa maafa makubwa ya ufanisi na utulivu wa nafsi, yanaotokana na tabia mbaya ya hasira ya kushindwa katika medani ya kutafuta maisha au kushindwa kwako katika kile unachokitafuta katika kuboresha maisha yako, kiasi ya kuvuruga mtiririko wa fikra chanya na kupelekea kuvuruga uthabiti wa kiroho wa mtu. Huenda ni kutokana na sababu Fulani fulani za kukosea hapa na pale au kujaribu hiki na kile. Kushindwa uku umfanya muhusika kupata hamaki na kujichukia na kupelekea kuwachukia wale waliofanikiwa kimaisha, kiasi ya kwamba kwa wale wasio na uvumilivu uamua kuwasingizia mambo haya na yale wale wanao waona kuwa ni maadui zao. Kiasi ya kusahau kuwa kufanikiwa au kuto fanikia ni mipango yako tu kutokuwa mizuri au kwa kutaka kutumia njia ambazo si za kimaadili, kama vile wizi au utapeli.

Hamaki hizi ni ile chuki iliyojengeka muda mrefu kiasi cha kusababisha moto uliofunikwa chini ya majivu ambao unaweza kutoa cheche za chuki na uadui zitakazounguza na kuteketeza mazao ya ufanisi na utulivu wa nafsi yako.

Bila shaka kutozijali hisia za watu huleta matokeo mabaya ya kudharauliwa na wengine na kuonekana ni mtu duni usiyefaa katika jamii za watu wastaarabu na wasomi.

Kama vile ambavyo kusamehe kunaonyesha utukufu na umakini wa nafsi ya mtu pia kunaleta usalama na umoja na utulivu wa nafsi, vivyo hivyo, uadui na uhasama kunapelekea kuwa na, chuki ambayo uzaa chanzo cha mfarakano na ugomvi. Ingawa uhasama hufanywa ili kutuliza misukosuko ya ndani ya nafsi, lakini madhara anayopata mtu kwa kulipiza ubaya kwa ubaya huwa ni makubwa zaidi kuliko madhara anayopata kwa njia nyingine, kwani maudhi licha ya kuwa ni shida kuvumilia, mwisho wake uondoka, lakini uhasama unapoota mizizi huchoma moyo wa mtu kama miba ya sumu na humkera daima. Isitoshe, uadui hauwezi kuondoa ubaya. Bali hulipanua na kulichimba zaidi donda. Kwa kawaida, uhasama humfanya hasimu ajitetee zaidi na alipize kisasi zaidi, akitegemea kupata utulivu wa nafsi, kumbe ndio anajirimbikizia machungu ambayo umletea maradhi ya saratani ya akili na kupelekea kuwa na maamuzi yasiofaa na yaliojaa visasi na chuki.

Wakati mwingine matokeo ya uadui huwa machungu mno kwa kadiri kwamba huwa hayumkiniki kurekebisha uharibifu unaotokana nao. Huenda mtu katika umri wake wote akaungua moyoni mwake na akaitesa roho yake kutokana na kosa kubwa alilofanya la kuweka chuki. Kutotumia akili na kutofikiria matokeo mabaya ya kufanya ugomvi, akifikiria kwamba anamkomoa mtu kumbe anajikomoa mwenyewe. Maana kila binadamu ana kamusi ya maisha yake na kuna baadhi ya watu, hawana maneno kama vile ‘samehe au upendo‘ kabisa, bali kuna maneno kama vile ‘uadui, ugomvi, nitamkomoa, atajuta katika maisha, ataipatapata fresh‘ na mishabaha na minyambuliko yake ndiyo iliyojaa humo. Kinyongo na hasira kali hutumia nguvu zote katika kulipiza kisasi na kujenga chuki kati ya watu. Tabia ya kupandwa na hasira haraka huandalia uwanja wa chuki. Mtu mwenye moyo dhaifu na mwepesi wa kuhamaki havumilii kusikia akikosolewa au akichambuliwa hata kidogo. Kinyume chake, watu wenye nyoyo safi na madhubuti huchukulia kukosolewa na kuchambuliwa kwao kuwa ni fursa nzuri ya kujirekebisha.

Watu wengi wanashindwa kuelewa kwamba kushikwa na hasira sana ni dalili ya kutopevuka kiakili, kwani huenda mtu anayekosoa huwa hana nia ya kumtukana au kumdharau mwenzake mwenye moyo dhaifu na mwepesi wa kukasirika. Hata kama kitendo hicho kitaonekana ni cha kutukana na kudharau, lakini huenda hakukusudia hivyo. Kwa hivyo, hakuna haja ya kuudhika na kulalamika.

Uchambuzi uliokusudiwa kuudhi na kudharau, kama una ukweli na unaonyesha kosa lenyewe, basi huwa ni zinduo na funzo kwa mwenye akili badala ya kuwa chukio. Lakini uchambuzi usiokuwa na msingi na ukweli usitiwe maanani, kwani unatokana na husuda na ubaya. Kitendo cha kuchambua bila ya msingi wowote ni kitendo cha kitoto, kichuki na kiwivu chenye lengo la kujitukuza kwa kuwadharau wengine. Hata hivyo, tusikereke na watu kama hao, bali tuwafunike kwa shuka ya amani na upendo.

Moyo wa kuweka kisasi na kukomoana ni dalili ya unyonge wa nafsi. Na ni ishara ya maudhi na maonevu aliyoyapata mtu udogoni mwake aidha shuleni, mtaani kwake alipokuwa akiishi au aliyo yaona katika familia au wazazi wake. Mambo haya huweka athari mbaya na kinyongo katika moyo wake kwa kadiri kwamba nafsi yake husumbuliwa na aina moja ya chuki iliyotia fora. Kwa ufupi, kukomoana na kulipiza kisasi ni njia mojawapo wanayoitumia wenye kujihisi duni ili kufidia kushindwa kwao. Hutumia visingizio mbalimbali kuwakera wengine na utenda uhalifu wa hatari kulipiza kisasi kwa yale yaliomsibu alipokuwa mdogo, akitafuta kujifariji ukubwani kwa masahibu ya utotoni. Watu wa aina hii mara nyingi wanakuwa wamelelewa katika koo duni na wakapata vyeo au kusafiri nchi za mbali na kujiona kuwa wao ni bora, hivyo kupelekea kuwa wajeuri. Kwa njia hii hutaka kufidia uduni waliolelewa nao katika koo hizo. Na ujiona ni watu bora kuliko wengine, na hutaka kutumia uhasidi na ubinafsi wao kujitangazia ubora wao. Wengi wetu tunaweza kuwatambua watu wa aina hii miongoni mwetu.

Njia mojawapo ya kuishi kwa amani ni kuwa na utulivu wa moyo na kusahau mabaya ya watu uku ukuzingatia shabaha ya maisha kwa kujaribu au kujitahidi kuishi kwa roho safi na huyapuuza mabaya na upinzani wa kiadui anaokutana nao mtu.

Kila binadamu ana hiari ya kudhibiti taathira ya ubaya katika roho yake, vile vile anao uwezo wa kubadilisha jambo baya kuwa zuri au fikra mbaya kwa fikra nzuri na kujibu ubaya kwa uzuri. Kwa hivyo, tunaweza kupunguza nguvu za taathira mbalimbali juu ya fikra zetu kwa kutegemea nguvu za matakwa yetu, na kwa njia hiyo tukapata nguvu za kutosha kuweza kuvunja hisia ya chuki ambayo huzisumbua roho zetu. Hakuna mtu atakayeweza kutusaidia tutakapo shindwa kutekeleza wajibu wetu zaidi ya mtu binafsi mwenyewe.

Kukomoana na kuzushiana mambo yasio mazuri, kama vile vifo au uhalifu ni mambo ambayo si katika ubinadamu, watu wa namna hii ujificha katika ngozi tofauti tofauti. Baadhi ya watu huvaa ngozi za urafiki au uswahiba au kujionesha kuwa ni mpenda dini na haswa hizi zama za utumiaji wa mitandao, watu uweza kukuomba urafiki na kuwaongeza kwenye orodha ya watu utakaokuwa ukiwasiliana nao au wengine ujitia kwenye siasa na kujifanya kuwa wao ni wapinzani, kumbe ni wanafiki na kuchukuwa siri za wengine kisha kuwachongea na kwa njia hii wanaweza kuwakomoa au kuwaangamiza wengine kisiasa au kiuchumi na katika jamii kuonekana kama ni wasaliti.

Niliwahi kusoma sehemu zamani kuwa:

“Chuki na uadui ni matokeo ya upumbavu hasa panapokosekana sababu maalumu. Tunaweza kuyatatua mambo mengi kwa urafiki, lakini ubinafsi hautuachii. Hutokea mara nyingine tukavunja urafiki kwa sababu ya adha ndogo kabisa, wakati tunaelewa kwamba kosa lao ni kuwa na imani tofauti na yetu au wakati mwingie wanaunga mkono fikra tofauti na sisi. Kwa kweli, tunashindwa vipi kuvumiliana katika mustakabari wa maisha yetu na hali sote tuna haki ya kuamini na kufuata fikra tunazo amini kuwa zitatukomboa kimaisha…!?”

Watu hawa wapo tayari kupoteza muda na wakati wao na nguvu zao katika kujitengenezea maadui, uku wakijikomba kwa watu (matajiri, watawala au wanasiasa) wanao amini kuwa wanaweza kuwasaidia katika kutatua maisha yao waliyo yaharibu kwa uhalifu wao. Hali hii uendelea mpaka pale hasidi huyu atakapo fanikiwa, ingawa ni mara chache sana kufanikiwa, lakini hata atakapo fanikiwa hakumpi utulivu wowote wa nafsi na matokeo yake umpelekea kutafuta adui mwingine na mwingine mpaka kumpelekea kupata maradhi mabaya ya nafsi na kuanguka kwa aibu.

Wengi wetu tunashindwa kuelewa kuwa mapenzi ya kijamii ni sababu muhimu kabisa ya mtu kupata maendeleo na mafanikio mazuri katika maisha yake. Mtu mwenye mapenzi na watu akaishi kwa wema na upendo kiasi ndio zikawa sifa zake, basi mtu huyu anayeweza kutawala hata nyoyo za watu na kupanda ngazi ya maendeleo kwa kunufaika kwa msaada na ushirikiano wa jamii na kupata ufunguo wa mafanikio. Mtu mzuri kwa tabia na amali ni kama taa inayong’aa yenye kuongoza fikra na maendeleo ya jamii. Usafi wake wa moyo una taathira kubwa katika muundo wa maadili ya watu.

Kwa kuwa kijicho kina sura mbaya, hivyo hujitangaza chenyewe kuwa ni adui wa tabia na sifa nzuri na kizuizi kati ya watu. Kijicho hakimpi mtu fursa ya kupendwa na watu anao ingiliana nao. Hivyo, mwenye kijicho hukosa fursa za ushirikiano na neema ya mapenzi. Hasidi huonyesha waziwazi ubaya wake unaotokana na vitendo vya tabia yake mbaya, na kwa sababu hiyo hulaaniwa na huchukiwa sana na watu. Na kupelekea kupata huzuni ambazo huingia moyoni mwake kutokana na uhasidi wake, kiasi huikandamiza roho yake katika moto mkali na kuteketeza maisha yake.

Siku zote moyo wa mwenye wivu, husda na roho mbaya, daima uona uchungu na uwa hauna raha wakati wowote. Kwa sababu anaishi kinyume na imani yake, kwa sababu ya kuikataa neema za Mwenyezi Mungu hambazo hazina kikomo, hivyo uishi kwa mashaka na wasiwasi kwa sababu hiyo zile kutu za huzuni huwa haziwezi kutoka kabisa katika moyo wake mpaka anaingia kaburini.

Hali hii ya uhasidi ikishamiri katika jamii, basi upelekea migogoro na ugomvi wa kila aina. Mazingira kama hayo yanayochafuliwa na ugonjwa wa chuki na roho mbaya ya uhasidi huwa ni kizuizi mbele ya maendeleo si ya mtu mmoja mmoja tu, bali jamii kwa ujumla, hivyo kuvuruga nidhamu ambayo ni kiini cha maendeleo ya watu na kusababisha maanagamizi ya jamii hiyo akiwemo hasidi mwenyewe.

Kila mtu au binadamu ana haki ya kuheshimiwa katika jamii kwa kadiri ya heshima na hadhi yake. Mtu anayejifunga katika kuta nne za majivuno na nafsi yake ikatawaliwa na chuki, hatajali kamwe kuwaaribia wengine isipokuwa atazingatia matakwa yake tu. Kwa hivyo, atajaribu kwa nguvu zote kuwaudhi na kuwakera wengine na kujifanya mashuhuri na msifiwa, na kuilazimisha jamii imuone yeye ni bora.

Dhana mbaya ni athari isiyozuilika katika nafsi ya hasidi. Miali ya moto ya mwenye dhana mbaya ya kujiona daima huwaka na huwadhania wote kuwa ni wenye kumchukia na kumtakia mabaya.

Kudharauliwa kwake na kupata mapigo ya daima kutokana na maringo yake hakumsahaulishi kamwe ubaya wake. Bali uendelea kutafuta mbinu hizi na zile kiasi ya kwamba kichwa chake husumbuliwa na fikra zake bila ya mwenyewe kutaka. Na kila akipata fursa hutaka kuifanyia chuki jamii, na uwa hawezi kuona raha madhali machafuko na machemko ya ndani mwake hayajatulia.
Kirusi cha majivuno na maringo hutokeza katika dhamiri ya mtu baada ya kuugua maradhi ya kinafsi ya kujihisi duni. Maradhi hayo hugeuka kuwa kirusi duni ambacho kwa sababu ya kuwa kiharibifu na chauma, huenda kikawa ni chanzo cha hatari nyingi na uhalifu wa kila aina. Kirusi hiki duni humfanya mwenye kujinata afanye ukatili na udhalimu.

Mtu mwenye thamani na hadhi ya kweli hatakuwa na haja ya kujivuna au kujionyesha mbele ya watu wakati wowote ule, kwa sababu anaelewa vyema kwamba kujiona si msingi wa ubora, na roho mbaya haimfai mtu yeyote wala haimfikishi mtu yeyote kwenye kilele cha utukufu na ufakhari.

Basi nadiriki kusema kwamba, kumdharau mtu mpumbavu na kujiepusha na marumbano yasio na tija ni fimbo tosha kabisa, kwa sababu ukiingia wenye marumbano na mtu mpumbavu atakushusha hadi ufikie upeo wake wa kufikiri kijinga na kipumbavu, na kisha atataka kukugaragaza kwa upumbavu wake, na kwa sababu hana hoja, mwishoni utashindwa kuendelea naye… Lakini ukiingia kwenye marumbano ya hoja dhidi ya wasomi, ukiwashinda au wakikushinda basi utafaidika kwa elimu yao, kwa sababu wana upeo unao lingana na wewe, na hapo lazima utaondoka na faida japo mbili au tatu.

Siri moja kubwa sana ya kumuumiza mtu mpumbavu kisaikolojia ni kumdharau na kumfanya kama hayupo, yeye mwenyewe ndio atakuwa akiangaika, maana hajui umeuchukuliaje upumbavu wake.

Kila mtu ana mwendo wake maalumu unaotokana na hali yake ya kimaadili na kinafsi. Msamaha ni mojawapo kati ya sura angavu kabisa ya utukufu na udhibiti wa nafsi, na ni aina moja ya ushujaa na uungwana. Mwenye kuwa na sifa hiyo kwa kadiri ya kutosha na mbali ya kuwa na nguvu na uwezo wa kulipiza lakini akasamehe, hufaidika kwa kuwa na uhakika na usafi wa moyo ambao hauwezi kulinganishwa na kitu chochote kingine. Kusamehe kunaitukuza na kuiimarisha roho ya mtu, na ni kipawa ambacho kwacho hububujika upole na wema. Kusamehe humtoa mtu kwenye kifungo cha ubinafsi. Ingawa ni shida sana kusahau madhara na mabaya ya wengine na moyo huumia sana mwanzoni, lakini kwa kadiri mtu atakavyovumilia katika njia hiyo ndivyo atakavyoweza kupunguza sana masumbufu yake ya rohoni na mwisho wake akawa ni mtu msamehevu na aliye bora kabisa katika jamii.

Hapana shaka kwamba kusamehe kunaweka athari nzuri katika moyo wa adui kwa kadiri kwamba uweza kuleta mabadiliko katika fikra na mwendo wake. Chuki nyingi zimeondoshwa kwa kusamehe, na uadui mkali na wa kizamani umeondoshwa na mahali pake kukaa usafi wa moyo na upendo. Adui mchokozi hulainika na husalimu amri mbele ya mtu aliyejizatiti kwa silaha hii kali na kwa fikra za kiungwana.

Jambo la kuzingatia:
Kimojawapo kati ya vipawa vikubwa kabisa vya binadamu ambavyo wanyama wengine hawakufaidika navyo ni hisia ya kusamehe makosa ya wengine. Mtu anayekuudhi huwa kwa wakati huohuo hukupa fursa nzuri ya kumsamehe na kuona utamu wake. Tumefunzwa kuwasamehe maadui zetu lakini hatukuambiwa tusiwasamehe marafiki zetu. Hivyo, ni wazi kwamba ni lazima tusahau mabaya tuliyotendewa na wengine. Unapomlipizia kisasi adui wako huwa ni sawa naye, lakini unapomsamehe wewe huwa ni bora kuliko yeye, kwani yeye huwa ni mwovu, nawe huwa ni msamehevu. Huenda tusifanikiwe tunapotaka kulipiza kisasi, lakini kusamehe ni njia bora kabisa ya kulipiza kisasi. Kwa kusamehe tunaweza kuwashinda maadui zetu bila ya kupigana na kuwafanya wainamishe vichwa vyao mbele ya utukufu wetu. Kwa hivyo, kuacha chuki na kukwepa uadui ni shambulio kubwa kabisa lenye kuwashinda mahasimu wetu. Tunapotendewa maovu, tuwatendee mema, kwani kulipa mema kwa mabaya uliyofanyiwa ni siasa ambayo kwayo hupatikana amani duniani.”

By Yericko Nyerere